Precision Air na matatizo yao: Wanaelekea wapi?

Kwa nn wasizisimamishe wakuu?Au mnasubili lije liue ndo muanze kuunda tume za uchunguzi kwa nn serikali inasua sua kufanya maamuzi sasa?
 
Ndege ya Precision iliyotarajiwa kuruka kwenda Mwanza mnamo saa 9 alasiri imeshindwa kuruka kuelekea Mwanza kama ilivyotarajiwa.

Awali wasafiri walielezwa kuwa ndege hiyo itaondoka saa 11 na boarding time itakuwa saa 9 alasiri. Mambo yalizidi kuwa ya mkanganyo ambapo wasafiri waliingia katika ndege hiyo na kukaa kwenye viti vyao kwa zaidi ya saa huku rubani akijikamua kuiwasha bila mafanikio.

Ngoma iligoma kabisa na wasafiri wakaombwa wavute subira wasishuke kwakuwa mafundi walikuwa bado wanakorokochoa. Ngoma ikachomoa kuwaka na wakalazimika kuwambia kuwaomba wasafiri washuke mida ya saa 1 hivi na kuwapeleka Lounge ili wasaidiwe namna nyingine ya kutoka.

Hadi naandika ujumbe huu ni saa 2 dakika 25 usiku (Tanzania) na ndege hiyo haijaondoka kwenda Mwanza na hakieleweki nini kitatokea.

Hili ni tukio linaloonekana kurandana na matatizo yaliyowakuta wenzao Community Airlines.

Wahenga walisema: Mwenzio akinyolewa....

Naona Mkuu jamaa wamekisikia "KILIO CHAKO" wameleta ndege mpya saba aina ya ATR.

Makubaliano ya Precision Air yatuzwa

Makubaliano ya ununuzi wa ndege mpya saba aina ya ATR 42-500 na ATR 72-500 za shirika la ndege la Precision Air yamepewa tuzo ya Makubaliano Makubwa Kuliko Yote Afrika 2008.

Tuzo hiyo ya makubaliano hayo yenye thamani ya dola milioni 129 za Marekani, imekabidhiwa kwa shirika hilo na jarida la Airfinance katika hafla ya mashirika mbalimbali duniani iliyofanyika New York, Marekani jana, kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo.

Ni heshima kubwa kwetu kupata tuzo hii inayosimika utaratibu wetu wa kununua ndege aina ya ATR kuwa moja ya mipango madhubuti na ya mafanikio katika nyanja za usafiri wa anga kwa mwaka 2008, alisema Alfonse Kioko, Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air.

Tunapenda kuwashukuru washirika wetu wote, ATR, Citi na Finnfund ambao kwa pamoja wamekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha mpango huu na kwa juhudi, ujuzi na mafanikio yao, sasa tunaweza kuongeza safari zetu nchini na hivyo kusaidia kuendeleza sekta ya utalii na uchumi kwa ujumla, alisema.

Akizungumzia tuzo hiyo , Mkurugenzi wa Fedha wa ATR, Giovanni Tramparulo, alisema Tuna furaha kubwa kuona jinsi mpango wa ununuzi wa ndege za ATR unaofanywa na Precision Air ulivyopata tuzo mbili katika kipindi kifupi. Tuna furaha pia na jinsi benki zilizohusika zilivyo na imani na ATR. Precision Air iliyoanzishwa mwaka 1993 imeongeza safari na uwezo wa kubeba abiria ikitumia ndege kumi ambazo ni ATR 42-320 nne, ATR 72-210 tatu, ATR 72-500 mbili na Boeing 737 moja.
 
Hivi hawa jamaa bado wananunua ndege zenye pangaboi hadi leo?
Hivi hawajaona model mpya? Naona wamenunua Boeing 1 tu katika oda nzima hio!
 
Back
Top Bottom