Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Ile sheria ya watumishi wa umma kutojihusisha na masuala ya siasa hasa ya kiuongozi haimuhusu huyu jamaa?
Brother ile sheria haitumiki utawala huu,ndio maana Kuna mapolis wamekuwa makatibu tawala na wanajeshi wamekuwa wakuu wa mikoa na wilaya na Mwanajeshi mstaafu wa mwaka mmoja amekuwa kiongozi wa ccm na wapo mbele kukitetea chama tawala na siserikali iliyopo madarakani.

Tukumbuke rais anatekereza ilani ya chama cha mapinduzi kwahiyo wateule wake wote watatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.
 
Zaidi ya kupunguza idadi ya wahadhiri vyuoni, uteuzi wa wahadhiri kujaza nafasi mbalimbali serikalini una athari nyingine muhimu na mbaya zaidi:

1/ Unafanya wahadhiri kuwa sycophants, kila mmoja akijaribu kujiweka kwenye nafasi ya kuteuliwa. Academic freedom imewekwa rehani.

2/ Kufuatia namba (1) hapo juu, tafiti na ushauri wa wahadhiri sio critical kabisa. Hivyo, zinafanywa tafiti kwa jina la sayansi lakini kumbe watafiti hawako tayari kufanya tafiti au kutoa matokeo yatakayowaudhi watawala. Kazi inakuwa ni kusifia serikali. Hiyo si sayansi.

3/ Wahadhiri wengi walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali hawana uzoefu wa kutosha unaoendana na hizo nafasi. Hivyo kama taifa, hasara ni kubwa kwa kuwa wengi wao hawataleta matokeo au maboresho tarajiwa. Ni bahati mbaya sana kuwa mamlaka ya uteuzi inaamini/imekariri kuwa mtu akishakuwa na PhD basi anaweza kuongoza mashirika yanayopaswa kuendeshwa kwa faida, hata kama uzoefu pekee alionao mhadhiri anayeteuliwa ni kuongoza idara mojawapo huko chuo kikuu.
 
with thousands of fresh graduates every year, a reasonable number of them qualifying for lecturing at universities i do not see any problems

You are missing the point. And a "reasonable number of them" DO NOT "qualify for lecturing at universities". Wamekariri tu kwa kuwa wanaopaswa kuwaongoza/mentor wameteuliwa kushika nafasi mbalimbali serikalini. The future of higher education in Tanzania is in tatters.
 
Mwendelezo wa kuua elimu nchini kwa kuteua wahadhiri kila kukicha na kusababisha vyuo vikuu nchini kuwa na uhaba mkubwa wa Wahadhiri.

Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
 
Yupo sahihi kuna majembe wameondoka CoET/UDSM pale hatari.Prof Rubaratuka bingwa wa indeterminant structures, Dr chamuliho Construction manegement, Dr Mwinuka jembe la mechancal, Prof Lema daaah ni hatari sana
Dr.Abdala Posi from UDOM dah tume kumis sana
 
Kabla ya uteuzi hupigiwa simu kuulizwa kuwa wapo tayari au lah!
Wakatae kwanini wakati waalimu hawaheshimiwi tz na njia rahisi wao kufanikiwa ni kuwa wanasiasa.
 
Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima

Wacha ELIMU ife kabisa,mbona watoto wetu tunawapeleka UGHAIBUNI nyie bakini na majengo tu.
 
Kwani hivyo vyuo havina SUCCESSION PLAN? Haviandai watu wa kushika nafasi iwapo mmoja akiondoka aliye chini apande? Hivyo vyuo vina tabia ya one man show kwenye vitivo ?
Kaka YEHODAYA Vyuo vyote vina SUCCESSION PLAN lakini hakuna budget kwa ajili ya implementation. Nipo Chuoni ndio hali halisi. Government haitoi fedha za kuendeleza walimu/wahadhiri mpaka muombe kwa wafadhili hasa SIDA ndio mwokozi. Vyuo vina kila kitu katika mpango kazi mtambuka ila tatizo hakuna fedha. mapato tunayopata ya ndani ndio matumizi makubwa ya kuendesha Chuo na hayatoshi maana OC haziletwi kabisaa ama unaletewa 20% ya ulichoomba ni shiida sana.
 
Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
Mi namshauli Raisi atazame na vyuo vingine kama University of Iringa, University of Arusha, Tumaini, TEKU, SAUT, St. Joseph, nk.
 
Naunga mkono hoja, anaathiri wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kukosa wahadhiri. Chuo kikuu Dar ndicho kinachoathirika zaidi maana wahadhiri wengi wameteuliwa. Idara iliyoathirika zaidi kwa teuzi ni ile ya kemia UDSM.
Wakemia wengi ni mbumbu kwenye uongozi huwaga hawafiki mbali
 
Kwani hivyo vyuo havina SUCCESSION PLAN? Haviandai watu wa kushika nafasi iwapo mmoja akiondoka aliye chini apande? Hivyo vyuo vina tabia ya one man show kwenye vitivo ?
One man show ndo kusemaje
 
Kweli kabisa halafu huko wanakoenda hawaonekani wakiutumia utalaamu wao.

Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
 
Naunga mko. Kazi ya wahadhili ni kutengeneza wataalam wakuja kufanya kazi huko kwingine. Sasa kama watengeneza wataalam wao ndio sasa wanachukuliwa nani atatuandalia wataalam.

Mbaya zaidi wanachukuliwa watu waliowiva kitaalum kutengeneza vijana wetu. Huku ni shida. Maana kuja kumtengeneza mtu kufikia hiyo level sio kazi ndogo. Kwa hili rais wetu ajitafakari upya.
 
Zaidi ya kupunguza idadi ya wahadhiri vyuoni, uteuzi wa wahadhiri kujaza nafasi mbalimbali serikalini una athari nyingine muhimu na mbaya zaidi:

1/ Unafanya wahadhiri kuwa sycophants, kila mmoja akijaribu kujiweka kwenye nafasi ya kuteuliwa. Academic freedom imewekwa rehani.

2/ Kufuatia namba (1) hapo juu, tafiti na ushauri wa wahadhiri sio critical kabisa. Hivyo, zinafanywa tafiti kwa jina la sayansi lakini kumbe watafiti hawako tayari kufanya tafiti au kutoa matokeo yatakayowaudhi watawala. Kazi inakuwa ni kusifia serikali. Hiyo si sayansi.

3/ Wahadhiri wengi walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali hawana uzoefu wa kutosha unaoendana na hizo nafasi. Hivyo kama taifa, hasara ni kubwa kwa kuwa wengi wao hawataleta matokeo au maboresho tarajiwa. Ni bahati mbaya sana kuwa mamlaka ya uteuzi inaamini/imekariri kuwa mtu akishakuwa na PhD basi anaweza kuongoza mashirika yanayopaswa kuendeshwa kwa faida, hata kama uzoefu pekee alionao mhadhiri anayeteuliwa ni kuongoza idara mojawapo huko chuo kikuu.
Umezungumza ukweli. Wasomi wengi sasa ni kusikia na kuongezana ili huyo aliyeteuliwa amkumbuke angalau hata ujumbe wa Bodi.
 
Hata mimi naunga mkono hoja,kwani upungufu upo kabla hata ya hizi teuzi sasa sipati picha baada ya teuzi uhaba wa wahadhiri umefikia kiwango gani
 
Back
Top Bottom