nilitoka kidogo JF, ile narudi tu kitu cha kwanza nakutana nacho.....hamadi.....ni fitina za DiniKoloniKristo NA DiniKoloniIslam. kama nilivokwishasema huko nyuma diniKoloni hazina lolote la maana la kumsaidia mwana wa Afrika zaidi ya chukizo, fitinisho, hasidisho, uuajisho, unafkisho nk nk. Ni jambo la kuchukiza na kuhusunisha sana kuona kwamba, kila mara waafrika watanzania wanapokuwa wanajadili jambo la msingi na maana kubwa kwa mustakabali wa TAIFA LA WATANZANIA na waafika kwa ujumla, inspirational point inayotumika ni DiniKoloni...kumbuka hizi ni dini zile zile zilizowabaka bibi zetu, zilizowaasi babu zetu, zilizowashika watumwa waafrika wenzetu, dini baguzi zilizoongoza, na bado zinaongoza, imani chukizo kuwa waafrika ni manyani yasiyostahili hata kuoana na mzungu wala mwarabu. Hadi leo wamiliki wa Dini Koloni wanawatupia waafrika maganda ya ndizi kaa nyani ili tuyarukie mithili ya tumbili. Lakini hatuoni haya yote, DiniKoloni zimetumika kuhalalisha mauaji ya waafrika huko Nigeria, huko Misri, huko Somalia, milipuko Huko Kenya, huku Dar, kumwagiwa tindikali huko zanzibar, Arusha nk nk. Leo hapa DiniKoloni zinatumiwa na kina Big Show na SimiyuYetu kama kete ya kutimiza malengo ovu ya kuwagawa maskini wa Tanzania kwa nia ya kuendelea kuwatawala kikoloni na kuwaibia hadi chupi zao za ndani. DiniKoloni ni Laana Kubwa kwa Mwana wa Afrika.