Prof. Assad ameonewa. Siri ni nzito, tuwe kimya tu

Prof. Assad ameonewa. Siri ni nzito, tuwe kimya tu

Habari ambazo sijazithibitisha. Prof Assad anaonewa tena wanao muonea sio kwa masilahi ya Taifa ila wanayo yajuwa wao.

Pia watu wanasema kuwa spika anamtega Rais ila kama tunavyo juwa Rais ni taasisi hawezi kukurupuka kumuwajibisha CAG maana kama ilivyo semwa hapo awali italeta mtikisiko mkubwa sana wakikatiba hivyo Mh Rais anatumia kila uwezo alio nao pasipo kushawishi Bunge kuacha jambo hili lipite nalo ila watakutana kwenye kamati za cc

Wapo watu wanasema Rais amsimamishe kiukweli watunga katiba walikuwa makin sana wakijuwa kuna siku litaibuka bunge kama la sasa kutaka kufanya mambo yao. Sasa ili Rais amsimamishe kuna takiwa kuwe na hoja ila hoja nzito sio hoja hii nyepesi ya spika. Wenye mamlaka wanauliza tusi au neno dhaifu maana yake nini na hapo ndipo bunge limeonekana kuchemka. Pia mchakato wakumuondoa CAG sio wakitoto maana wanatakiwa majaji wa nne walio iva kufanya uchunguz na sio kama zao za bunge sasa kiukweli kabisa kama rais akiunda hiyo Tume upo uwezekano mkubwa Prof akasafishwa jambo litaleta dowa baya sana kwa serikali na ndio maana wenye akili wanahepa maamuz ya bunge kwasababu azimio walilo litoa litawatafuna wenyewe take from me.

CAG ni mtu hatari sana kucheza na cheo chake kwakuwa nimkono unao tafuta matumiz mabaya ya serikal mpaka bunge sasa lazima awe na kinga Labda niwaulize nani amewahi jiuliza why spika anapambana na Huyu prof? Je issue ni hii hii au kuna siri nzito?

Wapo. Watu wanaamini Mkuu ndia alie amuru bunge litekeleze haya nataka niwaambie jambo hili limemkwaza hata Rais maana anashangaa nini kinaendelea na ili kuwa mbali na mgogoro huu amewaacha wale matapishi yao wenyewe. Rais hana ugomvi Wala hana mgogoro wowote na Prof Assad. Ila watu wanajuwa tu yao.

Yote tutayajuwa niswala la Muda tu.
Kwanini aliipokea ripoti kimya kimya?????

usitake kumtetea NGOSHA......yeye ndiye anaratibu huu mchezo
 
Acha kupotosha, msio kuwa na uelewa wa mambo ndiyo mnashabikia ukosefu wa maadili na kupungukiwa kwa hekima kwa huyo Prof Assad wenu. Nyie subirini muziki toka Ikulu lazima ang'olewe huyu mkeuka maadili, kwanza anaonekana hana siri, yaani hana maadili ya kazi yake, nyie mtapiga kelele lakini serikali huwa haishikwi sharubu na huwa haichezewi kabisa hata kidogo, just be alerted mtaona maamuzi very soon. Na endeleeni kumpa kichwa maji huyo Prof wenu. Huwezi kubishana na serikali, serikali ni mfumo na mfumo una mkono mrefu sana, yaani huwezi ukalidharau bunge ukadhani eti wewe una linda professional professional gani hiyo inayoruhusu kudhihaki mhimili mkuu wa nchi????
Kada maarufu. Usicokijua kwenye taaluma ya uhasibu ni kuwa neno dhaifu means dosari.
Hata makampuni makubwa yanayofanyiwa ukaguzi huwa wanaambiwa udhaif wao uko wapi.
Huchukua ujumbe huo na kuufanyia kazi. Tofauti na serikal haswa bunge ambalo limeonyeshwa dosari yake wakawa wakali.

