TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 24,891
- 11,288
Mkuu jamaa ni weupe mno na wanadhani watatawala mileleHizi aina ya sheria zilitungwa ili kufuatwa lakini zina maumbile ya kuvunjwa.... Na ni kama vile zimeandikwa 'bend here to break'
Mkuu jamaa ni weupe mno na wanadhani watatawala mileleHizi aina ya sheria zilitungwa ili kufuatwa lakini zina maumbile ya kuvunjwa.... Na ni kama vile zimeandikwa 'bend here to break'
This is ridiculous isn't it?- kwenye Majukwaa tunaambiwa na Waunda Azimio, "usawa", "usawa", then many years later wanatuambia, "si usawa kwa maana vidole havilingani".
You ask me what did I find on my own, I just find that we were duped!, a kind of Animal farm where some animals are more equal than others. this kind of flip flop is destined to fail and this is what happened exactly few years later.
ngoja sasa nikuwekee baadhi ya masharti ya Azimio la arusha then utaona kwamba Azimio la Arusha lilihitaji modification katika kipengele cha Maadili ya Viongozi...................................
Ha ha ha! na wewe unayemtetea unafanya hivyo kwasababu za kidini au sivyo?? watu bana!
Mimi nilishakwambia mara nyingi kwamba tatizo la nyerere alikuwa MBOVU period
kwangu mimi ujamaa, ubepari (sera yeyote) siyo tatizo, tatizo ni nani anayesimamia hiyo sera???
kwa hiyo nyerere tungepata faida kama angekuwa kiongozi mzuri hata kwenye ujamaa period..
Mimi mzima aisee, kwangu mimi watoto wangu na ukoo wangu nyerere siyo baba eat it..
Bwana Mchambuzi:Katika kikao cha CCM-NEC Zanzibar (1992) kilichoua Azimio la Arusha na kuzaa Azimio la Zanzibar, agenda kubwa/iliyo dominate kikao kile ilikuwa Maadili ya Uongozi na jinsi gani ya kutupilia mbalu suala hilo ili wakubwa wafaidi matunda ya soko huria, huku wananchi wakitapa tapa na massive unemployment and mushrooming of informal sector. Kwani, masuala mengine ndani ya Azimio la Arusha walisha yaua kimya kimya siku nyingi sana (tangia 1986), bila hata ya kuwaandaa au kuwapa wananchi elimu ya uraia juu ya mabadiliko yaliyokuwa yanakuja.
kipengele cha 4 kinasema hivi:
ASIWE NA MISHAHARA MIWILI.
Hii ilikuwa inadumaza, inakwaza mtu mwenye uwezo wa kutumikia kazi mbili kwa ufanisi kujiinua, na kutoa mchango mkubwa kwa jamii!, mathalani kuna ubaya gani daktari Bingwa/kiongozi wa idara kuwa daktari na kuwa lecturer na kisha kupokea ujira kwa kazi zake hizo mbili anazofanya?.
Azimio la Zanzibar lilikuja kuondoa discrepancies kama hizi, sasa badala ya watu kuona kwamba ni modification ya msingi kwa sababu Azimio la Arusha siyo Msahafu, wakaona kwamba eti ni kulipinga Azimio Zima, HIYO SI KWELI. bali hayo ni mabadiriko ya msingi ambayo yalibidi yafanywe kutokana na wakati.
kipengele cha Tano cha maadili ya Kiongozi kinasema hivi.
ASIWE NA NYUMBA YA KUPANGISHA
Hii pia ilikuwa ni kikwazo na unnecessary, kama mimi ni mkulima na mfanyakazi nina kipato halali kwa nini nisiweze kuwa na nyumba na nikaipangisha pia?.
Je kama nina nyumba tupu, au nina nyumba ambayo siitumii yote, je siwezi kupangisha vyumba vilivyobaki?.
Nani amekwambia hatukuwa na viwanda vidogo vidogo vya watu binafsi?Bwana Mchambuzi:
Ukweli ni kwamba Mwalimu Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM mara tu alipong'atuka mwaka 1985, kwa hiyo notion ya kudai kwamba masuala mengine ya azimio la arusha waliyaua kimya kimya as if Mwalimu hakushiriki fully vikao vya Chama, mwaka 1986 si ya kweli!.
