Prof Haroub Othman na Shivji ni wachochezi?

Gamba La Nyoka:

Upo sahihi unaposema kwamba:

Bwana Mchambuzi:
Ukweli ni kwamba Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM mara tu alipong'atuka mwaka 1985, kwa hiyo notion ya kudai kwamba masuala mengine ya azimio la arusha waliyaua kimya kimya as if Mwalimu hakushiriki fully vikao vya Chama, mwaka 1986 si ya kweli!.

Mwalimu aliendelea na uenyekiti wa CCM taifa mpaka mwaka 199 alipojiuzulu – two years before msiba wa Azimio la Arusha. Lakini ni muhimu rekodi iwekwe katika mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na haya:

Kuna makala by Biermann and Wagao, (1987), titled "The IMF and Tanzania" – A Solution to Crisis? - Waandishi hawa wanazungumzia hali ya majadiliano yaliyojiri wakati ule baina ya Serikali na IMF.

["During the negotiations, the IMF maintained that Tanzania change its economic policies by reducing the role of the state in the economy in order to give room for market forces to operate freely. Tanzania rejected this condition as a matter of principle: that it was totally unacceptable for the IMF to meddle with its economic policies."]

Huu ulikuwa msimamo wa Mwalimu, hata pale alipobakia na kofia ya Uenyekiti wa CCM (1985-1990), and he was opposing IMF, ndani ya vikao, lakini vievile publicly, kufikia hatua ya kuulizia, tangia lini IMF stands for INTERNATIONAL MINISTRY OF FINANCE? Mengi sana yameandikwa kuhusu vita vya Mwalimu ndani ya Chama kupinga masharti ya IMF.

In another article by Andrew Kiondo in Mid 1980s, Khigoma Ali Malima, is quoted arguing:

["Indeed any attempt to control the prices of such imported goods has been resisted not only by the domestic business interests concerned but also their spokesmen in the party and government. There is also some indication that liberalization has led to an increase in the smuggling of our commodities, outside the country, as the scramble for dollars to import commodities which no one can afford amounts. Yet, despite all this glaring evidence, the IMF and the World Bank and their domestic supporters are counseling more and not less liberalization."]

Malima alikuwa karibu sana na Mwalimu katika vurugu zile za SAPs. Maneno ya Malima, mbali ya kuelezea uhalisia ule, pia ni reflection on jinsi gani Mwalimu bado alikuwa anapingana na hali iliyojitokeza. Swali la Msingi ni Je, Ni kitu gani kilikuwa kinamshinda Mwalimu kubadili hali ilivyokuwa inaendelea, huku akiwa na kofia ya Mwenyekiti wa CCM Taifa

Kiondo anaendelea kutuelezea:

["One thing to note here is that the economic reforms and the agreement were all taking place at a time when the ruling party (CCM) had greatly been weakened in its mobilization capacity. Furthermore, as noted above, by this time, forces of liberalization had already gained support in the party and state. This leads to a conclusion that the political character of the state is gradually changing as the politically dominant, economic actors change as well."]

Gamba La Nyoka, kama unavyoelewa, hakuna mtu mwenye nguvu kama Chama, Chama ni Watu, sio mtu mmoja mmoja. Kwahiy, Mwalimu hakuwa na la kufanya zaidi ya kujiuzulu mwaka 1990 ili kuwapisha ‘wenye nguvu' waendeshe mambo yao –, kwa lugha aliyokuja tumia Mwalimu baadae… "kwa kuacha ya maana na kuchukua ya kijinga, unlike yeye ambaye ali admit kwamba alifanya ya maana na ya kijinga".

