Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Hakika hakuna mbunge makini na mwenye msimamo kama Zitto. kama ulivyomsoma january makamba alivyosema hayo yapo wazi. na ndio maana Zitto anasema ukweli kabisa kuwa Hoja hiyo ameitoa katika mpango wa maendeleo wa Serikali na si kama ameibuni yeye.

Hakika Zitto ni mkweli na ana kauli Thabit.

Big up Zitto.
 
Serikali hii inapiga blah blaha nyingi sana hivyo ukitaka jambo lolote litekelezwe lazima ulipigie mstari kama alivyofanya zitto
 
Hata hivyo CCM wanatumia kama kisingizio cha kuwajali wananchi, ukweli ni kwamba hawa jamaa wamefulia hawana hela za mchezo kama mwanzo maana kwa kupoteza majimbo mengi, Ruzuku wanayopata sasa haiwatoshi na kuna wafanyakazi wa CCM Makao Makuu ambao wana miezi minane 8 mpaka sasa hawajalipwa mishahara
 
Generally here Zitto is the who develop and pumped up more pressure this argument of banning sitting allowance....na siyo sirikali as Lukuvi defending kama walivyozoea siku zote kupanga bila kutekeleza kama walivyozoezwa na wananchi ...kuwa wakipanga wasipotekeleza sawa tu.....Hoja ya Zitto ipo kiutekelezaji zaidi kwani namnukuu Zitto ''Kuanzia kikao cha 8jun naomba ofisi ya bunge isitishe kunilipa posho ya vikao kwani siyo stahili halali kwasababu kuwepo kwenye vikao nisehemu ya kazi yang ambayo ninalipwa mshahara...therefore naiomba ofisi ya bunge uielekeze posho yangu mpaka pale serikali itakapoifuta''... namshangaa sana Lukivi anaposema bado serikali ipewe mda?

Let tell you..unajua ccm hawana makasa kabisa ila makosa yapo kwa wananchi ambao bado wanaipa dhamana ya kuongoza ili hali ccm haionyeshi kutaka kuongoza... it's like we're waiting a soup into an empty cooked port of beans..!

Bila ya Zitto haya yote tunge yasikia wapi..?ivi zitto ana fight kwa faida yetu at least kuwe kuna uwiano wa kikigawa kuzingatiwa uhalisia wa kitakachobaki kwa ajili ya kusukuma miradi ya maendeleo itakayonufaisha taifa kwa ujumla.

Zitto already thrown his token is up to us..!kama tunataka ifutwe kwa vitendo au kwa maelezo ya bla bla as usual..!
 
Tatizo la serikali ya Tanzania ni usanii, wana mipango lukuki utekelezaji hakuna, Mpango wa kuteketeza malaria, mpango wa kuondoa umaskini Tanzania (MKUKUTA), MKURABITA, yote ni mianya ya kuvuta hela za ufisadi mwananchi wa kawaida haoni tofauti yeyote. Zitto alichokifanya ni kuufanya mpango wa serikali kuwa utekelezaji otherwise wangelifanya kama mipango yao mengine usanii tu!!!!
 
Hivi huo mpango wa miaka 5 wa maendeleo SPIKA na hao wabunge wengine hawakuupitia? Hii inaonyesha wazi kuwa huwa hawayapitii makabrasha wanasubiri kusema NDIYO au HaPANA na kuchukua posho..
 
Acheni porojo kwa maana hiyo waziri wa fedha na spika wa bunge walipokuwa wanaipinga wanawakilisha serikali ipi?au tuna serikali ya chadema na serikali ya ccm kwenye nchi moja?hoja ya katiba mliikimbilia hivyo hivyo ikawatia aibu?kumbukumbu mmepoteza!!!!!
 
Nimekua nikifuatilia ingawa mara machache hoja ambayo wabunge wanaitumia kulipwa posho eti kwamba wanamajukumu mengi na wananchi wanawaomba hela huko majimboni. Mimi binafsi sikubaliani na hoja hii. Hivi ni kweli mbunge anaweza kutosheleza matakwa ya watu wake kwa kuwagawia hela zake? Atagawa kwa watu wangapi ili umaskini uishe? Kwa mtazamo wangu hii sababu siikubali. Hizo hela zinatakiwa zikawekezwe kwenye miradi ya maendeleo ili wananchi wote wafaidike. Sidhani kama mbunge akiombwa hela na mwananchi na kama hana akamwambia ukweli sina huyo mwananchi atamlazimisha ampe hela hasa kama kuna maendeleo yanayoonekana jimboni.
Kwa mtazamo wangu mbunge kugawa hela kwa mtu mmoja mmoja ni rushwa ya kuwafanya wananchi wamchague kipindi kijacho. Jamani ni hatari kama wabunge wanaendekeza tabia ya wananchi wao kuwa omba omba wa hela mifukoni mwa watu badala ya kuwaletea maendeleo. Hizo hela za posho zikawekezwe kwenye vikundi vya maendeleo vijijini na kuwatafutia shughuli za kufanya ili waendelee.

NAUNGA HOJA HIZI POSHO ZIKATILIWE MBALI.
 
