Precision Air na matatizo yao: Wanaelekea wapi?

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Feb 10, 2006
4,235
13,434
Ndege ya Precision iliyotarajiwa kuruka kwenda Mwanza mnamo saa 9 alasiri imeshindwa kuruka kuelekea Mwanza kama ilivyotarajiwa.

Awali wasafiri walielezwa kuwa ndege hiyo itaondoka saa 11 na boarding time itakuwa saa 9 alasiri. Mambo yalizidi kuwa ya mkanganyo ambapo wasafiri waliingia katika ndege hiyo na kukaa kwenye viti vyao kwa zaidi ya saa huku rubani akijikamua kuiwasha bila mafanikio.

Ngoma iligoma kabisa na wasafiri wakaombwa wavute subira wasishuke kwakuwa mafundi walikuwa bado wanakorokochoa. Ngoma ikachomoa kuwaka na wakalazimika kuwambia kuwaomba wasafiri washuke mida ya saa 1 hivi na kuwapeleka Lounge ili wasaidiwe namna nyingine ya kutoka.

Hadi naandika ujumbe huu ni saa 2 dakika 25 usiku (Tanzania) na ndege hiyo haijaondoka kwenda Mwanza na hakieleweki nini kitatokea.

Hili ni tukio linaloonekana kurandana na matatizo yaliyowakuta wenzao Community Airlines.

Wahenga walisema: Mwenzio akinyolewa....
 
mambo ya kichaka hayo
ndege zote low profile zitakwama maana nasikia jamaa amekuja na system kali ya ulinzi mambapo inasaidia kuharibu system zingine.
poleni sana
mtaenda kulala kempiski? au?
 
Haya madege mabovu yata tuua jamani
You're damn right man. Dege lilikuwa bovu. Si suala la Bush tusimtafute ubaya. Wametafutiwa usafiri mbadala na wameondoka dakika 30 zilizopita (wakati muda wa kuondoka ulikuwa saa 9 alasiri!).

Ndiyo hali halisi. Si Community wala Precision wenye afueni
 
haya madege mabovu yanaingiaje Bongo kila siku? kuna lingine la ATCL nasikia linakuja kutoka kwa akina joji wea.Bongo kweli kunahitajika ufagio wa nguvu upite.Haya mitambo ya umeme used,cheses za mabasi used,dege la Rais used.
 
Haya madege mabovu yata tuua jamani

Na yakiua tunasema ni kazi ya Mungu. Mie naona Mungu anasingiziwa mambo mengine, hii ni kazi ya mikono ya wanadamu, ni sisi tu tunajitakia. Ukiambiwa ndege mbovu mie nadhani ubadili mawazo yako na kutafuta namna nyingine kwani ndege si sawa na gari kwamba "anyway ikizima njiani tutasukuma". Hivi ndege ikizimika hewani huko itakuwaje, kama si kushuka jumla jumla! Mambo mengine si vyema kujaribu!
Long Live Tanzania.
 
Habari zilizotufikia muda si mrefu kampuni ya ndege ya PRECISSION air ambayo wamekuwa na ubia na kampuni ya KENYA AIRWAYS wameanza kufuta safari zao mara kwa mara kama yaliyotokea kipindi cha nyuma na ATCL
akiongea na muandishi wetu na kutuonyesha baadhi ya safari zilizofutwa walisema kwa kweli sijui nini kimetokea;embu angalia mimi nilikuwa nije majuzi na ndege toka shinyanga wakaifuta wakaleta siku inayofata kesho yake naelekea mwanza naamka asbh bila hata kuwa na huruma ya kutupigia tunafika airport wanasema ati tumekancel ndege.;kibaya zaidi tukaomba tuamishiwe kwenye ATCL wakadai wana ndege jion hawawezi kufanya hivyo...baadhi wakafanya fujo wakapelekwa ..tuliporudi jion tunaambiwa ndege imefutwa jamani hii kampuni siyo kabisa ndipo nikaanza kuchunguza tatizo ni nini tukaambiwa wameanza kuwa na tatizo la mafuta hata mshahara kaka wametulipa tarehe kumi wa mwezi uliopita....alisema dada mmoja kazi kweli kweli.......
Naona umefika wakati wa kurudi tena ATCL JAMANI...mi nimeapa sirudi tena uko precission......alisema abiria ...
Habari zaidi zinasema saari za mwanza zinaendelea kuwa cancelled mpaka jaana huku baadhi ya watu wakinyimwa hata kufaulishwa huu ni ushenzi
 
