Press conference: Lowassa apelekewa ujumbe mzito

Jan 2, 2015
87
0
watanzania wanatakiwa kumpuuza edward lowassa
attachment.php


ndugu wanahabari, poleni na hongereni sana kwa kutimiza majukumu yenu mazuri ya kila siku katika ujenzi wa nchi yetu.

Ndugu zangu nimewaita hapa ili kutoa maoni yangu kwa taifa nikiwa kama mwanachama hai wa uvccm na ccm, pia kama raia mzalendo wa nchi yangu,

napenda nichukue fursa hii kutoa wito wangu kwa wanaccm wenzangu na wananchi wote wa tanzania, waliopo ndani na nje ya nchi yetu, wa kumpuuza ndg edward lowassa na timu yake kutokana na historia yake isiyoridhisha na ukikwa ji wake wa taratibu za uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi na hata tume ya taifa uchaguzi.

Hii ni kutokana na hali ilivyo ndani ya nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, yametokea mambo ambayo kimsingi sio mazuri kwa mustakabali wa nchi yetu, ambayo kwa kiwango kikubwa yameanza kusababisha mgawanyiko baina yetu na hata kutishia upotevu wa amani, umoja na mshikamano wetu kama watanzania.

Mambo haya yamekuwa yakifanywa sana na ndg edward lowassa ambaye kwa muda mrefu ameonyesha kuitafuta nafasi ya uraisi kwa nguvu na hata kwa kuvunja taratibu za chama chake na nchi kwa ujumla, jambo hili sio jema na nikiwa kama mwanachama wa muda mrefu wa chama cha mapinduzi, kiongozi na raia mwema wa nchi yangu, nimeona nichukue nafasi hii

kama mzalendo ili niweze kuwakumbusha na kutoa rai yangu kwa wananchi wenzaangu kwamba wawe makini na wasihadaike na propaganda zake bali wanahitajika kumpuuza ili kuweza kudumisha umoja wa nchi yetu.

Napenda kuwakumbusha wananchi wenzangu kwamba wanapaswa kuikumbuka historia ya ndg edward lowassa vizuri na kwa kina sana, historia ya maisha yake na siasa zake kwa ujumla,

mara nyingi amekuwa ni mtu anyetajwa kuhusika na ubadhirifu pia ufisadi mbalimbali unaofanyika ndani ya nchi, ukiwamo richmond ambapo mara zote amekuwa akiwaadaa wananchi kwamba alijiuzulu ili kulinda heshima ya serikali na chama chake jambo ambalo sio kweli, taarifa ya tume ambayo iliundwa na bunge kufuatilia sakata hilo iliweka wazi namna waziri mkuu alivyohusika moja kwa moja katika ubadhirifu huo vikiwamo viambatanisho vya vinote vyake, mawasiliano, na namna jinsi zoezi zima la ugavi ulivyoendeshwa. Lakini pia amehusika na ufisadi katika ujenzi wa jengo la ukumbi wa mikutano ya kimataifa aicc.

Lakini pia watanzania wanapaswa kufahamu na kukukmbuka namna jinsi alivyokuwa mtu mwenye kutumia vibaya madaraka yake, akiwa waziri mkuu alikuwa ni mtu mkorofi na mwenye maamuzi ya kukurupuka, alikuwa ni mtu mwenye kuwafukuza watu kazi kwa uonevu papo kwa papo bila hata kuwapa haki ya kuwasikiliza (right to be heared au natural justice)hasa wanapokataa kulinda maslahi yake , aliwah kumdhalilisha na kutaka kumfukuza kazi dc aliyekuwa ameteuliwa siku tatu tu na sasa ni mkuu wa mkoa, ndg mongela.


