Nawapa pongezi sana lakini wasiwasi wangu ni umri wa hiyo ndege na matengenezo yake yako vipi? Nawaomba maofisa wa TCAA waifanyie uchunguzi ndege hiyo kabla haijatua bongo. Ni ndege kubwa kwa safari za medium range kama south na Dubai. Keep it up precision.
Kumbukeni katika PA Kenya wana hisa 41% na huyo mchaga ana hisa 51%. TZ ina hisa .....
Let us support our lovely wing of Kilimanjaro(air Tanzania with a leased Airbus 320-214). Hii mapato yake tunauhakika yanarudi serikalini kwa maendeleo ya Taifa. Wasafiri tuwe na moyo wa utaifa.
Huyu mchaga wa watu kajitutumua na kuendesha shirika la ndege. Huyu ni mtanzania halali kabisa. Sasa wewe ndugu unasema tuwe na moyo wa utaifa, wakati ni serikali ndio kilibeep kuibinafsisha ATC, wakaiua ATC wenyeeeeeeeeewee, sasa alalamikiwe nani..??
ATC imeanza kufufuka, ila bado huduma mbovu. Ma-air hostess hawana adabu kwa abiria, wanavaa mashati yamepauka na kuchakaa, wazee kibao..!! ATC inalelewa na swala la kuwa na boeing pamoja na rubani bora i.e. Captain Mazulla. Otherwise, huduma za ndani ni mgogoro..!! Cha muhimu ni ushindani uendelee ili hawa watu wawe na discipline kwenye biashara.
Ila pamoja na kuitetea PW (PW ni code ya precisionair), ukweli ni kuwa, nao wawe serious katika kuajiri marubani. Wameajiri vitoto vidogo, vibrazameni yaani ni kasheshe tupu mtu ukiwa angani. Yaani kama una roho ya mshtuko, unaweza wahishwa ICU ukishatua.
Manake ndege inacheza sebene wakati wa kutua, mpaka unahisi utumbo unachomoka. Na hii si swala la udogo wa ndege, bali ni uwezo mdogo wa pilot. Hii imethibitishwa na wataalamu kadhaa wa anga, ambao wamecomment kuhusiana na huu uvamizi wa mabrazameni wa PW. Hapo kwa kweli, hata mimi naunga mkono mamlaka za anga kufuatilia kwa ukaribu huduma za anga.
Hayo ni maoni yangu..!!