Pia niliahidi kukurudia kuhusu your questioning of Equality notion/Usawa in the context of Azimio La Arusha. Binafsi nadhani professor Shivji anatusaidia vizuri zaidi kutupa msingi jinsi gani tuukabili huu mjadala, pale anaposema kwenye article yake titled: Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa (2000):

["The theoretical or conceptual building blocks of the new consensus should be the notions of social justice and equity as opposed to the notions of natural justice and equality. The ideas of equality and natural justice are the foundations of liberal/bourgeois political doctrines, jurisprudence and theories of right" (here Shivji also refers to: Cormick and Bankowski ‘1989', Enlightenment, Rights and Revolution: essays in legal and social philosophy….'). Shivji continues "The right ideology built around the concept of equal rights (Dworking 1977, Pashukanis 1978), as I have argued elsewhere, has little resonance in the popular consciousness besides being obviously inequitable and unjust (Shivji, 1995). As it has been said, equality among Unequals is Inequitable. I have no time here to go into details, but I have shown elsewhere, the notions of Usawa and Haki in the ideology of Ujamaa, for example, are closer to notions of Justice and Equity rather than equal rights."]

Pia kuna issue uliyo raise last time, and I quote:

Kama chama kinaona mambo ni ya Msingi basi kiyatungie sheria, au kiyaingize katika katiba kupitia bunge la Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, badala ya kubaki kama Maazimio, kwa maana katika nyakati hizi Chama hakishiki hatamu siyo kama enzi zile!

I second you on that point.

Lakini unaposema:

Narudia kusema, Azimio la Zanzibar halikuua azimio la Arusha bali lililiboresha!- Muda ulikuwa umefika wa kwenda na wakati, mambo ya Viongozi kutokuweza kupangisha Nyumba zao yalikuwa yamepitwa na wakati!, na Azimio la Zanzibar ndilo lilikifanya.

Ni yepi hayo yaliyoboreshwa ambayo yanakuwa practiced leo kwa manufaa ya watanzania milioni zaidi ya 30 out of the total 45 million (i.e 70% waliopo in rural areas)? Ningependa sana kuyafahamu in 2011.
 

Mwl Nyerere was behaving like a substitute player after retirement in 1985. You always see the opportunity of scoring and change the game plan when you are watching it but you get lost when you are actually on the pitch.

It is true that hope was the best weapon to maintain peace and Nyerere knew it, he knew that as more and more Tanzanians get educated and more and more educated Tanzanians lost their hopes after graduating without having employment of their dream, they will start to use their education educating others that there was no hope then, there is no hope now and there will be no hope in the future. The best hope he saw was to change country's leadership to revive the hopeless hopes of Tanzanians. When you in the same party change country presidents to 2, 3, 4 and still there is no hope for the hopeless Tanzanians. People will lose hope for the party, once people lose faith for the party in order to revive their hopes; the only remaining option is to change the party in power.

If CCM is smart enough to know this, it will not force to remain in power to coerce the hopeless Tanzanians. A hopeless individual does not value life or death, and when that happens which is happening now, there will be no fear, and that is where Mwalimu Nyerere player's substitute mind will bear fruit and materialised sooner or later(2015). The best way to preserve hope which is done everywhere in the way is to let people choose whoever they think will recharge the hope minds.

The current CCM moguls should learn that, we should not wait reconciliatory actions after some of them are summoned to The Hague. They should let people choose their leader and not force them a leader using Police and military equipment to oppress the hopeless people. Nyerere's philosophy will be proved right.

I second you 150%, but we should all agree that, neither CCM nor CHADEMA forinstance can restore that under the current circumstances and policy frameworks -; not even in 2015 and beyond because they both fail to understand that they have a common enemy, regardless of the party lines: The meddling of our development policies by the IMF and WorldBank with our consent, in the context of unfair participation of our rural mass in the so called 'free market"; And it is for the same reasons that if CHADEMA, or whoever manages to beat CCM in 2015, that party will shortly find itself in the verge of loosing to CCM or whoever in 2020 or not far from 2020; Otherwise, the truth remains that - Mwalimu made maskini live in Hope, but Soko Huria is making the same maskini live in 'despair';

CCM, CHADEMA, and other political parties - it is about time they realize that - the market doesn't count heads, it counts dollars; it favours the rich and powerful and not the miserable many just because of their numbers; and it is the miserable many that Mwalimu seems to be calling them into action;
 
