Press conference: Lowassa apelekewa ujumbe mzito

Press conference: Lowassa apelekewa ujumbe mzito

Mfukuzeni kwenye chama.unatuambia nini sisi kama unalea mwizi na wewe c mwizi kwani kuna tofauti gani kati ya El,chenge na JMK.nyie wote wezi tu ipo siku yenu,
 
Niseme wazi kwa mimi siegemei upante wowote ila nipenda Tazania na ningependa kuona nchi yangu inaendelea kuwa ya amani mshikamano na utulivu tuliozoea. Hata hivyo Reading Between the Lines, nashawshika kusema kuwa mwandishi wa habari hii pamoja na nia zake nyingine ambazo hazipo wazi yeye ndiyo hasa anataka kusababisha uvunjifu wa amani na mshikamano wa nchi hii. Uandishi wake ni ule ule wa kulenga wenye majibu marahisi kwenye masuala ambayo yanahitaji weledi na utashi wa hali ya juu kuyaongelea. Watanzania hawapo katika enzi hizo anazoziandikia, kunauelewa wa hali ya juu saa juu ya nani mkweli na nani hasa anataka kuvunja nchi hii. Tunajua huenda unafuata njia za wengine waliotoa matamshi kama hayo na kupewa UDC huenda nawe ukapata lakini sidhani kamabado nafasi hizo zipo, na pia tyle hiyo nayo pia inakaribia kupitwa na wakati. Waache Watanzania kwa wingi wao wajutie maamuzi yao wenyewe hata kama wakichagua Jambazi ni wao lakini siyo wewe kutoka usingizini na kutujazia ukurasa mambo yale yale. Tunatambua wapo watanzania wengi wenye sifa za kuliongoza taifa hili na wakati ukifika wananchi watafanya maamuzi yo sahihi.Kauli kama hizi zenu hatari kwa mshikamano na amani ya nchi yetu kulikojaza mafuta pikipiki na kweda kumuunga mkono mtu tunayedhani anafaa au hafaui. Ni vyema sasa watu wanaofikiria kutoa matamshi kama haya ambayo kimsingi ndiyo chanzo cha kuchochea uvunjifu wa amani na mshikamano wa nchi kujitathimini wenyewe endapo hata hizo sifa za kutoa matamshi kama hayo wanazo. Lipi ambalo unadhani mtazania atakuamini nalo kuwa wewe ni mzalendo kweli na unahaki ya kusimama mbele ya umma kusema uliyoyasema. Narudia Urais ni Jambo kubwa ambalo siyo kila mtu anaweza kuamka kutoka ajuvyo nakuanza kuropoka. Acha amani ya nchi yetu tafuta kazi ya kufanya. TUTAAUA WENYEWE NANI ANAFAA MUDA UKIFIKA
 
mbona waliojitangaza kutaka urais wapo ila kla cku anatajwa huyu lowasa! naanza kuamin kuwa huyu jamaa ana power
Mkuu wengi Tu wameshatangaza nia, akiwemo yule wa kimya kimya lakini CCM (Vuvuzela & company) wanahangaika Na EL ambaye bado hajatangaza even though nia ipo. Mtachokaaaaaaa
 
Nashangaa chama kikongwe kama ccm kuruhusu kila anayejiona ana mapenzi na chama kutoa ushuzi hadharani. Haya hayakisaidii chama bali inaonyesha upeo mdogo wa viongozi wake. Kama mkuu wa wilaya alipandishwa cheo - wakati EL alimwona hafai - hayo ni matakwa ya JK na hatujui alitumia vigezo gani. Ndiyo maana hatusongi mbele

Kitu kimoja ambacho CCM hawakijui ni kwamba kauli zote wanazotoa dhidi ya Lowassa zinampa umaarufu badala ya kumharibia!
 
Kweli kabisa watu wazuri tukikaa kimya watu wabaya kama wewe mtaihodhi nchi hii na kujipa HATIMILIKI huku tunawaangalia mkiendelea KUUPEPETA!
KWA KIFUPI MZEE, NENDA KAWAAMBIE WANAFIKI WENZIO KUWA HAYA YA LOWASSA SI MAIGIZO NA MNACHOFANYA NI KUJARIBU KUZUIA MAFURIKO KWA MIKONO! POLENI SANA!

