Abiria wa Precision Air waliokwama Bukoba kusafiri leo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
Abiria waliotarajia kusafiri kwa ndege iliyopata ajali Jumapili nje kidogo ya Uwanja wa Ndege wa Bukoba, sasa wataondoka leo kuelekea Dar es Salaam na Mwanza.

Wasafiri hawa ambao idadi yao ni 21 wa ndege ya Kampuni ya Precision, tangu Jumapili walikuwa Bukoba wakikaa hoteli ya ELCT, waliyopangiwa na kampuni hiyo baada ya ndege yake kutua kwa dharura ndani ya Ziwa Victoria, mita 180 kufika barabara ya kutua.

Katika ajali hiyo, jumla ya watu 19 walipoteza maisha, huku 26 wakiokolewa na wavuvi.

Abiria hao waliokwama Bukoba, hata hivyo hawatapanda dege kwenye uwanja wa mji huo, bali watabebwa na mabasi hadi Mwanza ambako wataendelea na safari ya Dar es Salaam na wale wanaoishia Mwanza, ndiyo watakuwa wamefika.

Mmoja wa Watendaji wa JamiiForums aliyekuwa miongoni mwa abiria waliotarajia kupanda ndege hiyo anaeleza kuwa Kampuni ya Precision imewataarifu leo kwamba wataondoka saa 4 kwa mabasi hadi Mwanza.

Anasema kuwa uongozi wa Precision umewaeleza kuwa watapanda ndege ya saa 3.15 usiku kutokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam.
 
Yaani wapande basi mpaka Mwanza halafu ndiyo nauli Yao ya ndege itakuwa imeisha ama?
 
Nauliza tena hivyo vifo 17 ni vipya ama? Maana Dunia nzima wanajua waliokufa wako 19
 
Yaani wapande basi mpaka Mwanza halafu ndiyo nauli Yao ya ndege itakuwa imeisha ama?
Nadhani wana jambo la msingi.Yawezekana kampuni haipendi kuwaonesha/abiria walione lile eneo walilopata ajali.Litawakumbusha uchungu na kuwaletea fadhaa au kuamsha hisia hasi juu ya usafiri wa ndege.Nimewaza tu.
 
jumla ya watu 17 walipoteza maisha, huku 26 wakiokolewa na wavuvi.
Mbon tunaambiwa 19 walipoteza maisha na 24 wamekua manusura baada ya bwana Majaliwa Jackson kujitoa muhanga/kujitosa ziwani na kwenda kuwaokoa, sasa mboni unatimix mkuu?
 
Back
Top Bottom