Gamba la Nyoka,

Kwahiyo hoja yako hapa ni sustainability of the leadership code as time went by au ni kwamba haikuwa practical from the outset? So should i understand your argument as the code was great at the outset given the socio-economic conditions of the time but it had to be adjusted kulingana na socio-economic changes za nchi? kama nipo sahihi, kimsingi nakubaliana na wewe, lakini nabakia na swali moja kwamba, je: Adjustments for who? (rejea majibu/hoja ya mwalimu kwa viongozi waliokuwa wanapinga the code in 1967);

Hoja yako kwamba Mwinyi argued kwamba kilichotokea zanzibar ni kuliokoa Azimio La Arusha, na sio kuliua, swali langu ni je, kuliokoa limsaidie nani? Leo hii, in practice, What content of the declaration ipo katika hali ya wokovu leo in the eyes of the 70% of the population? Kwa mawazo yangu, ambayo yanaweza kuwa finyu sana, azimio la znz ndilo chimbuko la ufisadi kwani halikuweka masharti, mipaka wala muongozi, na hilo linachangia sana to justify utajiri wa viongozi wetu leo hii uendelee bila kuhojiwa. Na hoja yako kuhusu kuweka haya mambo kikatiba na kisheria, naiunga mkono mia kwa mia;

Lakini jibu lako kuhusu swali from mwanakijiji to you kwamba: Maskini could claim ownership on Azimio La Arusha, but ni viongozi tu who can claim ownership to azimio la Zanzibar, i think stands very well; majibu yako juu ya hili kidogo yamekuwa yakuzunguka, something which i can totally understand, and we don't have to explore it further;

Kuhusu population ya dar-es-salaam, inawezekana tunasoma sources tofauti, my source is: Worldbank Tables 1971; na pia a book titled The Crisis in African Agriculture, By Mohamed Lamine Gakou, kuna a chapter on Tanzania.

Pia ni muhimu tukatambua as of today, about 1/3 of the urban population in Tanzania is in Dar, na hali ilikuwa tofauti zaidi miaka ya nyuma where almost 3/4 of urban population in Tanzania was in Dar. So whether tutumie source yako au yangu, suala la msingi hapa ni kwamba when we talk of Tanzania, Tanzania then ilikuwa ni vijiji na sasahivi bado ni vijiji.
 
"Ni yepi hayo yaliyoboreshwa ambayo yanakuwa practiced leo kwa manufaa ya watanzania milioni zaidi ya 30 out of the total 45 million (i.e 70% waliopo in rural areas)? Ningependa sana kuyafahamu in 2011.

Aziomio la Zanzibar halikuboresha Azimio la Arusha bali lilifuta; miiko yote ya uongozi iliondolewa na viongozi wakapata mwanya wa kujilimbikzia mali kwa kutumia nafasi zao za uongozi. Kama azimio la Zanzibar lilitaka kuboresha Azimio la Arusha wasingeondoa miiko ya uongozi bali wangewawekea checks viongozi kuwa kama walikuwa na mali walizopata kihalali [ they were supposed to declare their properties annually]wangeziweka kwenye TRUST wakati wote ambao wangekuwa viongozi na kwa kufanya hivyo viongozi wasingejihusisha na biashara zao [ hence avoiding conflict of interst] mpaka hapo uongozi wao utakapokoma. Naamini kwa kuweka hizo checks juu ya viongozi Azimio la Zanzibar lingeboresha Azimio la Arusha!
 
Aziomio la Zanzibar halikuboresha Azimio la Arusha bali lilifuta; miiko yote ya uongozi iliondolewa na viongozi wakapata mwanya wa kujilimbikzia mali kwa kutumia nafasi zao za uongozi. Kama azimio la Zanzibar lilitaka kuboresha Azimio la Arusha wasingeondoa miiko ya uongozi bali wangewawekea checks viongozi kuwa kama walikuwa na mali walizopata kihalali [ they were supposed to declare their properties annually]wangeziweka kwenye TRUST wakati wote ambao wangekuwa viongozi na kwa kufanya hivyo viongozi wasingejihusisha na biashara zao [ hence avoiding conflict of interst] mpaka hapo uongozi wao utakapokoma. Naamini kwa kuweka hizo checks juu ya viongozi Azimio la Zanzibar lingeboresha Azimio la Arusha!