Kinachowatesa CCM ni hofu kubwa kwa Lowassa, vijana kama hawa na akina Makonda plus Nape ndio itakuwa mwisho wao na hawatokaa wasikike popote!!
 
viongozi wa chama kuendelea kumsema mh.EL ni kuvunja kanuni na maadili ya chama.
Kumchonganisha kiongozi aliyeambiwa muda bado kwa watu ni sawa na kuzidi kumpatia umaarufu maradufu.
Kiongozi yeyote ndani ya CCM anayemchokonoa Mh.EL katika kipindi hiki ambacho chama kimepiga marufuku ya kampeni na kujinadi,hakika atakuwa asiye na akili timamu.
Sawa kusemana,lakini walau kwa kutumia akili na si kwa hotuba ndefu isiyokuwa na maana yeyote.
Si vyema na wala si lazima kuita watu na kuanza kumsema senior wako kwa mwamvuli wa UV-CCM.
Sidhani kama hiyo press comference ilikuwa kwenye schedule ya chama.

Kweli kabisa mkuu! Sana sana ni hofu tu na wanajua ikiwa EL atapata hiyo nafasi ndo itakuwa mwisho wao!!!
 
Lowassa ni fisadi Kwa mujibu wa kauli zenu mbona mnashindwa kumshgulikia MNA dola kila kitu. Mnacholinda hapa no ufisadi uliyofanyika miaka kumi mnaungana bila kujua kilicho waunganisha. CCM without Lowassa rest in peace.

CCM miti yote inateleza, muda si mrefu nyani atadondoka chini na ndo itakuwa mwisho wake!
 
CCM NI GENGE LA WAHUNI,,,,AMBALO LIMEIFANYA NCHI KUWA GHETO... HAKUNA MWEMA NDANI YA CCM SULUHU NA MWISHO WA HIZI SINEMA NI KUWAONDOA TU MADARAKANI NA KUWAWEKA MUFILISI WENYE CCM NA VIBARAKA WAO,, USA NA UN WATATUSAIDIA KUWAWEKEA VIKWAZO HAWA CCM DUNIANI KOTE... NA INABIDI HIKI CHAMA CCM KIPIGWE MARUFUKU NA OFISI ZAO ZIBAKI kuwa makumbusho ya taifa..
 
Nawashangaa sana waandishi wetu....wao wanaenda enda tu kwenye mikutano hadi ambayo haina hadhi wala tija!!

Lakini pia nimshangae huyo mwanaUVCCM kwa kutokujitambua.... Labda awe anataka nafasi kama zile za akina Makonda. Tofauti na hapo ni ujinga uliotopea kujadili jina la mtu mmoja kwa zaidi ya 98% ya Press conference... tena bila kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya mhusika!!

Nitawadharau sana wale watakao amini tuhuma dhidi ya Lowassa zinazotolewa na haya "machuma ulete" tena bila ushahidi wa kueleweka...
Kila mtu anaweza kuongea ujinga wanaouongea lakini kuweka kumbukumbu sahihi watanzania wanahitaji ushahidi wa hayo yote!!
 
Nawashangaa sana waandishi wetu....wao wanaenda enda tu kwenye mikutano hadi ambayo haina hadhi wala tija!!

Lakini pia nimshangae huyo mwanaUVCCM kwa kutokujitambua.... Labda awe anataka nafasi kama zile za akina Makonda. Tofauti na hapo ni ujinga uliotopea kujadili jina la mtu mmoja kwa zaidi ya 98% ya Press conference... tena bila kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya mhusika!!

Nitawadharau sana wale watakao amini tuhuma dhidi ya Lowassa zinazotolewa na haya "machuma ulete" tena bila ushahidi wa kueleweka...
Kila mtu anaweza kuongea ujinga wanaouongea lakini kuweka kumbukumbu sahihi watanzania wanahitaji ushahidi wa hayo yote!!

This is a legal offense (tot); a defamation case... Haya machuma ulete yakiburutwa mahakamani nadhani huu ukanjanja utaisha....!!!
 
AKSANTE mtoa hoja kwa maoni yako.Nafikiri kuna haja ya watia nia kuruhusiwa mapema ili watu wamjadili na kutoa maoni na wasiwasi wao,naamini nao utajibiwa kwa hoja si matusi kama ya Gwajima la sivyo wengi mtachunguzwa mali zenu mkitukana watu.
 
dah kweli kuimba taarabu kugumu...nimejaribu kufuatilizia mipasho yako ulioandika hapo hadi nimechoka nimeishia njiani maana kila 'mpasho' unao mpasha Mzee Ngoyai ma-CCM yote yanafanya.

ndiyo ile habari ya kuona kibanzi katika jicho la mwenzio wakati kwako kuna boriti.