Umeniuliza kwamba ningemjibu vipi Mwalimu kuhusiana na maadili ya viongozi?- infact ningemjibu wazi kwamba, pamoja na kwamba ni kiongozi lakini nina haki ya kutumia ujuzi wangu mwingine kwa malipo halali ya kazi yangu, kisha ningemweleza wazi kwamba sioni mantiki ya mimi kutokuweza kupangisha nyumba yangu niliyoijenga kwa jasho langu mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo sijaiibia serikali!.
ndo maana nimeweka vipengele viwili vilivyofanyiwa mabadirisho na Azimio la Zanzibar najinukuu hapa chini, kisha naomba maoni yako kuhusiana na vipengele hivyo:
Bwana Mchambuzi, Msingi mwingine wa Azimio la Arusha lilikuwa ni kwamba njia zote za Uchumi zimilikiwe na Umma kupitia Serikali, sasa mimi sitaki kuingia katika mjadala wa kiitikadi, lakini ni dhahiri Serikali ili "overdo" utekelezaji wa dhana hii, kwa maana hata viwanda vidogo vidogo ilikuwa lazima vimilikiwe na Serikali, Serikali ingeruhusu uwanzishaji wa viwanda binafsi toka awali ili kutimiza lengo la kujitegemea, hata baadhi ya mashamba kama vile mkonge Serikali ilikuwa haina haja ya kuyahodhi( Nyerere alikiri kukosea katika hili).
Sera ya Soko huria aliyoiadapt Mzee Mwinyi siyo mbaya, ubaya unakuja pale aliposhindwa kuweka mechanism ya kumlinda mlaji/mtumiaji kupitia mechanism ya kuangalia bei vis-a-vis kiwango kinachokubalika kwa mfanyabiashara naye apate faida lakini si ya kupitiliza na hatimaye kumuumiza mlaji.
Lakini Kikubwa bwana Mchambuzi, ilikuwaje ikawa Rahisi kubadirisha Vipengele vya Maadili ya Uongozi kimya kimya?- Je haya maadili ya Uongozi yalipata kuwa ndani ya Katiba yetu?, je yalikuwa ni sehemu ya Sheria zetu?- Kama Mwalimu hakuyaweka hayo ndani ya Katiba na Sheria zilizotungwa na Bunge alitegemea nini?.
Narudia kusema, Azimio la Zanzibar halikuua azimio la Arusha bali lililiboresha!- Muda ulikuwa umefika wa kwenda na wakati, mambo ya Viongozi kutokuweza kupangisha Nyumba zao yalikuwa yamepitwa na wakati!, na Azimio la Zanzibar ndilo lilikifanya.
Mwalimu Nyerere mwenyewe katika maandishi yake mengi anasema wazi, yale yenye makosa mnarekebisha, mazuri mnachukua.
Sasa basi bwana Mchambuzi, mambo ya MAAZIMIO tuviachie vyama vya Siasa, mimi Si mwanachama wa Chama Chochote cha Siasa, nitachagua Chama kulingana na wakati na mazingira yangu!, nikiwa middle class naweza kufavor chama fulani, nikiwa tajiri naweza kufavor chama kingine. Cha msingi ni katiba ambayo iko fair kwa raia wote na sheria zinazo level ground kwa raia wote kuishi kwa jasho lao, Mambo ya Azimio la Arusha/ Zanzibar ni mali ya WanaCCM, kwa sababu ilikuwa ni dira yao waiongoze nchi vipi!.
Kama chama kinaona mambo ni ya Msingi basi kiyatungie sheria, au kiyaingize katika katiba kupitia bunge la Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, badala ya kubaki kama Maazimio, kwa maana katika nyakati hizi Chama hakishiki hatamu siyo kama enzi zile!
wakati mwingine inabidi tu uvumilie ujinga wa mwenzio. Utadhani mtu hakufundishwa fasihi bwana, loh!Kiranga, haujaelewa dhumuni la mada yangu; Jasusi na wengine wamenisoma vizuri; Jasusi hapo juu has inferred mtazamo wangu mia kwa mia;
Weren't we told that Ujamaa refers to equality?- what equality were we talking about then?
Ha ha ha! na wewe unayemtetea unafanya hivyo kwasababu za kidini au sivyo?? watu bana!
Mimi nilishakwambia mara nyingi kwamba tatizo la nyerere alikuwa MBOVU period
kwangu mimi ujamaa, ubepari (sera yeyote) siyo tatizo, tatizo ni nani anayesimamia hiyo sera???
kwa hiyo nyerere tungepata faida kama angekuwa kiongozi mzuri hata kwenye ujamaa period..
