Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #41
so the question is, if the arusha declaration didn't promise to do away with our poverty why did we adopt it as our economic, social and political compass? from the early beginning.
Wasn't poverty one of our enemies?- so if we had exhausted all those decades to implement azimio la arusha only to be told by our "muasisi" that it didn't mean to do away with poverty then why did we waste our time with it in the first place?.
Hope, hope, hope,hope- people dont eat hope, dont wear hope, dont sleep in hope, hope will always be there even when you are rich, you will still hope for more!
People want tangible results.
Now i think, if azimio didn't mean to do away with poverty then it was wise to do away with it/modify it , and thus congratulations to president mwinyi.
Mkuu, umelisoma lakini vizuri Azimio La Arusha? Nina nakala soft hapa, I can send you. Na je, umeelewa mantiki nzima ya Mwalimu hapo? Na nani dunia hii anaweza kusema anaweza kumaliza tatizo la poverty? hata Mwalimu, from the outset, didn't promise to do so; alichotupa ni self determination, na kuondokana na minyororo ya unfair global capitalist system, ambayo yeye hakuichukia per se, bali alipigania fair participation;
Mwaka 1970 Mwalimu alitamka haya:
******
"We say man was created in the image of GOD. I refuse to imagine GOD who is poor, ignorant, superstitious, fearful, oppressed, and wretched – which is the lot of the majority of those HE created in his own image. MEN are creators of themselves and their conditions, but under present conditions WE are creatures, not of GOD, but of our fellow MEN.
JKN, 1970
*******
Vinginevyo, Mwalimu hakuchukia Ubepari Per Se, bali unfairness that was inherent in Ubepari. Hata kwenye kitabu chake cha TANU na RAIA, in 1962 (p.8), even before Azimio La Arusha Lililokuja kuzaa UJAMAA, Mwalimu anasema:
"Kwahiyo, ikiwa serikali ya TANU itachukua hatua za kuzuia tofauti iliyopo sasa kati ya watu wa juu na watu wa chini, sina shaka watu wote walio juu hawatapenda. Hata mimi ninayeandika maneno haya, sitapenda; kwani hata mimi napenda kuwa Tajiri! Lakini kitakachotuwezesha kujenga nchi safi siyo tamaa yangu mimi kuwa tajiri, bali ni vitendo ambavyo, ingawa tunajua kuwa vitaudhi wachache, tunayo hakika kuwa ni vya manufaa kwa ndugu zetu walio wengi".
Gamba La Nyoka, no offense, na nina heshimu haki yako kutoa mawazo unavyopenda, lakini niwe mkweli - sijaamini macho yangu niliposoma WEWE kutoa pongezi kwa Mwinyi (na hata ingekuwa Mkapa au Kikwete) kwa madhara ya soko huria yaliyopo sasa, wakati inajulikana wazi kwamba nchi imechukuliwa mateka na IMF na WordBank since 1986. Viongozi baada ya Nyerere wanafanywa na WorldBank na IMF kuwa "viongozi watekelezaji" (au tuseme managers), hawana mamlaka tena kimaamuzi juu ya ndugu zetu vijijini ambao ndio wanatuweka mjini kwa vyakula, na pia wanatupatia fedha za kigeni kutanua na magari ya kifahari kama waheshimiwa kutokana na kilimo cha cha kifukara, ambacho watawala wetu, zaidi ya kuchuma, hawana muda nacho tena kama wakati wa Mwalimu. Ni audience hiyo ambayo Mwalimu hapo juu kwenye my original post ndio ana wa address, kitu ambacho wengine wanaweza kuona Mwalimu ni Mchochezi.
Vinginevyo Gamba La Nyoka, ni muhimu utambue kwamba, hata kama Rais baada ya Nyerere in 1985 angekuwa anaitwa ni Peter, Khadija, Said, au Stella, Rais huyo angeitwa "RUKSA".
Watu wanamkejeli Mwalimu ambae juhudi zake zililenga kitu kimoja tu: To give our country a self determination baada ya kupotezea muda na direction na wakoloni. Hilo ndilo lilimpa heshima kubwa duniani, kiasi cha kuombwa na nchi zote za kusini chini ya Waziri Mkuu wa Zamani wa Malaysia, kutoa mwongozo kama Mwenyekiti (aliefeli na Ujamaa), jinsi gani nchi maskini zinaweza kujikomboa; Sote tunajua mafanikio ya South Commission yalikuwa nini.
With all due respect that I have for Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Je, ni nani/nchi gani/taasisi gani ilimfuata/imemfuata kwenda ku replicate mafanikio ya soko huria Tanzania, katika nchi nyingine za Africa, Latin America, Asia? Unatambua kwamba wakati wa mwinyi, in early 1990s Tanzania ilikuwa nchi ya tatu kwa umaskini duniani – mbele tu ya Somalia na Afghanistan? Unakumbuka hali ilivyokuwa tete? Nina imani hautakuja na jibu kwamba ni kwasababu Mwinyi alipokea nchi ikiwa tete toka kwa Nyerere. Iwapo utasema hayo, Je hicho ndio kipimo cha uongozi ambao unapelekea wewe binafsi kumpa pongezi?
Kwa mtu makini, kusingizia failure za Rais aliyepita kwamba ndio kikwazo kwa rais aliyepo ni kukubali failure, hakuna lingine. Hata wenzetu Marekani, moja ya sababu kubwa zilizomsaidia Obama kushinda uchaguzi mwaka 2008 ilikuwa ni matatizo ya kiuchumi aliyoyaacha Rais aliyemtangulia – yani, BUSH. Lakini katika mbio za uchaguzi mwingine- miaka mine tu baadae (2012), Obama ana kazi ya ziada kushinda tena uchaguzi 2012, lakini tunaona kwamba, sio yeye, wala washauri wake wanaotumia utawala wa Bush kama kisingizio, na wakithubutu tu, game is over, kwani wananchi waelewa (tofauti na wengi wetu Tanzania ambao sio waelewa) watamhoji Obama: Ulitueleza matatizo ya Bush, tukaelewa na kukuamini ili uyatatue, Je umeshindwa tumpe nafasi mtu mwingine?
Gamba La Nyoka, Uchaguzi mkuu wa Marekani 2012, wananchi hawatampigia Kura Obama kwa sababu ya Bush, watampigia kura Obama kwa sababu ya Obama.
Kwa hoja zenu hizi juu ya Mwalimu, sitashangaa hata uchaguzi wa Tanzania miaka 50 ijayo/mwaka 2065, wapo watanzania wengi watakaowakataa wagombea fulani kwa sababu ya Mwalimu Nyerere, sio Kwa sababu ya uwezo na sifa za wagombea.
Mwisho naomba niongezee tu kwamba – na on this one, I am not addressing you as Gamba La Nyoka, bali ni kwa vijana wote, kwani limenijia akilini sasahivi. Vijana wenzangu, viongozi hawa wanaotutuma kuwafagilia au kuwapigia debe, baada ya miaka 15-20 watakuwa wamestaafu wanakula pensheni zao; Wewe utakuwa wapi kijana mwenzangu? Chungeni sana msije mkachagua the wrong side of history sasahivi. Otherwise, utaweka uso wako wapi, na utaishi vipi katika jamii wakati umri wako ndio kwanza utakuwa pengine unakaribia miaka 50 tu, mbichi kabisa, wakati hao mnaowafagilia watakuwa HAI au HOI, kama wastaafu. Ni dhahiri kabisa kwamba, mkiwafuata kwa msaada, ushauri, miaka hiyo, wataambia "Mimi Mstaafu Bwana"
Tafakari.