*******************
Bulesi,


Ni sahihi kabisa , uboreshwaji wa azimio la arusha ungelenga hayo hayo - otherwise, azimio la zanzibar ni la watawala, unlike azimio la Arusha ambalo lilikuwa ni la wanyonge; inaniumaga sana unapopita kwenye kata na vijiji na tarafa na kukutana na wazee kwa vijana, wale makada wa CCM, wakiwa wanaelekea kwenye mikutano ya chama wakiwa wamebeba azimio la Arusha lile lenye rangi ya kijani na nyeusi on the cover (kwani kuna version mpya toka Kigoda Cha mwalimu, same content, different cover); huwa nabaki kujiuliza, isnt this the timing bomb as well? maana unakuta vijana wa UVCCM wanatimua vumbi kwa shangwe kuwapokea wakubwa toka makao makuu na kuwaimbia viongozi waliokaa meza kuu:

KAULI YETU NI KULINDA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA;


Na viongozi hawa wanatabasamu na kuwapigia makofi. Huwa naishiwa na nguvu kabisa, na kubakia kuwaza tu kwamba, kama kweli Vijana wanataka kulinda hayo, they should take action, not just rhetoric; ila sijasema action ambayo anaizungumza mwalimu in my original post, maana nisije kuitwa mchochezi;
 
Aziomio la Zanzibar halikuboresha Azimio la Arusha bali lilifuta; miiko yote ya uongozi iliondolewa na viongozi wakapata mwanya wa kujilimbikzia mali kwa kutumia nafasi zao za uongozi. Kama azimio la Zanzibar lilitaka kuboresha Azimio la Arusha wasingeondoa miiko ya uongozi bali wangewawekea checks viongozi kuwa kama walikuwa na mali walizopata kihalali [ they were supposed to declare their properties annually]wangeziweka kwenye TRUST wakati wote ambao wangekuwa viongozi na kwa kufanya hivyo viongozi wasingejihusisha na biashara zao [ hence avoiding conflict of interst] mpaka hapo uongozi wao utakapokoma. Naamini kwa kuweka hizo checks juu ya viongozi Azimio la Zanzibar lingeboresha Azimio la Arusha!

*******************
Bulesi,


Ni sahihi kabisa , uboreshwaji wa azimio la arusha ungelenga hayo hayo - otherwise, azimio la zanzibar ni la watawala, unlike azimio la Arusha ambalo lilikuwa ni la wanyonge; inaniumaga sana unapopita kwenye kata na vijiji na tarafa na kukutana na wazee kwa vijana, wale makada wa CCM, wakiwa wanaelekea kwenye mikutano ya chama wakiwa wamebeba azimio la Arusha lile lenye rangi ya kijani na nyeusi on the cover (kwani kuna version mpya toka Kigoda Cha mwalimu, same content, different cover); huwa nabaki kujiuliza, isnt this the timing bomb as well? maana unakuta vijana wa UVCCM wanatimua vumbi kwa shangwe kuwapokea wakubwa toka makao makuu na kuwaimbia viongozi waliokaa meza kuu:

KAULI YETU NI KULINDA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA;


Na viongozi hawa wanatabasamu na kuwapigia makofi. Huwa naishiwa na nguvu kabisa, na kubakia kuwaza tu kwamba, kama kweli Vijana wanataka kulinda hayo, they should take action, not just rhetoric; ila sijasema action ambayo anaizungumza mwalimu in my original post, maana nisije kuitwa mchochezi;[/QUOTE]

Umoja wa vijana wa ccm wa leo sio ule wa zamani enzi ya mwalimu; wale wa siku hizo walikielewa chama na malengo yake ya kuwahudumia wananchi kwa ujumla wao. Hawa unaowaita makada vijana wa ccm wa siku hizi hawakielewi chama chao kwani wanaongozwa na tamaa ya pesa na ndio maana imekuwa rahisi kwa mafisadi kuwatumia kwa malengo yao ya kisiasa ;hivyo vitabu vya kijani na rangi nyeusi wanavyobeba sidhani kama hata wamesoma yaliyoandikwa humo. Siwalaumu hawa vijana kwa umbumbumbu wao kwani system ndiyo inataka wawe hivyo!!
 
