Mbona hiyo posho ya katibu mkuu unaitetea sana?? Au unaona ni sahihi yeye kuipata?ccm haimpi mtu cheo kupitia JF kwa kutetea upuuzi ila endelea na jitihada za kutetea yawezekana nape akakuona ukamsaidia kutetea ulaji wa kundi flani
kwani nyoka anazaa mjusi?? huyu nae ni walewale, babake alishawahi kusema eti dawa ya babu wa loliondo ilikuwa kwenye ilani yao, mmmh!! simshangai zuzu mtoto.
Wazt ni wadanganyika anajua sisi ni watu wa kulalamika tu kwa hiyo anaweza kuropoka chochote tukalalamika na asiathilike kwa chochote/lolote...............siamini km kweli alistahilio kuwa w/mkuu, nadhani ilitakiwa nafasi hiyo iwe wazi tu kwani toka akalie kiti hicho bado sijaona kilichofanyika zaidi ya kubabaisha tu na kuhadaa watz................
ni wazo zuri...sisi kama CDM tutalifikiria , mie ndo ntakalo liwasilisha kwa katibu mkuu...worry notikishindikana kabisa kuondoa posho, CDM wachukue posho lakini zisinufaishe familia zao waanzishe clubs shule za msingi,sekondari na vyuoni kushughulikia matatizo yanayokabili makundi haya na ipendekeze cku ya jumapili au jumamosi kama siku ya kukutana na kupeana changamoto za kielimu kwa kuwashindanisha kwa mitihani na kuwafundisha haki za binnadamu,mwanafunzi;kisiasa kwa kuwajengea uwezo wa kujenga hoja na kutetea,michezo kwa kurefresh
kweli mkuu. Kimsingi kinachotokea hapa ni kujikweza kulikopitiliza. Na hili la utukufu ni kashfa nyingine kwa mwananchi. Maneno yanatumika bila kumaanisha uhalisia. 'Mheshimiwa mbunge ndani ya Bunge tukufu...' kiukweli yanahitajika mabadiliko.Ndugu raia Fulani, sisi wananchi tuliowachagua Wabunge (Waheshimiwa) ndio Wadharauliwa, hujabaini hili ndugu. Kama kweli hawatudharau wanafanya nini cha maana ili kutusaidia sisi???? Toka Bunge la kwanza hadi leo hakuna juhudi za waziwazi kumsaidia Mdharauliwa. Kama hawatudharau unafikiri kungekua na kauli kama "Hata mkila nyasi, Ndege ya Rais itanunuliwa." Leo umeleta hoja ya kulifuta jina la Mh. ambalo kimsingi lina wakweza bila sababu ya Msingi na kutufanya tulivae jila la Wadharauliwa. Ila mimi pia na leta hoja ya Kulifuta jina La Bunge TUKUFU. Lile Bunge letu lina UTUKUFU gani au labada mimi mafikirio yangu ni duni (ntakubali hili) kama kuna Mtu humu ndani na nje ya Jukwaa, atakapo kuja na kujaribu kuniaminisha UTUKUFU wa bunge letu. Sina uhakika, japo kuwa nilisha acha na kufuta imani yangu kwa dini za Kigeni, ila kama neno UTUKUFU, litaacha kama lilivyo then, ntaingiwa na mashaka makubwa sana na watu wanaohusishwa na neno hilo.
tutabadili mengi sana, hadi jina la nchi hii maana nasikia ni kuna jina la mtu na imani yake kwenye tanzanIAkwa mantiki hiyo basi hata salamu yetu ya kiswahili yaani SHIKAMOO!! na MARAHABA!! nayo inakuza matabaka kwani ilikuwa ni salamu ya mtumwa kwa bwana wake kwa hiyo tuwe tunasalimiana habari za asubuhu, mchana na jioni tuache yale mambo ya primary school shikamoo mwalimu!!
Wabunge na viongozi wa serikali huitana waheshimiwa, hivyo kutulazimu kuwaita hivyo. Ni waheshimiwa kwa lipi? Kuna tofauti gani kati ya raia huyo aliyekuwa anagombea ubunge mwaka jana na mwaka huu yupo mjengoni (kariakoo)? Ana kipya kipi cha kumzidi yule ambaye aligombea nae ama yule raia aliyempigia kura? Au ni hizo posho na hiyo mikopo na mishahara minono? Hakuna tofauti. Ifike muda sasa wabunge na viongozi serikalini, pawe na sera ya kuitana NDUGU
UNACHOKIZUNGUMZA KINA UKWELI, NAKUMBUKA WAKATI WA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA KWANZA NA AWAMU YA PILI MARAIS WALIKUWA WANAITWA 'WATUKUFU':bange: LAKINI ALIPOKUJA KAKA BENI AKAKATAA KUITWA MTUKUFU NDIPO LIKAANZA 'MHESHIMIWA' :israel:KWA UPANDE WA RAIS.HIVYO HATA KWA WABUNGE INAWEZEKANA TU, MBONA KWA RAIS IMEWEZAKANA?NA IWE HIVYO