CCM yote chafu jamani waTZ tufike mahali tufanye mabadiliko. this chama has to go vinginevyo tutaendelea kuumia tu.
 
watanzania wanatakiwa kumpuuza edward lowassa


Nani msafi ccm, mbona wote ni makazi, kuhusu lowassa-kukaa kwenye utumishi wa uma kwa miaka 30,sio hoja, katiba haizuii, mbona wapo wengi tu ccm, mzee kingunge alikaa miaka mingap? Tukiingia madarajayaleseni, lazima tuanze na wewe, kama una ushaidi wa ufisadi wa lowassa, mbona haujaupereka kwa vyombo vya dola, iam ashitakiwe,
 
.
Hivi vitoto vya mitaani vikishamtukana EL, vinazawadiwa ukuu wa wilaya. hivi ni nani mwenye mmlaka na kugawa hivi vyeo visivyosomewa? nahisi huyo ndie mfadhili wa kila mbaya wa EL na kwa maana hiyo yeye ndio mbaya kiongozi.
.





Wadhamini wa hivi vikundi vya mbwa mwitu wa kumshambulia Lowasa ni hawa waliopo kwenye madaraka :
Baadhi ya Mawaziri wanaotumia uwaziri wao na pesa za umma kuusaka urais akiwemo wasiri mkuu mwenyewe.
Lowasa anapigwa vita na kundi lenye nguvu ya kimadaraka ndio maana wanatengeneza njama za kutuma vijana watoe matamko ya kumdhalilisha Lowasa na hakuna mtu wa kuwauliza wala kuwakemea.

Sasa mwaka huu tunataka tuwaonyeshe kuwa hii nchi sio ya watawala peke yao .Na kwamba wananchi ndio wanaochagua viongozi.
Maadam Lowasa ana watu ndani ya CCM na pia kundi kubwa zaidi nje ya CCM patachimbika tu kama fitina ndio zitafuatwa kwenye maamuzi ya Chama chao.

Kwa mwenye macho ya kuona na akili ya kutambua mambo bila kuangalia maslahi ya kuhongwa vyeo ni ukweli kuwa Lowasa ana nafasi kubwa ya kushinda nafasi ya urais ndani na hata nje ya CCM.Ndio maana mahasimu wake wanataka kutumia kila njia ya kumuangamiza kisaikolojia na kimwili pia lakini bado Mungu anawaonyesha watanzania wengi kuwa Lowasa ndiye alama ya amani na utajiri wa Tanzania.
 
Kama mlijua yote hayo ilikuwaje bado ni mbunge, mwenyekiti wa kamati nyeti bungeni, na hata nafasi zote alizozishika baada ya kula hela za AICC? Japo mimi najua AICC ilijengwa wakati wa EAST AFRICA COMMUNITY Lowasa akiwa bado kijana na alikuwa umoja wa bijana na TANU. Lowasa amekuwa mkurugenzi na sio msamizi wa ujenzi wa jengo la AICC.
Kwa vile alitoka hapo na kuwa waziri hadi waziri mkuu huo unaoongea ni upuuzi ma unastahili kupuuzwa.
Issue ya afya ni siri ya mtu na daktari wake tupe ukweli na sio kuropoka. Mrema alipoambiwa anaumwa aliweka vyeti wazi wewe weka vya Lowasa. Mbona JK alianguka majukwaani wakati wa kampeni lakini hadi sasa ni raisi?? Mkikosa cha kuongea muwe mnakaa kimya. Watanzania mnao onhea nao sio wale wa 1954, hilo mlijue kabisa.
Naomba niweke angalizo hapa mimi sio mwana Ccm na wala sijawahi kuwa mwana Ccm na sitokaa niwe mwana Ccm kutokana na unafiki wenu, ila imenilazimu kuandika haya kupinga huu ujinga wa kitoto mnaoanza kuwaletea watu wenye akili.

Yote uliyoyazungumza hapa ni tisa,kumi ni hili,ccm wanajua Lowassa ni fisadi na mwizi aliyekubuhu,mbona hawampeleki mahakamani kumshitaki?mbona hawamfukuzi uanachama?Ni hatua gani chama kimemchukulia zaidi ya kumpa vyeo lukuki?Ifike hatua ccm na sarakasi zenu zote watanzania wa leo sio wa 2005.
 
Mungu alishakataza ufisadi katika Ardhi. Iweje Mungu huyo huyo amteua fisadi kuwa Rais wa nchi?

Nyie ccm ni chama la wanafiki,kama mlijua ni mwizi na fisadi mbona hamjawahi kumshitaki wala kumwambia alete hati miliki za malizake zote na kumfanyia upekuzi kama mnavyotaka kumfanyia Gwajima? Ni muda wa kufa huu lazima mrushe miguu kabla ya kukata roho
 
Mungu alishakataza ufisadi katika Ardhi. Iweje Mungu huyo huyo amteua fisadi kuwa Rais wa nchi?
Mkuu Kama ni hivyo mbona huu mtambo wa kuzalisha mafisadi -ccm hatujauteketeza toka kwenye USO wa dunia
 
Back
Top Bottom