Ametumia madaraka yake vibaya kwa kujilimbikizia mali mbalimbali ikiwamo umiliki wa ardhi mkubwa hasa jijini dar es salaam kwa mfano eneo la peninsula pale masaki ambapo amejipatia viwanja kadhaa na ushahidi amejenga nyumba ya ubalozi wa south africa, akiwa waziri mkuu alishiriki kuamuru uvunjaji wa ghorofa masaki kwa sababu linaziba nyumba yake kukosa upepo kutoka baharini, huku akidanganya umma kuwa ghorofa lile limejengwa kinyume na utaratibu, amekuwa mtu mbadhirifu wa mali za umma sana kwa kutumia madaraka yake kwa mfano amejimilikisha majengo ya ppf na kumpa mtoto wake.

Ni mtu msanii sana na si mkweli hasa kwa utaratibu wake wa kukwakupua mipango ya serikali na kusema amefanya yeye, akiwaaminisha watu kwamba amekuwa anaisimamia ama kuanzisha yeye jambo ambalo limekuwa likifanywa na serikali kama timu, mara nyingi anazungumzia shule za kata ambazo zimeanza tokea enzi za mkapa wakati wa waziri ndg joseph mungai, pia amekwapua mradi wa maji ziwa victoria akisema ameanzisha yeye jambo ambalo sio kweli kabisa, mradi ule ulisainiwa na ndg benjamini mkapa mwaka 2002 wakati huo waziri wa maji akiwa ndg pius ng'wandu.

Ndg wanahabari nashangaa kuona mhe lowassa akijinasibu kwa hoja yake ambayo sio nzuri kwake lakini yeye amekuwa akiwadanganya wananchi kwamba ana maamuzi magumu, maamuzi yake hayakuwa magumu bali ni ya kukurupuka na yasiyokuwa makini yaliyolenga kujikampenia uraisi ambayo yamelitia taifa hasara sana, kwa mfano kuvunja mikataba kinyume cha sheria ambayo baadae ameitia hasara serikali kwa kulipa fidia mfano mradi wa maji wa jiji (city water) amevunja majengo masaki ambayo hayo yote serikali ilibidi kutoa kodi za wananchi ili kulipa fidia amelitia hasara taifa, hayo ni kwa ufupi tu lakini yapo mengi sana.

Kwa hakika wananchi wanapaswa kukumbuka kwamba hii sio mara ya kwanza kwa ndg edward lowassa kugombea urais, aliwahi kufanya hivi mnamo mwaka 1995 lakini jina lake liliondolewa katika mchakato na baba wa taifa mwl nyerere kutokana na rekodi zake za utumishi wa umma kujaa dosari nyingi na kupoteza uaminifu zikiwamo kujipatia utajiri mkubwa akiwa bado kijana sana huku vyanzo vyake vya utajiri vikiwa havijilukani na havifahamiki.

Wananchi wanapaswa kukumbuka kwamba ndg edward lowassa amejidhihirisha wazi kuwa ni mtu mwenye tamaa kali ya mali na madaraka, wakumbuke ni wastani wa miaka ishirini sasa ndg lowassa amekuwa akiutafuta urais wa nchi hii kwa tamaa zake binafsi, na mara zote amekuwa akiutumia utajiri wake na marafiki zake kufanya kampeni na kuyashawishi makundi mbalimbali ya watanzania kumuunga mkono ili kufikia malengo yake binafsi, anatumia baadhi ya vyombo vya habari hasa vile vya habari coorperation vinavyosimamiwa na ndg hussein bashe kumsafisha na kumtangaza nchi nzima ili aweze kuonekana anakubalika, lakini pia amekuwa akitumia fedha alizoliibia taifa letu kufanya harambee mabalimbali hususani kwnye taasisi za kidini na makundi mengine ya kijamii, kuchapisha fulana, kununua watoa matamko na kuyatengeneza makundi mbalimbali yafike kwake kusema yanamshawishi na kumchangia achukue fomu za kugombea urais, kumbe ni uwongo na maigizo yaliyopitiliza kwakuwa makundi hayo na fedha anayaandaa yeye mwenyewe na rafiki zake.

