Press conference ya ACT-Tanzania

Press conference ya ACT-Tanzania

SURVIVAL OF THE WILD~BEAST IN THE MOUTH OF CROCODILE We'l never never join there [HONGERENI WAMANYEMA] CDM SHALL NEVER BROKE!OR DEVIDED
Oooh, do you belong to chaggas party ee? Ngoja mnyolewe kwa kijinga cha moto
 
Chadema ikifa wazee wale sijui watapata wapi hela ya kutumia act inaiua chadema.
 
Huu utitiri wa vyama vya upinzani ni wala haujengi kabisa!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app

Mpaka hapo ccm wanakribia kufanikiwa 7bu kura zitawanywa na Waanzisha chama watapewa chao maisha yatasonga! Hizo mambo inasemekana zilikuwepo huko ZAIRE enzi y a MOBUTU SSESEKO vyama vingine viznaanzishwa kwa Malengo maalum ya Watawala,,!
 
Kwahiyo ACT-New Zealand ni sawa na CCM ndiyo maana iko against upinzani. Ahsanteni kwa kuwaelewa
 
Nianze kuwapongeza kwa juhudi zenu za KUUA mabadiliko kwa kigezo cha kuleta mabadiliko.

Jina la Chama chenu kwanza linaonyesha namna ambavyo hamna uhalisia na maisha na tamaduni za kitanzania. Katika nchi ambayo mamilioni ya wananchi wanazungumza lugha safi na maridhawa ya Kiswahili ninyi mmekuja na jina la "KIMAGHARIBI". Hapa ndipo ninapovisifu vyama vya CCM na CHADEMA kwa kuheshimu lugha yetu ya Taifa. Ni rahisi Zaidi kwa sisi wakulima na wafugaji kuelewa lugha yetu ya Taifa kuliko lugha ya "kimagharibi"Jina hilo linafanana na baadhi ya majina ya taasisi za kimaendeleo za kimagharibi (Maarufu kama NGO's)


Kuna namna ambavyo majina ya vyama yanasadifu yale yale yaliyomo kwenye sera zake kwenu ninyi CHAMA CHA MABADILIKO NA UWAZI (CHAMAU au CMU au ACT). Kwa akili ya haraka haraka mabadiliko ni jambo ambalo ni endelevu (yanaweza kuwa hasi au chanya) na sio kitu cha mara moja! Ninyi ndio mlihubiri na kutuaminisha kuwa kuna mabadiliko mkiwa kwenye baadhi ya vyama(Mwigamba na Wenzio) leo mmebadilika nini ili tuwaamini?

Mapambano ya mabadiliko ya kweli hayakuanza leo ni ya kihistoria. Kwa kumbukumbu za haraka haraka mabadiliko yalianzia maeneo ambayo wananchi walipambana na UKOLONI na WAKOLONI. Tazama ramani halafu utambue kuwa ni MIKOA gani ambayo watu walipambana na WAKOLONI na ni ipi WAKOLONI walikuwa marafiki na kucheza nao NGOMA. Kuna mahusiano makubwa kati ya mikoa iliyopambana na UKOLONI na MABADILIKO ya MAGEUZI Tanzania!!


Kama alivyotangulia kusema role Model wangu(Julius Kambarage Nyerere) dhambi ya Usaliti ni mbaya ni sawa na kula nyama ya mtu! Ukuaji ni maumivu na unahitaji uvumilivu! Ninyi mpendao honey moon na pesa za Kuhongwa na kina Rostam na Nimrodi Mkono kazi kwenu. Honey Moon ikiisha kumbuka mtaachika tena!!
 