Profession ya uhasib haina longolongo. Na si ukosefu wa maadili hata mhe.rais anaelewa hiko kitu ndio maana mpaka sasa kakaa kimya.
Bunge wajirekebishe.. wao sio malaika kuwa kila kitu watafanya sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huyo mzee ana dharau,majivuno na kiburi sana..baada ya maamuz ya bunge akaenda kuharisha tena TBC, huku akipewa kick na wanasiasa uchwara na wachambuzi wasio na akli na wnye chuki na spika...CAG amefanya counter offensive moja kali sana kwa kauli yake hyo....mda wake unaisha mwez wa 11 na ndo itakuwa exit door...
Wapi alionyesha kiburi na dharau..?mbona mnakazana kutaka kuaminisha watu kuwa CAG ni mbaya wkt alichosema ni ukweli?
Kama ni muhasib na umeshawahi kufanya ukaguzi wa makampuni makubwa.. neno dhaifu means dosari mahali fulani.
Na kwa taasis kubwa haswa makampuni makubwa huchukua hatua ya kuboresha miundo yao baada ya report za ukaguzi.

Bungen kimeambiwa ukweli wamekuwa wakali ? Why? Sion kosa lake hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaona alipoonewa CAG binafsi, Prof kiukweli alilikosea bunge na ata wakati anahojiwa na kamati ya maadili na hadhi ya Bunge bado hakutaka kuona kama kauli yake ni mbaya alionesha dharau na kiburi bado na kusema ataendelea kuitumia kauli hii..! bado CAG amekuwa mjivuni mnoo kwa kuidharau Taasisi na Muhimili na sioni kama CAG yuko juu ya muhimili wowote kikatiba alipaswa kuwa na tahadhali juu ya kauli zake.
tufike mahali tunapoambiwa ukweli, hasa na mtu ambaye ndio kazi yake kuusema, tuukubali tuu...hata kama unauma....kama tunakubali kuambiwa ukweli kwa mazuri tukubali kuambiwa tuna madhaifu pia...ungwana ni kuufanyia kazi ...sio kusemwa tumedhalilishwa...jamii zote zilizendelea zinafanya kazi katika misingi hiyo!
 
KATI YA BUNGE NA CAG NANI NI DHAIFU?