Umoja wa vijana wa ccm wa leo sio ule wa zamani enzi ya mwalimu; wale wa siku hizo walikielewa chama na malengo yake ya kuwahudumia wananchi kwa ujumla wao. Hawa unaowaita makada vijana wa ccm wa siku hizi hawakielewi chama chao kwani wanaongozwa na tamaa ya pesa na ndio maana imekuwa rahisi kwa mafisadi kuwatumia kwa malengo yao ya kisiasa ;hivyo vitabu vya kijani na rangi nyeusi wanavyobeba sidhani kama hata wamesoma yaliyoandikwa humo. Siwalaumu hawa vijana kwa umbumbumbu wao kwani system ndiyo inataka wawe hivyo!!

Kimsingi, hawa ndio wanatakiwa wawe mstari wa mbele kuyalinda yale ya mwalimu ambayo bado yana manufaa kwa taifa hili, ndio maana hata kwenye katiba yao UVCCM, hilo la kulinda siasa ya ujamaa na kujitegemea, kama lengo na kauli yao kuu, bado lipo; Cha kusikitisha sasahivi wanakuja na kauli za ovyo ovyo kwamba wazee wapishe vijana, wapishe kwenye yepi? ni dhahiri CCM haina dira, na cha kuiokoa ilikuwa ni UVCCM, lakini na yenyewe mbali ya kutokuwa na dira, haina fahamu;
 
Bulesi,
Naona kidogo tunachanganyana kwenye quotes za mjadala wetu, hazileti mtiririko mzuri.
 
Hapajakuwa na jema na haitatokea lilijema litakalofanywa na serikali hii kwa watanzania. Ni janga la kitaifa,
 
Mi nawashangaa hata hawa watu wa vyama vingine wanaoendelea kwenda iKULU kutoa maoni, wakati jamaa alishakuwa stiff-necked!..Haambiwi, haelewi hasikii wala hakamati network yoyote!
 
Bulesi,
Naona kidogo tunachanganyana kwenye quotes za mjadala wetu, hazileti mtiririko mzuri.

Suala hapa nadhani ni substance, wale wanaotaka kuelewa kilchoandikwa kwa mtiriiko huu watafanya hivyo na wengine have resigned not to understand until there is divine intervention!!
 
Dunia hii itashuhudia result ya kiburi cha JK na CCM yake siku si nyingi... Tanzania maskini kipindi hicho utakuwa unerudi nyuma kimaendeleo na East Africa yote itakuwa Juu yako... Nasikitika kusema tutakumbuka Shuka asubuhi .... Naomba maisha marefu kwa JK ili aweze kushuhudia matokeo ya kiburi chake na kizazi kijacho kiweze kumhukumu
 
Suala hapa nadhani ni substance, wale wanaotaka kuelewa kilchoandikwa kwa mtiriiko huu watafanya hivyo na wengine have resigned not to understand until there is divine intervention!!

Ok. Hivi, kwa mtazamo wako, UVCCM - do they still have a role to play kusaidia rekebisha hali tete iliyopo in the context of what we are discussing about? Ila iwapo una mtazamo kwamba they still have a role to play; kama unaona they cant, who can - kitaasisi? ukitilia maanani kwamba taifa hili sasa ni la vijana - 50% ni watoto under 15, about 70% ni vijana miaka 30 kushuka chini mpaka watoto; almost 80% ya watanzania hawajavuka miaka 40...
 
haya mambo ya katiba mimi yananiboa sasa,kwa nini tunapoteza mda kumshauri jk ambaye ashaonekana hataki kusikia la mtu.Tuje na wazo mbadala mfano atakapotangaza hiyo tume watu twende barabarani.Apart from that tutulie tu tusubiri hiyo katiba mpya kwenye cover page tu.
 