Na ndio maana mara nyingi yamekuwa yakipingwa na mamlaka husika, kwa mfano ndani ya siku nne makundi yote yamekusanyika kwake hii inaonyesha ni nmna gani jambo hili lilivyotengenezwa kwa maigizo, kibaya zaidi wanawadanganya wananchi kuwa kuna vijana wa bodaboda wametoka mbalali kuja kumshawishi dodoma, hivi ni kweli ndg wananchi inawaingia akilini kwamba vijana wetu hawa waache kutafuta ridhiki ya kujikimu na kuwalipa vipande mabosi wao bali waweke mafuta na kutembea kilometa nyingi kuja dodoma, lakini walipitia njia gani kwa msafara mkubwa huo hadi usionekane hata na traffic.

Sasa ni hatari kwetu wananchi kuacha kuyaapuuza mambo kama haya ya mtu anayetafuta uraisi kwa uwongouwongo, uraisi ni jambo kubwa sana, imeshangaza sana kuona wachungaji kutoka mikoa mbalimbali na mabango yao ghafla wanakutana nyumbani kwa ndg lowassa, walijipanga muda gani, ni vigumu saana wachungaji kutoka sehemu tofauti wakawa na wazo moja kwenda kwa lowasa wakawa na wazo moja kuandika bango, harafu wakawa na wazo moja la kwenda tarehe moja na kwa pamoja wakakutana inaonyesha dhahiri wanawanadanganya wananchi na kuyatumia majina ya mashekh na wachungaji kwa uwongo ili kupata madaraka,

nataka wananchi watambue namna ambavyo ndg lowassa amekuwa anafanya utapeli wa kuungwa mkono huku akiyaita mafuriko kwamba hawezi kuyazuia, ndg wananchi yale sio mafuriko bali ni mazingaombwe ama kiini macho, yote anayafanya ili kufuta madhambi yake na aonekane ni mtu anayetakiwa na kukubalika na wananchi. Napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kukumbuka usia wa baba wa taifa alivyosema "muogopeni kama ukoma mtu anayetafuta kwenda ikulu kwa kutumia fedha, hatufai" sasa tuziipuuze hizi propaganda zake za hovyo ili kulisaidia taifa letu, hauwezi kusema nilikuwa mwizi na sasa siwezi kuibaa tena la hasha! Wizi ni tabia na wahenga walisema tabia haina dawa.

Lakini pia ndg edward lowassa bado anatumikia adhabu ya kifungo cha kutokujihusisha na maswala ya kampeni za urais , adhabu hiyo imetolewa na kamati kuu ya ccm baada ya kuanza kampeni kabla ya muda na mpaka sasa adhabu hiyo bado haijaisha, wananchi wanapaswa kumpuuza ndugu lowassa kwakuwa tayari mpaka sasa ameshakiuka masharti ya adhabu hiyo dhahiri kwakuwa ameendelea na kampeni chafu ambazo umma umeshuhudia, sikukuu ya chistmas iliyopita, ndg lowassa aligawa fedha kwa wajumbe wa nec na mkutano mkuu nchi nzima, katika hali ya kushangaza ndg lowassa aliwagharamiaa vijana wa ccm wasiojitambua kwenda lituhi kijijini msibani kwa komba, aliwapa usafiri, malazi, posho na fulana walizozivaa msibani kama sehemu ya kampeni zake, ndg watanzania wenzangu hili ni jambo la kusikitisha sana kwa mtu anayegeuza msiba wa mpendwa wetu kuwa sehemu ya kampeni zake.

