Kwanza kabisa nampongeza Prof Kitila kuteuliwa na raisi ktk nafasi hiyo.
Pili nampongeza raisi kwa kuzingatia elimu ktk teuzi zake.
Tatizo kubwa naloliona ni misuse of resource pamoja na mislocation of resource.Teuzi nyingi za mh, raisi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa Mkumbo zimepelekea matumizi mabaya ya rasilimali watu.
Mfano, Prof Kitila ni miongoni wa wataalam wachache wa saikolojia ya binadam waliokuwa wamebaki pale UDSM lakini naye amepelekwa akaoneshe saikolojia yake wizara ya maji na umwagiliaji.
Akiwa wizara ya maji kama mtendaji mkuu atalazimika kutegemea ushauri na maelekezo ya wahandisi wa maji waliopo pale wizarani ktk kutoa maamuzi yoyote kwakuwa yeye si mtaalam ktk fani hiyo.Hili likitokea tayari tutakuwa tumeshindwa kumtumia vizuri ktk utaalam wake
Mbaya zaidi wengi wa wataalam hawa tuliwasomesha kwenye fani hizo kwa kodi zetu.Kuna mlolongo mrefu wa wataalam ambao tuliwasomesha ktk fani zao kwa pesa nyingi lakini tunawatumia ktk nafasi ambazo haziwezi kuleta manufaa mapana kwa taifa.Wengi wao wanatumika ktk siasa huku kule kwenye fani zao kukiwa na upungufu mkubwa wa wataalam,hivyo wananchi kukosa huduma muhimu.
Mfano kuna upungufu mkubwa wa madaktari wa binadamu na wahadhiri wa vyuo vikuu huku tukiwatumia wataalam hao ktk mambo yasiyo na maslahi mapana ya kitaifa kama orodha hii inavyoonesha;
Prof Kitila Mkumbo-maji na umwagiliaji
Dk Mwakyembe-habari,wasanii na utangazaji
Dk Hussein Mwinyi-ulinzi na jeshi la kujenga taifa
Dk Bilali- makamu raisi mstaafu
Orodha ni ndefu sana sitaweza kuimaliza.wataalamu hawa na wengine waliobobea tumeshindwa kuwatumia ipasavyo na badala yake tunawatumia vibaya kwa maslahi binafsi.
Kiufupi uteuzi waProf Kitila ni mwendelezo wa misuse of human resources
Ushauri; Serikali iboreshe maslahi ya watumishi wote wa umma.Kipaumbele ktk maslahi kiwe ktk kazi za kitaalam kama wahandisi,walimu,madaktari wa binadam na nyanja nyingine za kitaalam
Hii itasaidia wataalam wetu kujikita ktk taaluma zao badala ya kukimbilia siasa na teuzi mbalimbali.