Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Mbowe, Zitto wamekwisha kopa posho zao kwa hiyo hawana cha kuchukua wanatudanganya. Mbowe hajapinga baada ya lukuvi kudhibitisha kuwa walikopa
 
Mbowe anasema tujikite kwenye hoja na dhana nzima ya posho vyombo vya habari vinapotosha wananchi
 
Wabunge imagine wanapata Mil 12 kwa mwezi. Hata nape nnauye hana aibu kusema Mshahara wa Dr slaa. Wabunge wenyewe wanapata mipesa si mchezo.
 
Safi sana amejibu vizuri ujinga aliouliza Zakari juu ya kuwa wameshakopa hizo posho, amemwambia kama wapo wakopeshaja kupitia posho basi wanamatatizo kwa kuwa posho hulipwa baada ya kuhudhuria vikao.[/QUOTE]

Mkuu kama posho haiwezi kukopeshwa kwa kuwa inalipwa baada ya kuhudhuria vikao inakuwaje mshahara ukopwe, mshahara nao si unalipwa baada ya kufanya kazi au?
 
deep down lukuvi anakiri posho hazifai...ila anajibaraguza tu
 
Mhe. Mbowe kakiri kiutu uzima posho wameshachukulia mikopo,
kaamisha mada, mtangazaji imebidi awe muelewa,na kuacha kuhoji suala la posho
 
uwe unasikiliza mpaka mwisho ndo unachangia sio unaongea as if unahara kama mgonjwa wa kipindupindu...kwani mtu akichukua mkopo means ya kuulipa ni posho tu?mbona una mawazo ya kishamba sana wewe!!! ndo maana mawazo yako yamefanana na mwalimu wa UPE lukuvi
 
Mbowe, Zitto wamekwisha kopa posho zao kwa hiyo hawana cha kuchukua wanatudanganya. Mbowe hajapinga baada ya lukuvi kudhibitisha kuwa walikopa

Patamu hapo wakuuu. Wanasiasa wote ni wasaka tonge tu. Kumbe hili ni changa la macho!!
 
Gabriel ZaChariah: Kugomea posho ni msimamo wa chama au mtu momja mmoja

Mbowe: Hapa tunaomba tueleweke kuwa dhana halisi ya issue hii ni ni Posho za watumishi wa umma, wabunge ni sehemu ya watumishi wa umma wapatao miatatu tu miongoni mwa watumishi wengi wa umma. Sasa magazeti yameotosha ukweli, sisi tunapinga sitting allowance ambayo dhana yake inatolewa kwa watu walioewa majukumu nje ya majukumu yao ya kawaida. Sasa watumishi wa umma wana mishahara, wanapokaa kwenye kazi zao za kawaida hawastahili kupewa posho na hii imeambukiza hadi kwenye halmashauri. Chadema tunasema posho hizi zinaharibu sana utendaji katika serikali, sasa nani kalisema kwetu sio issue bali ishu ni dhana nzima ya posho za watumishi wa umma

Gabriel Zacharia: Mheshimiwa Lukuvi,Unalisemeaje hili la Mbowe?

Lukuvi: Concept hii nzima hakuna anaeipinga. Kila mtumishi wa umma amepewa majukumu yake pamoja na malipo yake kwa mujibu wa sheria. Sasa matumizi yake ndio kitu cha kutazama. Hapa nipishane na Zitto, aliyesema posho ziangaliwe ni Mkulo. Serikali imesema wazi katika kipindi hiki itaipitia posho mbalimbali kwa watumishi wa umma ili zilete tija na kuziondoa zinazoondoa tija.ALICHOKOSEA ZITTO ni kulifanya jambo hili kama amelivumbua yeye.

Gabriel Zacharia: Mheshimiwa Mbowe unazungumziaje maelezo ya waziri?

Mbowe: Kulipersonalize kwa kumtaja Zitto ni kumuonea. Nimkumbushe waziri kuwa Viongozi wa serikali walilipinga hili mwanzoni. Suala hili wether kalisema Zitto au Serikalini kwa sasa halina maana kulipersonalise ila tujadili dhana halisi ya suala hili

Gabriel Zacharia: Zipo taarifa za uhakika kuwa Mheshimiwa Mbowe na wenzako wa Chadema mmeshakopa pesa hizi

Mbowe: Si kweli, kwanza mkopo ni haki ya mkopaji na ni makubaliano kati ya mkopajio na mkoeshaji. Posho za bunge ni sitting allowance na hutolewa unapokuwa kwenye kikao. Sasa kama sitakuja Dodoma sitapata hiyo posho sasa watanikopeshaje osho wakati sijahudhuria kikao? Kama ni kukopa unakopa kwenye mshahara wako na sio kwenye osho na kama mtu kakopeshwa kupitia osho basi tatizo lipo kwa mkopeshaji

Gabriel Zacharia:Mheshimiwa waziri unalisemeaje hili

Lukuvi:Concept nzima sio posho bali kupunguza gharama za serikali ndiomaana sasa hivi magari aina ya vx hayanunuliwi tena yananunuliwa GX.
Kuhusu kukopeshwa posho ni kweli walikopa na Mbowe alikopa ppia. Walikopa milioni mia mbili, mia hamsini , mia tisina saba kwa hiyo mh. Zitto na wengine wamekopa.

