Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 246
kumbe ujerumani inaRAISI.Zito ni mshauri wa rais wa ujerumani juu ya uchumi wa afrika-amekataa posho.
kumbe ujerumani inaRAISI.Zito ni mshauri wa rais wa ujerumani juu ya uchumi wa afrika-amekataa posho.
Sema wewe, unadhani hayupo?!kumbe ujerumani inaRAISI.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema suala la posho za vikao hasa kwa wabunge limekuzwa kuliko ukubwa wa jambo lenyewe. Pinda amebainisha kuwa, zipo baadhi ya posho ambazo haziwezi kutenguliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria, ikiwamo posho hiyo ya Mbunge hadi sheria na Katiba vitakaporekebishwa. Pia amewataka wabunge wawe wakweli kuhusu suala la kutaka kufutwa kwa posho zao za vikao, kwa kuwa pamoja na kupewa fedha hizo, bado hazitoshelezi mahitaji na majukumu mengi yanayomkabili Mbunge, jambo ambalo linawafanya wengine kuendelea kukopa. Amelieleza Bunge mjini Dodoma kuwa, pamoja na kwamba jambo hilo linazungumzwa sana na kushikiliwa kidedea na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto (Chadema), anafahamu kuwa wapo baadhi ya wabunge wa chama hicho ambao bado wanazimezea mate posho hizo za vikao.
Pinda alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF) aliyetaka kujua Serikali ina tamko gani kuhusu posho za vikao, suala ambalo baadhi ya wabunge wamekuwa wakilijadili na kutoa matamko yao dhidi yake na kusababisha kujenga fitna na kadhia kwa wabunge wengine kutoka kwa wananchi wao. "Katiba Ibara ya 73, inazungumzia masharti ya kazi ya wabunge, kwamba watashika madaraka yao na watalipwa mishahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa kanuni na kwamba kila mbunge ana wajibu wa kufuata sheria hiyo.
"Sasa hivi karibuni kumeibuka kadhia iliyoanzia kwa baadhi ya wabunge na vyombo vya habari na kusababisha fitna na wananchi wetu, naomba jibu mheshimiwa Waziri Mkuu," alisema Mnyaa. Waziri Mkuu, alikiri kuwa stahili za wabunge zipo kwa mujibu wa Katiba na Sheria nyingine zilizotungwa na Bunge. Alianisha kuwa, zipo posho ambazo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha hana mamlaka ya kuzirekebisha, kwa kuwa zipo kwa mujibu wa Katiba na Sheria, hivyo ili zibadilike, Katiba na Sheria hizo hazina budi kubadilishwa pia.
Lakini pia alisema zipo posho ambazo Katibu Mkuu ana mamlaka ya kuzirekebisha kwa jinsi anavyoona inafaa. "Katika kundi la posho za kwanza ambazo hadi sheria zirekebishwe wapo pia madiwani ambao hawana malipo ya aina yoyote zaidi ya posho ambazo ndizo zinazowawezesha kutimiza majukumu yao, hivyo mnapozungumzia posho mtambue kuwa kuna madiwani," alihadharisha. Alitolea mfano pia posho wanazopewa polisi, za chakula, kuwa huo ni utaratibu uliopo ndani ya Jeshi la Polisi ambao hauwezi kubadilishwa, kwa kuwa upo kwa ajili ya kumwezesha askari atimize majukumu yake.
"Jamani tuangalie na posho zenyewe tunazozingumzia, mfano makatibu wakuu wakati wa maandalizi ya Bajeti wamekuwa wakikesha, mimi nikikesha hadi asubuhi sawa, lakini sheria hizi zimeona ni vizuri watu wa aina hii kuwapa motisha, si dhambi hata kidogo kuwapa posho.
"Najua kumekuwa na maneno mengi kama vile kuna jambo kubwa, nashangaa suala hili lilivyokuzwa, lakini liko wazi kabisa ni masuala ya sheria, Katiba na utaratibu tu wa kufuatwa, kwani hata Spika wa Bunge akitaka kuongeza posho za vikao za wabunge hulazimika kwanza kumwandikia Rais kuomba kibali, huyu mbunge mnayempigia kelele posho hizo hata wakati mwingine hatumii mwenyewe," alisema Pinda.
