Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Yetu macho tukisubiria mkumbo akatae uteuzi ili kusimamia kauli yake yakupinga wahadhiri kuteuliwa teuliwa hovyo.
 
Wana jamvi Salaam

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
Mungu ibariki JF
 
Nakumbuka alisema hivi:

*"Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo kikuu cha Dar es salaam si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma
"*- Prof. Kitila Mkumbo. ITV 2016/4/17

Lakini Prof Kitila ni mtumishi wa umma,kupandishwa cheo toka Uhadhiri mpaka Ukatibu Mkuu ni "promotion" as far as he is a civil servant.

Zenobius,Mwanafalsafa wa Uyunani aliwahi kusema miaka hiyoo hata kabla ya Afrika kuwa hivi ilivyo.Zenobius alisema "Kila uchwao,kituko kipya huzaliwa Afrika"
 
Acha ubishi wa kijinga unaweza kuwa na madarasa bora kama huna wakufunzi ni bure, lakini ukiwa na wakufunzi bora hata chini ya mwembe elimu inapatikana

Ukibishana na mjinga nawe mjinga. We unadhani Kitila akiondoka chuo ndio wlimu imekufa? Walikuwepo walimu mahiri kina Prof Shivji, nani angedhani law school ingesurvive bila wao?! Acha mawazo ya kijima.
 
Mhadhiri Muandamizi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo amemshauri Mh Rais Magufuli aache kuteua Wahadhiri katika nafasi za kisiasa ama majukumu mengine kwa kuwa vyuo vikuu vimeanza kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri baada ya wengi wao kupewa teuzi mbalimbali.

Aidha Prof Kitila amesema vyuo vikuu vilivyoathirika zaidi baada ya wengi wa wahadhiri wake kuteuliwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Chanzo: Tanzania Daima
Prof Kitila: Magufuli usiteue Wahadhiri

Swali:
Atalamba matapishi yake au?
Unakumbuka mtu anaitwa Humphrey Polepole? Alikuwa ni mpingaji mzuri wa vyeo vya ukuu wa wilaya na mikoa. Alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya alisahau kila kitu na akakubali hicho cheo alichokuwa anakipinga. Tusubiri Mkumbo atakuja na lipi. Binadamu wanabadilika, tena kwa kasi ya ajabu!
 
Back
Top Bottom