Pamoja na kusua sua kwa uchumi, mpinzani wao karudi sokoni hivyo wanagawana wateja. Soko ni dogo sana hivyo wakati wote wanaombea ATCL ife kabisa. Usije shangaa hata kusuasua kwa ATCL kwa kipindi chote kulikuwa na mkono wa mtu ili kuhakikisha kuwa haitoi upinzani wa kibiashara.
 
mwaka juzi nilikata tiketi na kupanda precision air ATR 42, niliripoti airport saa moja ili niondoke saa 2 from dsm to kia. however, tuliombwa msamaha kuwa kuna technical problem, hivyo tukaondoka saa tatu, na rubani akatutangazia kuwa kila kitu kiko ok. tukiwa hewani just kama 10 minutes ngede ikaanza kutoa moshi mweupe nyuma, yaani ndani ya ndege, moshi ukawa mwingi na ikalzamu rubani airudishe ndege back to mwalimu nyerere airport. kile kihoro kikanifanya niachane na ile safari ingwa walikuwa wako tayari kutufaulisha kwenye ndege nyingine. sababu ya kutoa moshi eti walisahau grease juu ya air conditions wakati wanafanya service, hivyo ndege ilipowashwa na kuruka ile grease ikaana kuuungua na kutoa moshi.

sijawahi kuipanda tena hiyo precision na tiketi nikawaachia
 
baadhi ya matokeo ya economic downturn jamani.Na bado tutasikia mengi.

Kutangaza kukubwa na economic crisis si dhambi, tatizo ni pale ambapo hizi safari zinavunjwa ghafra. Hivi hakuna namna ya kuwashtaki kudai fidia kwa kuwapotezea abiria muda (Value for Money)?
 
nyie acheni mambo ya majungu ndani ya hii jf.hayo ni majungu ya kibiashara.Kuna mtu kawatuma mupigie debe ATCL au ndege nyingine.Ni jambo la kawaida kusitishwa kwa safari hasa kama kuna tatizo.Nyie mnataka wawaletee ndege yenye matatizo then mkipata tatizo mseme Ooh walikuwa wapi,Oo serikali, Oooooooooooooooo!
 
Sio majungu. Ni kweli, ndege huahirishwa pale kunapokuwa na tatizo - kwa ajili ya usalama wa abiria.

Lakini unaelezaje pale unaporipoti kwa ajili ya safari na kuambiwa ndege imeshaondoka? Binafsi hii imenitokea mara mbili kwa Precision Air. Reporting time ni saa 12 na nusu asubuhi, departure saa mbili. Nikafika airport saa 12 na dakika 45 asubuhi nikaambiwa ndege imeshaondoka! That day 15 passengers tulikuwa stranded. The next time that happened to me, 9 passengers were stranded.

Hili nalo ni jungu? It happened to real people - frequently.

Ingelikuwa ni mara moja moja watu tusingililalamika, kwa kuwa inaanza kuwa ni the rule rather than the exception - flight cancellation - ndio maana watu wana voice frustrations zao na hii hali. Myself included!

Nyau
 
Jamani mdau mkubwa wa hii kampuni ana kesi huko mahakamani. Pesa ya kuendeshea kesi inapatikana wapi kama sio kuanza kuminya minya hizi za mafuta. Hata mzee wa vijicent si unaona kapunguza madereva siku hizi anaendesha mwenyewe!
 
Habari zilizotufikia muda si mrefu kampuni ya ndege ya PRECISSION air ambayo wamekuwa na ubia na kampuni ya KENYA AIRWAYS wameanza kufuta safari zao mara kwa mara kama yaliyotokea kipindi cha nyuma na ATCL
akiongea na muandishi wetu na kutuonyesha baadhi ya safari zilizofutwa walisema kwa kweli sijui nini kimetokea;embu angalia mimi nilikuwa nije majuzi na ndege toka shinyanga wakaifuta wakaleta siku inayofata kesho yake naelekea mwanza naamka asbh bila hata kuwa na huruma ya kutupigia tunafika airport wanasema ati tumekancel ndege.;kibaya zaidi tukaomba tuamishiwe kwenye ATCL wakadai wana ndege jion hawawezi kufanya hivyo...baadhi wakafanya fujo wakapelekwa ..tuliporudi jion tunaambiwa ndege imefutwa jamani hii kampuni siyo kabisa ndipo nikaanza kuchunguza tatizo ni nini tukaambiwa wameanza kuwa na tatizo la mafuta hata mshahara kaka wametulipa tarehe kumi wa mwezi uliopita....alisema dada mmoja kazi kweli kweli.......
Naona umefika wakati wa kurudi tena ATCL JAMANI...mi nimeapa sirudi tena uko precission......alisema abiria ...
Habari zaidi zinasema saari za mwanza zinaendelea kuwa cancelled mpaka jaana huku baadhi ya watu wakinyimwa hata kufaulishwa huu ni ushenzi

Mama mia usishangae hiyo no economic crisis cha kufanya ni kujifunga mkanda tu
 
nyie acheni mambo ya majungu ndani ya hii jf.hayo ni majungu ya kibiashara.Kuna mtu kawatuma mupigie debe ATCL au ndege nyingine.Ni jambo la kawaida kusitishwa kwa safari hasa kama kuna tatizo., Oooooooooooooooo!

