Dickson Ng'hily
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 473
- 508
Safi sana amejibu vizuri ujinga aliouliza Zakari juu ya kuwa wameshakopa hizo posho, amemwambia kama wapo wakopeshaja kupitia posho basi wanamatatizo kwa kuwa posho hulipwa baada ya kuhudhuria vikao.[/QUOTE]
Mkuu kama posho haiwezi kukopeshwa kwa kuwa inalipwa baada ya kuhudhuria vikao inakuwaje mshahara ukopwe, mshahara nao si unalipwa baada ya kufanya kazi au?
Mkuu Kimbunga...Mshahara kwa mawazo yangu madogo ni given na unatumika kama security, hivyo mwajiri anaweza kumkopesha mwajiriwa alafu akamkata kwa mshahara wake...Ila inategemea na makubariano yenu...Mwaka 2007 nilikuwa nafanya kazi kampuni moja na nikafiwa na mama yangu mzazi hapa Dar na tulitakiwa kuusafirisha mwili wake kwa maziko huko Musoma. Nilienda kwa mwajili wangu na kukopa mshahara wangu wa miezi miwili hivyo katika makubariano yetu ni kuwa nitalipa deni hilo kupitia mishara yangu itakayofuata. So kwa muda wa miezi miwili sikupata mashahara coz pesa yote iliishia kulipa mkopo...Ila si unajua mambo ya mjini, niliishi hivyo na hatimaye nikamaliza deni...Unajua wakati mwingine ukiwa na shida kama ugonjwa na msiba, unawezajikuta unakubali tu mashart ya namna hiyo hata kama yanaumiza...Yangu ni hayo mkuu...