Gabriel Zacharia:Mbowe wakati mnakataa osho miongoni mwa wabunge wa Chadema wanapokea osho kwenye kamati?

Mbowe: sisi tunazungumzia kupunguza ghara za serikali lakini kujadili mbunga fulani kapokea posho au fulani hapokei ni ishu ndogo sisi tunataka wote kwa pamoja tujadili ishu ya msingi, tusipoteze muda kujadili jambo lisilo na tija

Gabriel Zakaria: kwanini msiige alichokifanya waziri mkuu kwa kukataa VX akapokea GX ingawa Mbowe yeye anaendesha VX?
Lukuvi: Tupe muda tumedhamiria kupunguza gharama ndani ya miaka mitano tutakuwa tumepunguza gharama za serikali

Tanesco washachukua chao
 
kabisa yaaani huyu kasikiliza kidogo bila hata kuelewa content ya mjadala mzima,anakuja na upupu wa hatari apeleke facebook huo ujinga,sio hapa jamvini
 
Kazi ziko wapi wakati mmegawiana wenyewe Mafisadi?!! ndio tunataka kulianzisha mbelle kwa mbele mpk kieleweke..na hizo kazi tugawane na sisi tufurahie keki ya taifa..
Mbona hukwenda kuchota mchanga wa dhahabu au wewe pia ulikuwepo?
 
Wanatafuta umaarufu tu hawana lolote si chochote hao! Mboe,zitto kila siku wanagombania madaraka ndani ya chadema wiz mtupuuuuu!!


Umaarufu ndiyo siasa, haujui?
Kwa sasa wananchi wa kipato cha chini ambao ndiyo wengi wanataka matumizi na anasa zipunguzwe mojawapo ikiwa ni hii. We unamlipa mtu laki na nusu kwa siku wakati waajiriwa wengi hawapati mshahara huo kwa mwezi, achilia mbali wale ambao ni wengiii hawana ajira. Hizi posho zitoke tu na zitawafanya wengi waganga njaa kujifikiria mara mbili kabla ya kuchukua fomu za kugombea ubunge.
Mtaji wa kisiasa huo.
 
live TBC,
CDM wanang'ang'ania posho zipunguzwe kumbe mpaka Mhe.Mbowe na Mhe.Zito wamezikopa teyari , Mhe.Lukuvi kamuaibisha Mbowe live.
Mhe. kaamisha mada kawa mpole kama kamwagiwa maji.
hivyo hata ikisemekana wakatae posho watakataa nini na zote wamechukulia mikopo


acha kukurupuka........unaandika wakati mbowe hajajibu....sasa umesikia alivyojibu mbowe?!!!
 
uwe unasikiliza mpaka mwisho ndo unachangia sio unaongea as if unahara kama mgonjwa wa kipindupindu...kwani mtu akichukua mkopo means ya kuulipa ni posho tu?mbona una mawazo ya kishamba sana wewe!!! ndo maana mawazo yako yamefanana na mwalimu wa UPE lukuvi

Kigogo, vijana wa NAPE kazini - hapo peusi pamenifurahisha, inaonekana alipiga kitimoto kimechacha jana - ha ha ha
 
Safi sana amejibu vizuri ujinga aliouliza Zakari juu ya kuwa wameshakopa hizo posho, amemwambia kama wapo wakopeshaja kupitia posho basi wanamatatizo kwa kuwa posho hulipwa baada ya kuhudhuria vikao.[/QUOTE]

Mkuu kama posho haiwezi kukopeshwa kwa kuwa inalipwa baada ya kuhudhuria vikao inakuwaje mshahara ukopwe, mshahara nao si unalipwa baada ya kufanya kazi au?

Mshahara ni wa mkataba ambao hata ukiumwa mwezi mzima utalipwa tuu hata kama utakuwa hujafanya kazi, lakini posho kama hujahudhulia vikao huwezi kupewa. Mtoaji/mdhamini wa mkopo anakuwa na uhakika gani kwamba huyo mkopaji atahudhulia vikao vyote mpaka apewe mkopo wa posho kabla ya vikao?
Hapa nakuwa na wasiwasi na bunge letu.
 
Napendekeza siku ya maandamano ya Posho, picha ya huyu mbunge aliyepiga mboji iwekwe kwenye bango kubwa na swali liulize je ni halali kumlipa posho kwa wabunge wa magamba kama huyu!

Naunga mkono hoja!
 
Lukuvi kanishangaza jambo moja, eti Zitto amepora hoja ambayo walikwisha iandaa, mbona wavaa magamba wenzake wanakataa posho kuondolewa. ila kama itakua hivyo mi nafurahia jambo jingine.Viongozi wa wilaya watakuwa wanapatikana ofisini mana cku hizi kila cku ni vikao kumbe posho!!! Kweli ufidadi tz umekinai
 
Back
Top Bottom