Naamini si vidole vyako kuandika haya.....japo la kawaida kusitishwa kwa safari?Unajua kwanini watu wanapanda ndege?Na hawapandi basi?Unafikiri kwa sababu wana mapesa mengi?Mtu anaangalia muda....ndio maana anapanda ndege sasa mtu anapanga kuwa dar saa nne kwenye mkutano,au anafanya connection ya ndege mchana kwenda J'burg...unapo sitisha safari una maana gani...how do u compasate(Ukizingatia tanzania hamna utaratibu huo)Tuliza kichwa kabla ya ku type.
 
Jamani mdau mkubwa wa hii kampuni ana kesi huko mahakamani. Pesa ya kuendeshea kesi inapatikana wapi kama sio kuanza kuminya minya hizi za mafuta. Hata mzee wa vijicent si unaona kapunguza madereva siku hizi anaendesha mwenyewe!

75% Ya share anazo yeye...yuko anahangaika na kesi....lazima mambo yawe magumu kwenye uendeshaji wa mali zake.
 
Tuliza kichwa kabla ya ku type.

hahahahahah tehetehekwikwikwi nicheke mie hivi JF ndio imekuwa sehemu ya kutangaza ushindani kati ya haya mashirika mawili ya ndege? halafu unamwambia mwenzio atulize vidole kabla ya kutaipu kwani hapa si kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake alimradi asivunje sheria? hahahahahaahha mwache atoe maoni yake bwana.

Ila mie kubwa nililoona hapa kuna matangazo ya biashara kiasi kwamba hao wenye mashirika wangewasiliana tu na wamiliki wa JF wakalipia basi wakawekwa sehemu ya matangazo kuliko kutumia nyie wadau wao kubishana hapa.
 
Naamini si vidole vyako kuandika haya.....japo la kawaida kusitishwa kwa safari?Unajua kwanini watu wanapanda ndege?Na hawapandi basi?Unafikiri kwa sababu wana mapesa mengi?Mtu anaangalia muda....ndio maana anapanda ndege sasa mtu anapanga kuwa dar saa nne kwenye mkutano,au anafanya connection ya ndege mchana kwenda J'burg...unapo sitisha safari una maana gani...how do u compasate(Ukizingatia tanzania hamna utaratibu huo)Tuliza kichwa kabla ya ku type.

Yani naungana na wewe kwa asilimia mia moja. Yani kusitisha safari si jambo la kawaida hata kidogo. Nakumbuka kuna siku fulani nilikuwa natoka Dar kuelekea Shinyanga. Nilifika Airport saa kumi na mbili asubuhi kwa ajili ya safari ya saa moja. Chakushangaza ni kwamba tulikaa pale Airport mpaka saa moja na nusu hatujaondoka. ilipofika saa mbili tukatangaziwa kuwa Pression ya kwenda Shinyanga haita kuwepo. Tukaambiwa tutaondoka na Ndege itakayokwenda Mwanza saa nne na nusu asubuhi. Yani hata nilichokuwa nakifuata Shinyanga nilikikosa kwa sababu nilifika Mwanza saa Sita mchana tukatafutiwa basi la kutupeleka Shinyanga. Shinyanga nilifika saa kumi jioni ambavyo ni sawa sawa na mtu aliye ondoka na basi saa moja asubuhi na kufika shinyanga saa 11 jioni.

Ukweli ni kwamba Pression Air imeanza kusua sua siku nyingi sana.
 
Hata mimi nakumbuka hii safari ilikua na stori nyingi sana. Mi nilikua naelekea tabora na ilibidi nifike saa mbili usiku.
Haya si Majungu wala si matangazo ya biashara.
Watanzania kama tunataka maendeleo ya kweli lazima tuongelee kutambua vinavyotukwamisha na kukubali kuachana navyo na si kufagilia uozo.

kama mtu unakosea njia kubali kuelekezwa ili ufike uendako. Vinginevyo utalala njiani.
 
Back
Top Bottom