Na Lusekelo Mwandemange.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza wote waliotumia muda wao kutoa maoni na kujadili suala la Bunge kukataa kufanya kazi na CAG (Controller & Auditor General-Mthibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali) kutokana na kauli yake tata alioitoa akiwa marekani kwa kuita Bunge ni DHAIFU.
Binafsi nimejiuliza maswali mengi kama wengine walivyo hoji. Kwanza nilijiuliza CAG ni nani hasa mpaka aite Bunge ni dhaifu hasa anapohojiwa kuhusiana na hoja za kigaguzi zinazopelekwa bungeni kutopatiwa majibu?. Je kuna kosa gani kwa yeye kuita Bunge ni dhaifu? Na je ni kweli Bunge ni dhaifu? Na kama ni dhaifu katika lipi? Na kwa nini atamke hadharani wakati ana nafasi ya kukosoa ndani? Na kwa nini akatamke nje ya nchi na sio akiwa hapa Tanzania? Na je Bunge kukataa kufanya kazi na CAG ni sawa? Na madhara yake ni nini? Na kama sio kupitia CAG Bunge watasimamiaje serikali? Pia nikajiuliza Bunge na CAG nani mwenye mamlaka ya juu kuliko mwenzake na nani anawajibika kwa nani? Hakika maswali ni mengi lakini sina nia ya kujadili maswali yote haya. Niseme tu katika hili naamini Bunge na CAG wote wakosaji.
Katika kujijibu maswali nikaona nifanye tafakali juu ya CAG Vs Bunge hasa katika kuangalia msingi wa uwepo wao katika katiba ya Tanzania. Kwanza CAG ndio mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali na amepewa madaraka hayo kwa mujibu wa katiba ibara 143 na katiba imeainisha kazi zake kuwa143(2) a) kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka mfuko mkuu wa Hazina ya serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya katiba hii na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe. Na ibara ya 136 (3) Fedha zilizomo katika mfuko mkuu wa hazina ya serikali hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili ya matumizi ila mpaka matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mthibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na pia kwa sharti kwamba fedha hizo ziwe zimetolewa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Na Bunge ni mhimiri katika JMT. Kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63(2) Bunge limepewa madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali ya JMT na vyombo vyake vyote(akiwemo CAG) katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii.
CAG KAKOSEA NINI?
CAG kakosea kwanza kwa kutotambua wajibu wake wa kikatiba au makusudi. Kwa msingi wa katiba ni wazi kwamba CAG amepewa wajibu mkubwa sana sio tu wa kukagua mahesabu lakini hasa KUTHIBITI. Na Bunge limepewa wajibu wa kusimamia na kushauri serikali. CAG ndiye mthibiti mkuu kutupia lawama bunge na kuita Bunge dhaifu naona sio sawa ila kinyume chake ni sahihi? Kwa mujibu wa katiba CAG anatakiwa athibiti matumizi ya fedha ya serikali, kama kuna lolote halijaenda sawa kwenye eneo hilo haitoshi yeye kukagua na kuonyesha tu mapungufu bali anatakiwa athibiti hayo yasitokee. Ikiwa katiba inampa CAG wajibu wa kuthibiti fedha isitoke kwenye mfuko wa serikali bila kuanisha matumizi sahihi na kufuata sheria alafu CAG anatuandikia taarifa kwamba kuna fedha 1.5Trn hazionekani zilipo na yeye ndo mthibiti udhaifu hapo unakuwaje wa Bunge?
Sababu ya pili, CAG ni kukosa uungwana tu. Kwasababu hata katika mahusiano ya kawaida ukimtolea ndugu ama rafiki kauli ya maudhi kwake hata kama wewe hukumaanisha kama alivyoelewa yeye na ukaona nduguyo kachukia busara ya kawaida tu inatuongoza kuomba radhi yaishe. Sasa CAG ingetosha tu kutambua kwamba kauli yake imeudhi bunge(chombo cha wananchi) na kuomba samahani yakaisha lakini kuweka msimamo kwamba hajakosea inaweza kuwa kweli kisheria hakukosea lakini ustaarabu wa kawaida tu ingefaa aombe radhi na kusema tu jamani mimi sikumaanisha hivyo mlivyoelewa lakini kwakuwa ndugu zangu mmeudhika na kauli yangu basi naombeni radhi tufanye kazi tusonge mbele. Lakini kukataa kuomba radhi kunazua maswali magumu. CAG katumwa na nani? Anatumika? Anajiamini nini?
Sababu ya Tatu. CAG kutamka mapungufu ya Bunge hadharani tena nje ya nchi. Yeye CAG ana access na Bunge ameshindwa nini kushauri Bunge mapungufu ya Bunge. Tukubali tukatae nje ya mipaka ya Tanzania watu hawajui Ndugai wala Prof Asad bali wanajua Tanzania. Sasa hata kama tuna mapungufu yetu kama taifa na kwa yoyote Yule haifai kutangaza kwa ulimwengu. Na anadhurika sio mtu mmoja au sio Bunge ni sisi wote. Hivyo suala la kujenga utamaduni wa kusemana, kuonyana, kuelekezana na kukemeana ndani ni muhimu sana. Sifurahii mtanzania yeyote wakiwemo akina Lisu kusema mambo ya nchi yetu nje ya nchi. Kwasababu kuna haribu taswira ya Tanzania. Katika hili CAG kakosea tena sana.
Sababu ya Nne: CAG kakosea kutamka Bunge ni dhaifu jumla jumla. Yaani kusema Bunge ni dhaifu bila kusema katika lipi? Hivi ni kweli kwamba mambo yooote yanayo ainishwa na CAG bunge halifanyii kazi? Kama ni hivyo ingewezekana vipi hati chafu zikapungua. Mbona mambo mengi sana yaliyoibuliwa na CAG yanajadiliwa Bungeni na kufanyiwa kazi. Sasa kutamka kauli isiyo na maelezo kama hii hakika ina tatiza. Unapolenga kumkosoa mtu inafaa kumwambia umekosea katika lipi na kama ni udhaifu wa bunge ni katika lipi? Je kutunga sheria? Kushauri serikali? Kusimamia serikali? Au katika lipi?
Kwa maoni yangu haya ndio makosa ya CAG katika hili.
BUNGE LIMEKOSEA NINI?
Bunge Spika naye amekosea katika hili.
Sababu ya Kwanza; Kuita vyombo vya habari na kuutangazia ulimwengu gadhabu yake dhidi ya CAG. Kama nilivyosema CAG ni mtu muhimu kwenye nchi na amefanya mengi mazuri kutoa kauli hii moja ya maudhi isingekuwa lazima kwa spika kuja juu kiasi hicho. Tena sio sawa kwasababu tunajenga tension kwa wengine bila sababu. Hoja kwamba CAG aliongea kwenye vyombo vya habari akihojiwa nje hivyo ajibiwe kwa vyombo habari sio sahihi. Katika hili CAG kakosea lakini spika kakosea zaidi. Ingefaa tu kumuita na kumhoji pengine bila hata media na vitisho. Kuchukia sana huku kunaweza kuthibitisha kauli ya CAG kwasababu mara nyingi watu huchukia wanaposemwa ukweli. Kama Bunge mnajua sio dhaifu kwanini kuchukia sana mnapoitwa dhaifu?
Sababu ya pili: ni kukataa kufanya kazi na CAG. Sasa mkikataa kufanya kazi na CAG wakati mnajua CAG ameshawasilisha taarifa yake kwa Rais mnataka Rais apeleke wapi hiyo taarifa. Na je Rais akiwaletea mtamkatalia?. Je hamuoni kama mnamuweka pabaya ndugu Rais. Na kwa kasi ya kazi ya Rais Ndugu John Joseph Pombe Magufuri hastahili kufanyiwa haya na ninyi nyote Bunge na CAG. Nadhani Bunge ingefaa tu kutoa onyo kwa kuwa CAG ni mara yake ya kwanza kufanya kosa la namna hii. Na hata kama hakuwaomba radhi ingefaa tu kutoa onyo ili akirudia ndio mchukue hatua kama hii. Lakini ndugu Spika umechukua hatua kali sana kwa kosa la kwanza. Na adhabu hii inaleta sintofahamu kubwa sana. Mnamuweka Rais njia panda. Na mpaka hapa tulipofikia watanzania tunasubiri busara za Mhe Rais aamue hatima ya jambo lenyewe.
Hivyo nitoe wito kwa Bunge na CAG kulimaliza hili. Na njia ninazo ziona ni tatu. Mosi Bunge mbadilishe adhabu iwe onyo tu na mtangaze kufanya kazi na CAG ,Pili CAG uombe radhi kwa bunge na wabunge nafsi zao zitulie wafute adhabu, Tatu Rais atumie busara kulimaliza hili kwa kuwa anazo busara nyingi na uzoefu wa kutatua migogoro kama alivyofanya kwa suala la Kikokotoo, Suala la Korosho n.k
Tanzania ni yetu sote tuijenge na kuilinda.
Ahsanteni.
Habari ambazo sijazithibitisha. Prof Assad anaonewa tena wanao muonea sio kwa masilahi ya Taifa ila wanayo yajuwa wao.