Karibu ACT, karibu kwenye mbio ndefu zenye kukatisha tamaa kutokana na ubabe wa CCM, kama umekuja kwa nia njema tunakuombea kheri kwani lengo ni moja tu,kumkomboa Mtanzania na kumfaidisha na rasilimali zilozopo tofauti na sasa zinapofaidiwa na wachache, lakini kama umekuja kukomoa chama fulani au watu fulani, nakushauri kajitafakari upya.
WATANZANIA WAMECHOKA WANATAKA MABADILIKO YA KWELI.
 
huyo mwenyekiti Limbu alikuwa CUF,akakimbilia ADC,nako tayari amehasi sasa ni ACT!kweli huu ni muungano wa waasi ambao utadumu tu iwapo jumapili mbili zitakuja kwa pamoja!
 
Historia inaonyesha vyama vinavyoanzishwa kwenye ubavu wa vyama vikuu vyenye Wabunge wengi havistawi, mfano CCJ ilitokana na CCM na kile kilichotokana na CUF (nimekisahau) vyote vimefubaa.

Tunategemea na hiki pia kusinyaa shortly!
 
hiki chama kama kitaoboa mwaka itakuwa ni sawa na mlima kilimanjaro kuhamia dsm,chama kimejaaa wahuni na wasafiri watupu,leo huyu mwenyekiti wa muda kila chama kipya kinapoanzishwa lazima ajiunge nacho na wafuasi wao wengi hawajui wamefuata nini kwenye hicho chama,wengi wao wana njaa na wachumia tumbo



A
 
Karibu sana act uwazi kwa wa tanzania ndio wanaoutaka sio kama wale wanaowatazama wenzie wamekuja kuwafifiza na kuwapoteza kwenye ulimwengu wa siasa wa tz wamekwisha wa pokea kabla ya kujitangaza
 
Oooh, do you belong to chaggas party ee? Ngoja mnyolewe kwa kijinga cha moto
NOT CHAGGA BUT ONE WITH TRUE GUT OF REAL CHANGES AND GROWTH OF ALL TANZANIANS and not just only fews to relax and hold everythings that worths,cheat u with khanga,7000,and much much blah! blah!
 
Watu na akili zenu mnaanzisha chama kwa nia ya kupambana na CDM!!
Hivi kweli watu wakikubali hayo mageuzi/mapinduzi itatuchukua muda gani tena kuwaondoa mafisadi MaCCM???
Malengo yenu ni kudhoofisha upinzani, nyinyi ni masaliti wa ajabu, laana zetu wapenda Ukombozi zitawaandama!!
 
Halafu ni kwa nini cdm hawakitaki hiki chama cha act kwani kimewashika wapi au kunasehemu kimewafungia njia wasipite? Jamani tujiulize kunani pale cdm na watu wao act ndiokinaanza wala hakina mbunge wala diwani au serkali za mitaa kwa nn ukisakame chama ambacho bado kinajitangaza kwa wa tz? Mm naona kunakitu wanakiofia act mpango mzima viva act viva
 
Utitiri wa vyama hautasaidia kuleta mabadiliko ya kweli ni ubinafsi na uchu wa madaraka. Wanatafuta njia ya kupata ruzuku. Na huyo Limbu ni mala** wa siasa mara CUF( aligombea ubunge Jimbo la Temeke 2010), akaenda ADC Alikua katibu mkuu na kuzunguka mikoani kukitangaza na leo yupo Act- Tanzania (mwenyekiti Taifa). Watanzania tusiwe wajinga tufikiri kwa makini juu ya mustakabali wa taifa leo.

Nawasilisha
Kamanda Seneta
 
Kosa kubwa la pili alilolifanya Zitto ni hili la kuanzisha chama kipya, ninaamini hana washauri wazuri na wala yeye mwenyewe binafsi hana maono ya mbali.Wanaopinga ukweli huu wasubirie 2016 wataelewa ninamaanisha nini. Yetu macho.

Hiyo nafasi ya uwenyekiti unakaimu tuu au ni ya kudumu maana Zitto akija ataitaka kwa nguvu
 
Huyu Limbu vipi? Kabla hajamkabidhi H-Rashidi uenyekiti wa ADC ameibukia ACT kumshikilia mwingine uenyekiti? Ama kweli njaa ni kitu mbaya sana.
.
 
Back
Top Bottom