Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

Hahaaaa!!!!huyu ni The Greatest
View attachment 2065734

Prof.Assad ametoa maoni yake kuhusu mfumo wa siasa wa nchi yetu. Siasa yetu inatufanya tusiwe na malengo yanayopimika. Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.

Anasema watu wanazunguka kutaka ku score point za kisiasa tu.

Amegusia kuhusu kilimo. Anasikitika sana kuona kilimo kinaimbwa wakati hakuna mabwawa ya kutosha. Anashangaa serikali imeacha maji yaende baharini/ziwani kama vile bahari ndio ina shida na maji kuliko sisi
 
We acha tu mkuu,nchi zao ni jangwa lkn huwez sikia hawana chakula wala shida ya maji.
Hapa tunachojua ni mapambio tu,mijitu mizima inatetea matumbo yao
Watu wa Misri, Libya, Tunisia, Morocco wakija tanzania wakaona tuna uhaba wa maji au umeme watashangaa sana tuna akili gani.
 
Hiyo benki ya kilimo ni kama pambo la kisiasa tu it is not efficient at all.

Kwa bahati mbaya sana hakuna administration hata moja ambayo imechukulia kilimo kwa uzito wake wakati ndio shughuli ambayo inafanywa na 80% ya watanzania.

Hakuna efforts za kihakikisha kuwa tunahifadhi mbegu zetu asilia ukiachana na hizi za kizungu wanazotuletea ambazo ukishapanda mara moja huwezi irudia tena.
 
Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.
Hapo yuko juu ya mstari, labda watu wengi watadharau lakini haingii akilini kuona kama mfumo haufanyi kazi hadi mtu mwenye cheo cha kisiasa anazurura mitaani kutatua kero.
 
Inawezekana sehemu kubwa ya nchi yetu watu wake wana uwezo mdogo sana kiakili na kufikiri kwa logic.
Sahihisha sentence yako, ni viongozi wenye uwezo mdogo sana wa akili lakini baada ya kukalia viti wametunga sheria kuhakikisha hawatoki madarakani. Wanadhibiti vyombo vya ulinzi na usalama, tume ya uchaguzi na bunge.
 
Hv unadhn nn tatizo????
Hiyo benki ya kilimo ni kama pambo la kisiasa tu it is not efficient at all.

Kwa bahati mbaya sana hakuna administration hata moja ambayo imechukulia kilimo kwa uzito wake wakati ndio shughuli ambayo inafanywa na 80% ya watanzania.

Hakuna efforts za kihakikisha kuwa tunahifadhi mbegu zetu asilia ukiachana na hizi za kizungu wanazotuletea ambazo ukishapanda mara moja huwezi irudia tena.
 
Ikitokea chama cha siasa kikakomaa na hoja ya kilimo na wakulima, kitaing'oa CCM mapema asubuhi.
Huwezi kuing'oa meli ya CCM huku nanga za vikosi vya ulinzi na usalama, tume ya uchaguzi na bunge zimekita chini.
 
Tangu lini mwafrika akawa na akili ya kujiongoza mwenyewe, hawa viumbe ni special species ambao wana element ya kutawaliwa na kuongozwa.

Mfano mwingine ni vile viwanda tulivyoachiwa na wakoloni vyote vimekufa, viongozi waliingia tamaa wakaviuza kwa wahuni, wahuni wakang’oa mashine na kuvitelekeza.
Viwanda havikuachwa na wakoloni, vilijengwa na Nyerere, vikauzwa na Mkapa.
 
View attachment 2065734

Prof.Assad ametoa maoni yake kuhusu mfumo wa siasa wa nchi yetu. Siasa yetu inatufanya tusiwe na malengo yanayopimika. Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.

Anasema watu wanazunguka kutaka ku score point za kisiasa tu.

Amegusia kuhusu kilimo. Anasikitika sana kuona kilimo kinaimbwa wakati hakuna mabwawa ya kutosha. Anashangaa serikali imeacha maji yaende baharini/ziwani kama vile bahari ndio ina shida na maji kuliko sisi

Ila huyu mzee basi tu kichwa kweli kweli! Alipaswa kuwa mshauri wa raisi na tungesogea
 
Ishu ya kuwa na mabwawa kila wilaya ni muhimu sana ili kuwa na kilimo cha uhakika kila mwaka!
 
Hili suala la mawaziri kuzunguka mikoani mfano stendi za mabasi kukakugua tiketi lidhibitiwe kupunguza matumizi ya serikali hasa kipindi hichi ambapo kuna mjadala mkali kati ya kukopa zaidi au kuongeza tozo.

Tatizo la hii nchi ni wizi
 
Back
Top Bottom