Gamba La Nyoka,
Mkuu wangu nadhani unajiumiza kichwa mwenyewe kwa kufikiri vitu ambavyo majibu unayo lakini unashindwa kuyaweka panapostahili ni kama vile umepewa hesabu za multiple choice ukaulizwa:- 2+2 = (a) 3, (b)4, (c)5 na (d) Hakuna kati ya hayo...

Sasa wewe unaanza kuchambua nini dhumuni la hesabu hii na kadhalika. Mkuu Azimio la ARUSHA ni Azimio kama lilivyokuwa na maana yake usitake kulitunguia ushahidi mwingine, na siku zote azimio linawekwa ili kupambana na kitu fulani iwe tumeazimia leo kupambana na Kipindupindu lazima litakuwa na mwisho wake tukisha dhibiti maradhi hayo na kinafuata ni kuweka kinga lakini hatuwezi kuendelea kuweka kambi za karantini kwa waathirika hali tumefanikiwa..

Azimio la Arusha lilikubaliwa kutokana na hali halisi - Ujinga, Umaskini na Maradhi ndivyo tulivyokuwa tukivipiga vita na hapakuwa na njia bora zaidi ya kuweza kupambana na vitu hivi bila kujitoa mhanga na ktk kuandaa nguvu ya kupambana na vitu hivi ndio kuzaliwa kwa Azimio hilo. Yes, linaweza lilikuwa na makali kupita kiasi lakini ni kipimo gani ulichotumia?

Hayo uloandika hapo juu kwamba viongozi ni sehemu ya raia halina ubishi, na kweli majukumu waliyopewa ni sehemu ya mgawanyo wa kazi lakini haindoi miiko kwao kwa sababu tu ni sehemu yetu...wadhungu wanasema - U can't have a cake and eat it too! halafu unachanganya vitu unaposema hivyo kwa sababu kama wao watafanya tunayoyafanya sisi kama raia huoni kama wao watakuwa wameacha jukumu la kuongoza na kufanya kazi ambayo ni jukumu letu?

Na ndio tunarudi ktk Ubepari, kwa nini Ubepari unasisitiza serikali kutoshiriki ama kuhodhi na kuendesha uchumi bali kazi yao iwe kutunga na kusimamia sheria na taratibu za uzalishaji hii ndio miiko yake, lakini ktk Ujamaa unatakaa miiko hiyo kwa kutazama Ubepari unaruhusu nini na kwa mipaka ipi bila hata kuzingatia kwamba mambo mengi sana tulochukua ktk Ujamaa yalitokana na hali halisi na ubepari ndio ulitufikisha pale. Wenye utajiri wetu wote walikuwa walowezi sasa unaendelewa kutawaliwa kiuchumi kwa sababu umebadilisha sura Ikulu..

Nitakupa mfano mdogo sana.. Tulipopata Uhuru tulikuwa na wasomi wachache sana na pengine naweza kusema hata wanasiasa wenyewe ilikuwa kwa kuokoteza - Hii ndio sababu ilotufanya tuchague Wabunge na hao hao wawe tena mawaziri maana hatukuwa na wigo kubwa la kuchagua watu.. Sasa Mbunge tayari ni waziri unataka tena awe mfanyabiashara wakati kazi tulizowapa tayari ni kubwa na haikutakiwa iwe hivyo...Hii kweli ni kugawana kazi ama kupeana ulaji...mkuu Azimio la Arusha hatukuwa na jinsi ilibidi tufanye hivyo..

Je, kulikuwa na mwisho, Bila shaka kama tungeweza kufikia hatua ya kuwa na wasomi na vyanzo vya uwekezaji wetu wenyewe wa kutosha kuendesha elimu, afya, kilimo, viwanda, madini na kadhalika bila shaka Ujinga, Umaskini na Maradhi visingekuwa vyanzo vya unyonge wetu hadi kufikia leo..tatizo ni kwamba tuliondoa focus yetu kwenye vitu hivi wakati tunatazama mfumo wa siasa na ulaji..Leo hii tungechimba wenyewe madini, kilimo na kadhalika kiasi kwamba hata unapokuwa na vyama vingi vinatazama maendeleo ya uwekezaji huo lakini sio kabla wakati tupo juu ya mabati tukiomba msaada wa kuokolewa.. Halafu swala la vyama vingi sio choice tena, ni vitu ambavyo vingetokea na tusingeweza kuvizuia na kama tungekuwa tayari tumefika mahala pazuri leo hii tungepeta na huu mfumo wa soko huria na demokrasia..