Mimi mzima aisee, kwangu mimi watoto wangu na ukoo wangu nyerere siyo baba eat it..
Mkuu wangu usituharibie mjadala tafadhali..... Ebu nikuulize wewe sifa za mwenyezi Mungu ni zipi? majina 99 kwa uchache wa sifa hizi - wewe binadamu huna? na kwa nini iwe wewe na sio viumbe wengine... Mkuu usijaribu kuipinga Injili pasipo kuelewa maana achana na tafsiri za watu ila jaribu kuilewa Injil ilikuwa na maana gani kulingana na Kuran..
Turudi kwenye mada yetu tafadhali..
Gamba La Nyoka, tuseme unakutana na wakulima katika kijiji kimoja Tanzania, ambao soko huria limewacha hoi bin taaban, suala la soko huria kuwacha 70% ya watanzania HOI sidhani kama lina mjadala; Sasa, katika mjadala wako na wakulima/maskini hawa wa watu, juu ya hali zao ki-uchumi, ki-jamii n.k, mmoja wao anatoa hoja kwamba Azimio La Arusha (1967 – 1992) lilikuwa ni la Wananchi, na Azimio la Zanzibar (1992 – 2011) ni la Watawala, utamjibu nini? Jibu hilo nalo litatusaidia sana to shed more light katika huu mjadala wetu on Azimio la Arusha.
Umeniuliza kwamba ningemjibu vipi Mwalimu kuhusiana na maadili ya viongozi?- infact ningemjibu wazi kwamba, pamoja na kwamba ni kiongozi lakini nina haki ya kutumia ujuzi wangu mwingine kwa malipo halali ya kazi yangu, kisha ningemweleza wazi kwamba sioni mantiki ya mimi kutokuweza kupangisha nyumba yangu niliyoijenga kwa jasho langu mwenyewe, kwani kwa kufanya hivyo sijaiibia serikali!.
ndo maana nimeweka vipengele viwili vilivyofanyiwa mabadirisho na Azimio la Zanzibar najinukuu hapa chini, kisha naomba maoni yako kuhusiana na vipengele hivyo...
Mchambuzi,
Shukran mkuu wee fimbo yao....Yes, a powerful speech by Nyerere mwaka gani huo 1962... daaaah! Mungu amweke mahala pema peponi yaani aliona mbali sana... leo yanajirudia tu...
............................
Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na ufahari ni mzito mno na watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia na sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tama yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila kujali maisha ya watu."]
JKN, Tanu na Raia, 1962.
********
Ntakurudia juu ya hoja zako nyingine.
May be pato la taifa likiongezeka tutaona mawaziri wa miaka ijayo wanatumia HAMMER. hakuna Uzalendo
Bora afanye hivyo kwa ipato chache lakini sio anatumia STK hammer bila kujishtukia. Tena mwingine unakuta anaitwa waziri wa mazingira.Tuna waheshimiwa tayari wapo huko; sasa inakuwa vigumu kuwaelewa kwenye TV wanapopinga suala la posho, sasa hatujui Fuel Guzzler kama HAMMER litakaa vipi barabarani; unless wao tayari wana bahati ya kuwa na mishahara miwili, nyumba za kupanga, na hisa katika publicly traded companies;
Gamba La Nyoka, tuseme unakutana na wakulima katika kijiji kimoja Tanzania, ambao soko huria limewacha hoi bin taaban, suala la soko huria kuwacha 70% ya watanzania HOI sidhani kama lina mjadala; Sasa, katika mjadala wako na wakulima/maskini hawa wa watu, juu ya hali zao ki-uchumi, ki-jamii n.k, mmoja wao anatoa hoja kwamba Azimio La Arusha (1967 1992) lilikuwa ni la Wananchi, na Azimio la Zanzibar (1992 2011) ni la Watawala, utamjibu nini? Jibu hilo nalo litatusaidia sana to shed more light katika huu mjadala wetu on Azimio la Arusha.
Hoja yako kwamba mwaka 1967, kama kiongozi wa taifa huru lenye miaka 6 tu, una haki ya kutumia ujuzi wako mwingine mahali popote, popote wapi? katika uchumi upi Gamba La Nyoka? Soko lipi wakati 95% ya nchi ni vijiji/wakulima? au una maanisha bwana shamba binafsi? Unazijua takwimu za uchumi za aliotuachia Mkoloni zilikuwaje Gamba La Nyoka? Social conditions pia?