Hivi juzi amekuwa akifanya matendo ya kuigiza ya kuandaa makundi mbalimbali aliyoyaita yanatekeleza agizo la mkt kwenda kumshawishi, mkt alisema watu washawishiwe kwa kufuata utaratibu na sio kwa uongo na uvunjaji wa kanuni, yale ni mazingaombwe kwakuwa makundi hayo ni feki na ameonyesha dharau kwa chama chake hivyo basi moja kwa moja atakuwa amepoteza sifa za kuwa mgombea wa ccm. Lkn pia ndg lowassa amekiuka hata taratibu za tume ya taifa ya uchaguzi ambayo bado haijatangaza rasmi kuanza kwa uchaguzi, yeye ameanzisha movement inaitwa 4u ambayo inafanya kampeni kwa niaba yake nchi nzima, hii si sawa na haitendi haki kwa wagombea wengine wenzake wanaofikiria kugombea wa ndani na nje ya chama chake , inapoteza usawa na haki ya kidemokrasia (fair political grounds ) pesa anazotumia kufanya kampeni zake zinatengeneza mazingira yasiyokuwa na usawa dhidi ya wagombea wenzie wasio na uwezo wa kiuchumi, hivyo kulinyima taifa kupata kiongozi mwenye sifa stahiki. Wananchi wenzangu nawaomba msidanganyike na hizi sanaa za ndg lowassa kwamba anakubalika sio kweli, nchi hii ni kubwa sana na bado watanzania wengi tokea enzi za mwalimu nyerere mpaka sasa wanamjua kuwa ni kiongozi mbadhirifu na fisadi.

Lakini natoa wito kwa watanzania wampuuze ndg lowassa kwakuwa hana mapenzi mema na taifa lake kwakuwa anajua fika swala la tatizo la afya yake linalomkabiri lkn amekuwa akiwaadaa wananchi kwa kutengeneza vipande vya picha kwa bandia ambavyo vinaonyesha akiwa anakimbia kwa kujivutavuta, kwa hali yake hatoweza kulitumika taifa hili lenye changamoto nyingi na nzito, tunatakiwa kujifunza kwa mataifa mbalimbali yaliyopata kuweka viongozi wenye matatizo ya kiafya jinsi walivyokabiriana na matatizo baadae zilivyowagharimu kisiasa na kiuchumi, kwa mfano zambia rais levy mwanawasa na michael sata, malawi rais bingu wa mutharika, na mataifa mengineyo pia, afya ni jambo la msingi kwa kiongozi na si la kubezwa au kuangaliwa katika jicho kengeza.

Ndugu wanahabari mnalo jukumu la kuwakumbusha watanzania lowasa ni mwanasiasa na mfanya biashara moja kati ya kosa kubwa ambalo watanzania watalifanya na watalijutia maisha yao yote ni kumpeleka mfanya biashara huyu aliyepelekea kupangwa mpangwa wa ardhi peninsula ya msasani kwa faida yake, ikulu katika taifa ambalo linalasimali nyingi zinaitaji kutengenezewa mpango mzuri na endelevu kwa manufaa ya watanzania na sio wachache wanaotamani ona zinawaneemesha wao tu .kumpa nchi mfanyabiashara mlafi kama lowasa ni kuchezea shilingi katika tundu la choo...

Kuna kila sababu ya kumuita lowasa mwanasiasa asiyetosheka maana kwa muda aliotumikia taifa hili kwa zaidi ya miaka 30. Yapo maswali ya kujiuliza kwa nini hatosheki? Kuna kipya kipi ambacho hajakifanya miaka 30 atakifanya ndani ya miaka mitano ya uraisi? Jibu linabaki moja tuu ni tamaa ya madaraka na mali, ndio tafsiri yake. Mwalimu julius kambarage nyerere aliwahi hoji pale ndg. Lowass alipojitokeza kugombea uraisi wa nchi mwaka 1995.

Hata kufikia sehemu ya kupelekea chama kuhengua jina lake katika ugombea. Ni lini ndg. Lowassa amejirekebisha katika tabia yake ya urafi na kujilimbikizia mali ? Ushauri wangu , bwanalowasa usigombee uongozi huu wa nchi hii iliyo na watu wema, wapenda maendeleo na wanaotamani kuona maendeleo iwe salama. Fedha ukizopeleka uingereza na kuanza kufuatiliwa na intelligensia ya uingereza kazitolelee majibu. Nyumba za kifahari unazonunua hadi vyombo vya nje vinajiuliza unapata wapi fedha zote hizi unapswa kuvitolea majibu.