Labda nimalizie tu kwamba wale walioathirika na janga la mafuriko, hawa watu jinsi wanavyoishi leo sii maisha ambayo wewe unaweza kuyatazama na ukayapenda lakini hawana jinsi na kwa kila anachojaribu kujinyima huwezi kusema anajionea ama anawaonea watoto wake kwa sababu tu hataki kuwaacha watoto wake wachukuliwe na watu wengine.. Haya ni matatizo ya kupita sii ya kudumu na ndivyo anavyotazama huyo muathirika ktk kila maamuzi yake ingawa wanalala ktk mahema tena basi mahema yenyewe yamejengwa palepale walipopata mafuriko wakimuomba Mungu mvua isirudi, wengine wamepelekwa ktk shule za msingi na kulala juu ya madawati, chakula cha kugombania na kadhalika haya sii maisha ambayo wewe unatakiwa kuyapima kwa watu hawa uikitazama na yako wewe usiyekuwa ktk hali yao..

Je, yatakuwa na mwisho? bila shaka ikiwa mipango bora ya kuwaondoa hawa watu ktk adha walizopo itafuatwa na pengine watakuwa na maisha bora zaidi huko mbeleni lakini sio leo uwaambie kwa nini hamkutaka kwenda kuishi Chalinze... kwani sisi tulipenda kutawaliwa hadi watuache wajinga, na maskini tukiwa na wasomi wasiofika 10.

Kwa kuongezea tu kama IMF, serikali sasa hivi inawapa masharti wao, wahame na bila shaka inawatakia kheri waathirika hawa lakini lazima wao pia waafiki tulingana na wanavyoitaza future yao. kuna maswala ya ajira yanahusu hapa, kati yao wapo wafanyakazi wa mjini wa mjini ktk maofisi ya serikali na mashirika, wengine ni wajasiriamali, leo ukamwamishie Chalinze hawa watu wataweza vipi kumudu maisha mapya?...Ndivyo, IMF ilivyotukuta wakatupa misaada na kutuhamisha toka Ujamaa kwenda Ubepari lakini tukubali tumepoteza ajira zetu..Na makazi mapya walotupa ni kurudi kuwatumikia mabwana kama tulivyokuwa wakati wa Mkoloni...
 
Mh Prof Shivji aanze kutafuta uraia wa Canada mapema maana ninavyomjua baba Riz kwa visasi, hachelewi kumvua Shivji uraia
 
Wanatafuta kila njia ya kubaki madarakani. Wakishindwa kwa kupata katiba mpya WATAAMRISHA JESHI liwaue raia. Hapo ndipo tutakapoingia MSITUNI. Amani haiji ila kwa ncha ya upanga, iliandikwa. Hatukupata UHURU KAMILI. Tulipata fursa ya kuwapa wenzetu Waafrika Weusi nafasi ya kututawala, tena vibaya kuliko wakoloni Wazungu. Sasa hawa WEUSI wamenogewa na madaraka, hawataki kuyaachia. Wako tayari kwa lolote. Si mmeona jinsi wanahabari wanavyoundiwa kesi za "uchochezi"? (Sedition!) Hivi nyie mnajua maana halisi ya uchochezi? Hata mimi, kwa mujibu wa hawa MAALUNI naweza kuitwa mchochezi, ilhali tu NIMESEMA UKWELI!
 
The president his pointing a loaded gun to wananchi as hostage.That may lead to short term victory to him and long term loss to the nation as all.Come his Exit 2015 we might see the light in the tunnel.
 
Back
Top Bottom