Yupo TBC na William Lukuvi, mjadala ni kuhusu posho za watumishi wa umma.
Pia ulihusu posho ambazo WABUNGE WA CDM wanazodai hawatachukua HUKU WAMEKWISHA ZIKOPA NA KUZITUMIA HATA KABLA YA KIKAO,HALAFU MALIPO YA DENI HILO LA POSHO HUWENDA LISIISHE HADI 2015,Sasa hawa jamaa wanamfanya nani mtoto wa kuwa amini tena ikiwa WANATUDANGANYA WAMESUSA POSHO KUMBE WAMECHUKUA KITAMBO AKIWEMO FAM MWENYEWE!
 
yees! hapo muziki ndo umeanza kunoga ngoja c mashabiki tuusikilizie ila magamba kazi mnayo
 
sasa kama ni hoja ya serikali kwa nini mama Makinda na waziri wa fedha walikuwa wanapinga???
 
Na nyinyi wachangiaji wengine muwe na akili na ufahamu, we toka lini posho akakopea mtu mkopo?kwani huo ni mshahara wa mtu mpaka waruhusiwe kukopa kwa posho,wao kwa nini wawalazimishe zichukuliwe hizo posho wakati wenyewe hawataki,huoni kuna wapenda posho kuliko kazi.Watu wengine wa ajabu sana siku zote walikuwa wapi kutangaza huo mpango wao wa miaka 5 ijayo?na kama ndo mpango wao na wanawakopesha kupitia posho mbona bado waliruhusu tena wachukue hiyo mikopo.Magamba msituletee danganya toto,toeni hoja za msingi kwa Wtz
Wewe ndio unapaswa kuwa na uelewa hao jamaa wamekopa mihela mingi kiasi kwamba imeonekana mishahara yao ya miaka yote 5 haitatosha kuwa kata hayo madeni imebidi sasa wawakate kupitia posho kwa utaratibu waliosain.Hata pamoja na kukatwa kupitia posho bado watakatwa kwa miaka yote 5.wamekopa mamilion mia kadhaa ukiyajua hata hutawatofautisha na hao magamba.Nao ni MAGANDA TU HAWANA JIPYA KELELE ZA BURE!
 
Acha wivu wa kijinga wenzio wana randa mbao wewe unaranda majungu hayata kupeleka popote.vua hicho kiatu cha wivu.Kanisani penyewe wachungaji wana maposho kibao sasa bungeni wasipewe kwa kuwa wao sio watu au? Achaneni na hoja za kitoto hizo kuna mambo mengi ya kutafakari kwenye hii inchi.Mathalali kuhusu migodi ambayo haitunufaishi kwa lolote lile.jaribu kukua wenzio wakina zito wanatafuta umaarufu wala hawawatetei wananchi.
 
Mbowe, Zitto wamekwisha kopa posho zao kwa hiyo hawana cha kuchukua wanatudanganya. Mbowe hajapinga baada ya lukuvi kudhibitisha kuwa walikopa
Baada ya kauli ya lukuvi mbowe alifadhaika hata mtoto wangu wa wa miaka 9 akasema KUMBE UNAPODANGANYA SHARTI UWE NA KUMBUKUMBU ,Mh. FAM amesahau kama Posho kisha ila na ATAENDELEA KUILIPA HADI 2015, Kwa kauli ya lukuvi wamekopa ma milioni ya Shs na hata wakikatwa mishahara haitosh. HADANGANYWI MTU HAPA,WANATOFAUTI GANI NA MAFISADI WANAOWAPIGIA KELELE?WAJITIA KUSHIBA KUMBE WANA NJAA SAWA NA WENGINE TU!
 
Kwa maana nyingine posho zinawapa wabunge uwezo wa kuwahonga wapiga kura wao kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mwingine?
 
Acha wivu wa kijinga wenzio wana randa mbao wewe unaranda majungu hayata kupeleka popote.vua hicho kiatu cha wivu.Kanisani penyewe wachungaji wana maposho kibao sasa bungeni wasipewe kwa kuwa wao sio watu au? Achaneni na hoja za kitoto hizo kuna mambo mengi ya kutafakari kwenye hii inchi.Mathalali kuhusu migodi ambayo haitunufaishi kwa lolote lile.jaribu kukua wenzio wakina zito wanatafuta umaarufu wala hawawatetei wananchi.

Na wewe unaranda nini? Toa hoja sio matusi
 
acha wivu wa kijinga wenzio wana randa mbao wewe unaranda majungu hayata kupeleka popote.vua hicho kiatu cha wivu.kanisani penyewe wachungaji wana maposho kibao sasa bungeni wasipewe kwa kuwa wao sio watu au? Achaneni na hoja za kitoto hizo kuna mambo mengi ya kutafakari kwenye hii inchi.mathalali kuhusu migodi ambayo haitunufaishi kwa lolote lile.jaribu kukua wenzio wakina zito wanatafuta umaarufu wala hawawatetei wananchi.
acha ujinga wewe makanisa yameingiaje hapa unatumia makamasi kufikilia!
 
Back
Top Bottom