Alisema hakuna Mbunge asiyefahamu kadhia wanayoipata ya kushikwa mashati na kuombwa fedha kila kukicha, hali inayowafanya fedha wanazopata kutowatosheleza na ndiyo maana posho hizo za vikao zinazolalamikiwa na kukuzwa, zimewekwa kwa ajili ya kuwasaidia wabunge hao kutimiza wajibu wao. Aliongeza kuwa, tamko la Serikali ni kuziangalia fedha hizo namna zilivyowekwa ili angalau zihuishwe na hata ikibidi kuziweka kwenye mishahara ya watumishi wakiwamo wabunge.
Akijibu swali la nyongeza la Mnyaa aliyetaka kujua ni hatua zipi Serikali inawachukulia wabunge ambao wamekiuka Katiba na Sheria zilizowekwa kwa kukataa posho hizo za vikao, Pinda alisema hakuna sababu ya kuwachukulia hatua kwa kuwa Zitto si mbunge wa kwanza kutaka fedha zake za posho zitumike katika matumizi mengine na kwamba hakuna mbunge anayekatazwa kuiandikia Hazina kuwa fedha zake za posho ziingizwe katika mipango ya maendeleo.
"Hofu yangu ni kukuzwa sana kwa jambo hili na ninajua hata wabunge wa Chadema wanazimezea mate fedha hizi za posho za vikao, ila hawana cha kufanya," alisema Pinda na kushangiliwa. Juzi Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani iliyosomwa na Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na baadaye Waziri Kivuli Zitto, ilibainisha dhamira ya kufuta posho zote za vikao kwa watumishi wa umma wakiwamo wabunge, jambo lililozua mjadala.
HabariLeo
Hapa naona Mkuu ameteleza. Serikali haiwezi kutoa posho kwa mbunge ili aweze kujipendekeza jimboni kwake. Pesa za kujipendekeza zinatakiwa ziwe zake mwenyewe na si ati anapewa posho kwa ajili hiyo. Kwa mfano, mbunge halazimiki kuchangia harusi, misiba, mabati n.k. katika jimbo lake. Akitaka kufanya hivyo, basi anatakiwa afanye kama tunavyofanya wengine, kwa kubana matumizi binafsi au kutumia kipato nje ya mshahara wako. Kuendekeza tabia hii kutaturudisha kwenye takrima. Mbunge anatakiwa kuibana serikali itoe huduma zinazohitajika na si kujifanya yeye ni mbadala wa serikali. Hao makatibu wakuu na watendaji wengine wa juu wa serikali nao wanapokesha ni sehemu ya kazi walioikubali. Motisha unatikiwa uwe ni jukumu na wadhfa aliopewa na si vibahasha. Tabia hizi ndizo zinazoturudisha nyuma. Kuendekeza vibahasha ndiko kunakochangia vikao visivyokuwa na tija, visivyoisha na vinavyohudhuriwa na wasiopaswa maana ulaji umewekwa mbele. Tujionee huruma.
Amandla........
Hapa naona Mkuu ameteleza. Serikali haiwezi kutoa posho kwa mbunge ili aweze kujipendekeza jimboni kwake. Pesa za kujipendekeza zinatakiwa ziwe zake mwenyewe na si ati anapewa posho kwa ajili hiyo. Kwa mfano, mbunge halazimiki kuchangia harusi, misiba, mabati n.k. katika jimbo lake. Akitaka kufanya hivyo, basi anatakiwa afanye kama tunavyofanya wengine, kwa kubana matumizi binafsi au kutumia kipato nje ya mshahara wako. Kuendekeza tabia hii kutaturudisha kwenye takrima. Mbunge anatakiwa kuibana serikali itoe huduma zinazohitajika na si kujifanya yeye ni mbadala wa serikali. Hao makatibu wakuu na watendaji wengine wa juu wa serikali nao wanapokesha ni sehemu ya kazi walioikubali. Motisha unatikiwa uwe ni jukumu na wadhfa aliopewa na si vibahasha. Tabia hizi ndizo zinazoturudisha nyuma. Kuendekeza vibahasha ndiko kunakochangia vikao visivyokuwa na tija, visivyoisha na vinavyohudhuriwa na wasiopaswa maana ulaji umewekwa mbele. Tujionee huruma.