Baada ya kutoa wito huo kwa wananchi wa kumpuuza ndg edward lowassa na kumchukulia kama ni mtu asiyejua analolifanya, napenda kuchukua fursa hii kumshauri ama kumuonya ndg hussein bashe mjumbe wa,mkutano mkuu wa ccm na mtendaji mkuu wa kampuni ya habari corporation ambaye amejipa mamlaka ya kuwa msemaji wa ndg edward lowassa, kwa kutoa matamko dhidi ya viongozi ambao wanatambulika kikatiba, ya kuwapinga na kutumia maneno yasiyofaa, hii inaonyesha utovu wa nidhamu alionao dhidi ya viongozi wake na chama kwa ujumla, kitendo cha ndg bashe kumshambulia katibu mwenezi wa ccm kwa kutoa agizo ambalo muhusika amelitii, kimemdhalilisha sana, ameonyesha kukurupuka na kukosa adabu.

Mh. Nape ni mwenezi wa chama na kwamba anapozungumza juu ya masuala ya chama lazima ajue kuwa huyu ni mtu mwenye mamlaka ya kusema katika chama. Kama amekosea sio yeye wa kusema hayo. Utaratibu upo wa kwenda kupeleka malalamiko na kwamba chama kitashughulikia kama kilivyoshughulikia malalamiko mengine.kitendo hiki kimenitia shaka juu ya uwezo wa mtu mwenye nafasi aliyojitaja kuwa msemaji wa ndg lowassa.

Shaka kubwa ni pale kauli zao zinapopishana na ndg. Lowassa juu ya kuwakusanya watu. Wakati bwana lowassa anadai hawaandai watu lakini ukweli nikwamba anajiongopea mwenyewe maana yule aliyejitambulisha kama msemaje wake amethibitisha kuwa wanaandaa watu. Ushahidi wa wazi ni juu ya kauli ya nndg. Bashe kuwa wamekusanya saini za wajumbe zaidi ya 1700 wa mkutano mkuu wa ccm na kwamba wanajipanga kwenda kumshindikiza bwana lowassa juu ya kuchukua fomu. Maswali mengi nimekosa majibu yake, yule mjumbe aliyepo kule mwambani tanga alipataje hiyo karatasi na kusaini fomu ya kumuunga mkono kama si kweli kwamba alipewa sababu za kusaini fomu hiyo?

Swali hata huyo aliyekwenda kumsainisha huyo mjumbe, alifanyaje kama si kwamba kuna kikao kilitangulia ambacho kilipanga mikakati ya kwenda kuwatafuta. Hapa nazungumzia wajumbe wote waliosemwa kusaini karatsi hiyo ambao wanatokea vijiji vya wilaya za nchi nzima maana wajumne ni wengi sana na kwa bahati mbaya hawaishi mtaa mmoja au nyumba moja. Na hata kama wangekuwa wanaishi pamoja basi wangelazimika kuitwa sehemu na kuambiwa madhumuni ya zoezi hilo. Ndg waandishi hata ninyi niliwaita hamkujikuta mpo ndani ya eneo hili pasi kujua agenda mliyokuja ifuata.

Natambua pia ni uhuru wake kumuunga mkono ampendaye lkn asubiri muda sahihi wa kikatiba kuhusu maswala hayo, na baada ya vikao kufanya uteuzi wa viongozi wasafi wanaofaa, watanzania wanapaswa kuwapuuza watu kama hawa kwa maana mara nyingi wanakuwa wanakurupuka bila ya kujijua, anastahili kuwa mtulivu aendelee kukua akijifunza siasa na asitumiwe kwa manufaa ya wachache wasiothamini watanzania tulio wengi.