Pia watu wanasema kuwa spika anamtega Rais ila kama tunavyo juwa Rais ni taasisi hawezi kukurupuka kumuwajibisha CAG maana kama ilivyo semwa hapo awali italeta mtikisiko mkubwa sana wakikatiba hivyo Mh Rais anatumia kila uwezo alio nao pasipo kushawishi Bunge kuacha jambo hili lipite nalo ila watakutana kwenye kamati za cc

Wapo watu wanasema Rais amsimamishe kiukweli watunga katiba walikuwa makin sana wakijuwa kuna siku litaibuka bunge kama la sasa kutaka kufanya mambo yao. Sasa ili Rais amsimamishe kuna takiwa kuwe na hoja ila hoja nzito sio hoja hii nyepesi ya spika. Wenye mamlaka wanauliza tusi au neno dhaifu maana yake nini na hapo ndipo bunge limeonekana kuchemka. Pia mchakato wakumuondoa CAG sio wakitoto maana wanatakiwa majaji wa nne walio iva kufanya uchunguz na sio kama zao za bunge sasa kiukweli kabisa kama rais akiunda hiyo Tume upo uwezekano mkubwa Prof akasafishwa jambo litaleta dowa baya sana kwa serikali na ndio maana wenye akili wanahepa maamuz ya bunge kwasababu azimio walilo litoa litawatafuna wenyewe take from me.