Amandla........
Mkuu kinachoniudhi hapa ni jinsi hili suala la posho linavyoelezewa kama suala la kikatiba. Katiba yetu inasema kuwa wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa Katiba hii na kwamba watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Katiba hapa hailazimishi wabunge kulipwa posho. Katiba inasema kuwa watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Nina uhakika hiyo sheria iliyotungwa na bunge hailazimishi mbunge kulipwa posho. Bali itakuwa inasema kuwa mbunge anastahili (entitled) kulipwa posho. Sasa kun tofauti hapo kati ya kulazimishwa na kustahili. Hakuna mtu anayelazimishwa kulipwa. The way walivyo interpret hiki kifungu raises many questions than answers.
Mkuu kinachoniudhi hapa ni jinsi hili suala la posho linavyoelezewa kama suala la kikatiba. Katiba yetu inasema kuwa wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa Katiba hii na kwamba watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Katiba hapa hailazimishi wabunge kulipwa posho. Katiba inasema kuwa watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge. Nina uhakika hiyo sheria iliyotungwa na bunge haimlazimishi mbunge kulipwa posho. Bali itakuwa inasema kuwa mbunge anastahili (entitled) kulipwa posho. Sasa kuna tofauti hapo kati ya kulazimishwa na kustahili. Hakuna mtu anayelazimishwa kulipwa. The way walivyo interpret hiki kifungu raises many questions than answers.
Uko sahihi kabisa, Mkuu. Itakuwaje mtu aliyeomba nafasi mwenyewe leo atake kupewa motisha ili atimize wajibu wake? Kwa nini huo motisha uishie kwa wabunge peke yao? Kwa msingi huo basi na walimu nao wapewe posho kila wakiingia darasani, madereva kila wakikamata usukani, mafundi mchundo kila wakishika spana n.k. Ingawa nakubaliana nawe lakini hata kama hiyo katiba inasema ilipwe posho basi inastahili kubadilishwa. Wakati wakifanya hivyo waondoe na hizo posho za chakula kwa wanaovaa magwanda maana haijaleta mabadiliko katika utendaji wao wa kazi. Walipwe mishahara mizuri na wawajibishwe wasipotimiza wajibu. Kuwawajibisha si kwa kuwapa posho au ulevi wa bei poa!
Amandla......
Yaani kisingizio cha katiba is so cheap, ni kama hao viongozi wa serikali walivyozoea kutotolea maamuzi magumu kwa kisingizio eti kesi iko mahakamani. Mfano, Unaulizwa siku ya tukio flani ndugu waziri ulikuwepo nchini? jibu: Siwezi zingumzia hilo kwa sababu kesi iko mahakamani.
Hapa pia kuna tatizo katika katiba - Wabunge kujitungia mishahara na posho zao wenyewe si vema. Hata mimi nikipewa nafasi hiyo nitajipangia masilahi kibao!Mkuu kinachoniudhi hapa ni jinsi hili suala la posho linavyoelezewa kama suala la kikatiba. Katiba yetu inasema kuwa wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa Katiba hii na kwamba watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Mkuu umenikumbusha juu wakati Mbowe alipotaka majibu ya kina toka Waziri Nundu juu ya uwekezaji wa KADCO na msimamo wa serikali juu ya uwekezaji wa kampuni hiyo ambayo alisema imekuwa ikichangia dola 1,000 tu kwa mwaka. Waziri Nundu alilishangaza Bunge aliposema kuwa serikali imerekebisha kasoro hizo na sasa mambo yanaendelea mbele kwa mbele. Mbowe alipotaka maelezo zaidi akapigwa mwongozo. Hili la posho nalo tunapigwa danadana tuu hapa na majibu ambayo ni unfair, unjustied and unreasonable. Majibu ya maswali mazito, yanajibiwa so cheap.
Unajua siamini kama ni waziri mkuu ndiye alikuwa anaongea maneno hayo!