Mwisho mshaurini bwana lowassa kuwa usafi wa kiongozi si kupiga picha na mheshimiwaraisi, viongozi wa dini, maaskofu na masheikh au viongozi wakimila. Usafi wa kiongozi unaenda sanjari na historia ya maisha aliyoishi kiongozi huyo. Kama uliishi katika uongozi wako ukiiba na kushindikiza maovu yafanyike kwa faida yake, basi jua wazi watanzania sisitunayokumbuku nzuriya uovu ulioutenda. Hivyo usitamani kujifanya unapenda sana na viongozi kwa kuwaandaa wapiga picha . Waombe radhi watanzania kwa yale uliyowakosea.

Pia naipongeza kamati kuu ya ccm kwa kutoa adhabu za kikanuni na kuendelea kama siku zote kusimamia sheria, taratibu na miongozo yake katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea uchaguzi mkuu, napenda kumtia moyo mkt wa chama na wajumbe wote pamoja na wanaccm wote kwamba sisi sote tupo pamoja nao, wafanye maamuzi ya haki kama sikuzote pasipo kumuhofia mtu yeyote, chama kisimamie kanuni, taratibu na miongozo yake ili kuweza kuwasaidia watanzania kama chama tawala kuweza kupata kiongozi bora.

Mwisho upo msemo usemo mambo hayaendi vibaya kwa sababu watu wabaya wanayafanya la hasha ila ni kwa sababu watu wazuri wamekaa kimya...kwa niaba ya watu wazuri wote wanaoitakia mema nchii hii nimeamua kuvunja ukimya dhiidi ya watu wabaya wanaotaka kulipeleka taifa hili sehemu mbaya

asanteni kwa,kunisikiliza
nawatakia kazi njema.

Comrade francis heri hoza mjumbe kamati ya utekelezaji ya balaza la uvccm mkoa wa morogoro na mwenyekiti mstaafu wa shirikisho la elimu ya juu la wanachama wa ccm mkoa wa morogoro.
 

Attachments

  • 1429008174963.jpg
    File size
    63.1 KB
    Views
    26,506

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
14,178
2,000
Yapo majengo yameendelea kujengwa hasa nyumba za kuishi watu.

Lowasa alihusika na ufisadi ujenzi wa jengo la ukumbi wa mikutano AICC?! Haya si yalijengwa Lowasa akiwa labda primary school? CCM msiruhusu wajinga kama huyu hoza kuvuruga watu. Lowasa atuhumiwe kwa haki si uzandiki kama huu.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,507
2,000
Kama mlijua yote hayo ilikuwaje bado ni mbunge, mwenyekiti wa kamati nyeti bungeni, na hata nafasi zote alizozishika baada ya kula hela za AICC? Japo mimi najua AICC ilijengwa wakati wa EAST AFRICA COMMUNITY Lowasa akiwa bado kijana na alikuwa umoja wa bijana na TANU. Lowasa amekuwa mkurugenzi na sio msamizi wa ujenzi wa jengo la AICC.
Kwa vile alitoka hapo na kuwa waziri hadi waziri mkuu huo unaoongea ni upuuzi ma unastahili kupuuzwa.
Issue ya afya ni siri ya mtu na daktari wake tupe ukweli na sio kuropoka. Mrema alipoambiwa anaumwa aliweka vyeti wazi wewe weka vya Lowasa. Mbona JK alianguka majukwaani wakati wa kampeni lakini hadi sasa ni raisi?? Mkikosa cha kuongea muwe mnakaa kimya. Watanzania mnao onhea nao sio wale wa 1954, hilo mlijue kabisa.
Naomba niweke angalizo hapa mimi sio mwana Ccm na wala sijawahi kuwa mwana Ccm na sitokaa niwe mwana Ccm kutokana na unafiki wenu, ila imenilazimu kuandika haya kupinga huu ujinga wa kitoto mnaoanza kuwaletea watu wenye akili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom