Prof. Assad: Mfumo wa Siasa una shida. Huwezi kuzungumzia Kilimo wakati huna Mabwawa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,155
103,588


Prof.Assad ametoa maoni yake kuhusu mfumo wa siasa wa nchi yetu. Siasa yetu inatufanya tusiwe na malengo yanayopimika. Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.

Anasema watu wanazunguka kutaka ku score point za kisiasa tu.

Amegusia kuhusu kilimo. Anasikitika sana kuona kilimo kinaimbwa wakati hakuna mabwawa ya kutosha. Anashangaa serikali imeacha maji yaende baharini/ziwani kama vile bahari ndio ina shida na maji kuliko sisi 🤣🤣🤣🤣
 
View attachment 2065734

Prof.Assad ametoa maoni yake kuhusu mfumo wa siasa wa nchi yetu. Anashangazwa na waziri kuzunguka kuchukua kero za wananchi wakati Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya wapo huko. Anasema labda sababu ni kupata posho tu.

Amegusia kuhusu kilimo. Anasikitika sana kuona kilimo kinaibwa wakati hakuna mabwawa ya kutosha. Anashangaa serikali imeacha maji yaende baharini/ziwani kama vile bahari ndio ina shida na maji kuliko sisi 🤣🤣🤣🤣

Ha ha ha hii kali
 
awamu iliyopita tulishuhudia mpaka mifarakano ya kifamilia analetewa rais kwenye mikutano ya hadhara.
 
Hata yule Mkuu wa Mkoa huwa anazunguka kusikiliza 'matatizo' ya Wanainchi kana kwamba hawayajui.

Hakika ni kutafuta tu score za kisiasa na posho, na akifanya hivyo lazima waalike Media.
Hili suala la mawaziri kuzunguka mikoani mfano stendi za mabasi kukakugua tiketi lidhibitiwe kupunguza matumizi ya serikali hasa kipindi hichi ambapo kuna mjadala mkali kati ya kukopa zaidi au kuongeza tozo.
 
Back
Top Bottom