CAG ni mtu hatari sana kucheza na cheo chake kwakuwa nimkono unao tafuta matumiz mabaya ya serikal mpaka bunge sasa lazima awe na kinga Labda niwaulize nani amewahi jiuliza why spika anapambana na Huyu prof? Je issue ni hii hii au kuna siri nzito?

Wapo. Watu wanaamini Mkuu ndia alie amuru bunge litekeleze haya nataka niwaambie jambo hili limemkwaza hata Rais maana anashangaa nini kinaendelea na ili kuwa mbali na mgogoro huu amewaacha wale matapishi yao wenyewe. Rais hana ugomvi Wala hana mgogoro wowote na Prof Assad. Ila watu wanajuwa tu yao.

Yote tutayajuwa niswala la Muda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How can you intimidate someone who audits your accounts? Of course the CAG is above the bunge ni vile tu alikuwa anawaheshimu. Na akisema I dhaifu lazima ni dhaifu kweli kwa kuwa anawaaudit.
Sasa wanataka wamlazimishe awasifie?
Na amekataa kuwasifia, kawaambia ukweli. Hii ingekuwa awamu ya Nyerere ama Kikwete mambo yangekuwa shwari kwa kuwa wanaekewa ukweli unahitani ufanyiwe kazi lakini siyo awamu hii ya kusifia tu!
 
lakini katiba imeeleza sababu za kumtoa huyu CAG, wala sio serikali itakayo mtoa ila ni katiba peke ake na hata kama kulidharau kweli bunge hebu tuletee kifungu alichokivunja kwa kufanya hivoo. ....remember huyu mpaka atolewe lazima tume iundwe tena na majaji wa nchi za madola wakiwepo ili uchunguzi uwe fair, huyu ana security of tenure kikatiba....hutolewa na katiba basi
Acha kupotosha, msio kuwa na uelewa wa mambo ndiyo mnashabikia ukosefu wa maadili na kupungukiwa kwa hekima kwa huyo Prof Assad wenu. Nyie subirini muziki toka Ikulu lazima ang'olewe huyu mkeuka maadili, kwanza anaonekana hana siri, yaani hana maadili ya kazi yake, nyie mtapiga kelele lakini serikali huwa haishikwi sharubu na huwa haichezewi kabisa hata kidogo, just be alerted mtaona maamuzi very soon. Na endeleeni kumpa kichwa maji huyo Prof wenu. Huwezi kubishana na serikali, serikali ni mfumo na mfumo una mkono mrefu sana, yaani huwezi ukalidharau bunge ukadhani eti wewe una linda professional professional gani hiyo inayoruhusu kudhihaki mhimili mkuu wa nchi????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
System inafanya kazi zake. JF huwa haibagui. Tuendelee tu
 
Mkuu unajua humu kuna watu wanajifanya wanajua na vingereza ushenzi kisa wanafanya kazi nje ya nchi au mashirika fulani wanafkr wanaupeo mkubwa wa akli af wengine Kama hawana akli.... Mtu analeta hoja et CAG ni msomi aliyebobea, ooh CV yake kali.. stupid kabisa, asa kuwa na hvo vitu ndo atukane bunge alaf bunge likae kimya..no no no !! hyo apana aisew....bunge ni mhimili wenye nguvu sana kikatiba, ndo mana kila raisi anayekuja lazima abane hyo angle ya bunge kwanza...bunge lina uwezo wa kupindua kila kitu na kukigaragaza chini...hata hyo power ya CAG inalindwa na bunge , leo hii hoja inaweza pelekwa bungeni ya kufumua fumua power ya CAG na kila kitu kikaenda sawa
Hata kumtimua kazi CAG si kazi ngumu kama tunavyodanganyana ni kazi rahisi tu ukisoma viz
 
Prof. Assad has put his hands where he shouldn't. So he must go! Kama anaamini ana haki na msimamo wa kutukana wenzake ajue na wenzake wana msimamo wa kumkataa. Anawang'ang'ania wa nini? Au alifikiri ni yeye tu mwenye msimamo? HE MUST GO!!!!!!
 
