Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

"Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo kikuu cha Dar es salaam si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma"

☆☆Prof. Kitila Mkumbo. ITV 2016/4/17☆☆
 
Kwani huyu Kitila si ndo yeye leo kateuliwa mbona hajakataa??
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Achana kabisa na kitu inaitwa STOMACH.
 
Mbona nasikia ameukataa uteuzi?,amemshukulu tu mh Rais..ameomba nafasi hiyo apewe mtu mwingine.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Subirini 'mchambo' wa Mkuu kesho kwenye kuapishwa
Mange Kimambi cha mtoto
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Naona analipwa fadhila, alikuwa mdau mkuu wa kudhoofisha upinzani sambamba na Zito!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima

Hii ni raha ya JF. Kufukua makaburi! Je atakata ukatibu ili kuonyesha uzalendo kwa Nchi yake? Au eti Ukatibu siyo mambo ya Siasa?
 
Back
Top Bottom