Habari ambazo sijazithibitisha. Prof Assad anaonewa tena wanao muonea sio kwa masilahi ya Taifa ila wanayo yajuwa wao.

Pia watu wanasema kuwa spika anamtega Rais ila kama tunavyo juwa Rais ni taasisi hawezi kukurupuka kumuwajibisha CAG maana kama ilivyo semwa hapo awali italeta mtikisiko mkubwa sana wakikatiba hivyo Mh Rais anatumia kila uwezo alio nao pasipo kushawishi Bunge kuacha jambo hili lipite nalo ila watakutana kwenye kamati za cc

Wapo watu wanasema Rais amsimamishe kiukweli watunga katiba walikuwa makin sana wakijuwa kuna siku litaibuka bunge kama la sasa kutaka kufanya mambo yao. Sasa ili Rais amsimamishe kuna takiwa kuwe na hoja ila hoja nzito sio hoja hii nyepesi ya spika. Wenye mamlaka wanauliza tusi au neno dhaifu maana yake nini na hapo ndipo bunge limeonekana kuchemka. Pia mchakato wakumuondoa CAG sio wakitoto maana wanatakiwa majaji wa nne walio iva kufanya uchunguz na sio kama zao za bunge sasa kiukweli kabisa kama rais akiunda hiyo Tume upo uwezekano mkubwa Prof akasafishwa jambo litaleta dowa baya sana kwa serikali na ndio maana wenye akili wanahepa maamuz ya bunge kwasababu azimio walilo litoa litawatafuna wenyewe take from me.

CAG ni mtu hatari sana kucheza na cheo chake kwakuwa nimkono unao tafuta matumiz mabaya ya serikal mpaka bunge sasa lazima awe na kinga Labda niwaulize nani amewahi jiuliza why spika anapambana na Huyu prof? Je issue ni hii hii au kuna siri nzito?

Wapo. Watu wanaamini Mkuu ndia alie amuru bunge litekeleze haya nataka niwaambie jambo hili limemkwaza hata Rais maana anashangaa nini kinaendelea na ili kuwa mbali na mgogoro huu amewaacha wale matapishi yao wenyewe. Rais hana ugomvi Wala hana mgogoro wowote na Prof Assad. Ila watu wanajuwa tu yao.

Yote tutayajuwa niswala la Muda tu.
Huyu akitoa kauli siyo ya kupuuza.

Wabunge wa CCM watakuwa wamerudisha heshima yao kama wataanzisha mchakato utakaowezesha speaker kuondolewa. Speaker kwa sasa analidhalilisha Bunge na anasababisha Rais kuchukiwa kwa sababu watu wanadhani kila anachokifanya ameagizwa na Rais, jambo ambalo siliamini.
 
kama kweli magufuli ni rais wa wanyonge na msafi kwanini kwenye taarifa za ufisadi anapenda kuficha ficha na kuwa mkali?
 
Acha kupotosha, msio kuwa na uelewa wa mambo ndiyo mnashabikia ukosefu wa maadili na kupungukiwa kwa hekima kwa huyo Prof Assad wenu. Nyie subirini muziki toka Ikulu lazima ang'olewe huyu mkeuka maadili, kwanza anaonekana hana siri, yaani hana maadili ya kazi yake, nyie mtapiga kelele lakini serikali huwa haishikwi sharubu na huwa haichezewi kabisa hata kidogo, just be alerted mtaona maamuzi very soon. Na endeleeni kumpa kichwa maji huyo Prof wenu. Huwezi kubishana na serikali, serikali ni mfumo na mfumo una mkono mrefu sana, yaani huwezi ukalidharau bunge ukadhani eti wewe una linda professional professional gani hiyo inayoruhusu kudhihaki mhimili mkuu wa nchi????
Huelewi hata ulichokiandika wewe, ulimsikiliza CAG alichomaanisha katika neno dhaifu! naona umetoa mapovuuu, kwani Prof. Assad hata kama akitolewa nafasi yake wewe unanufaika kitu gani?
 
Back
Top Bottom