Ndugu zangu wanakagera nyie ni watu wastaarabu mno, pamoja kwamba mmepatwa na majanga ya tetemeko la ardhi na serikali ikashindwa kuwasaidia bado mmeonesha kiwango cha juu kabisa cha kustaraabika nyie sio wa nchi hii kwa ustaarabu mlionesha kwa Mheshimiwa rais.
Pamoja na Mheshimiwa rais kuwasimanga baadala ya kuwapa pole lakini mliendelea kuwa wapole na kumsikiliza hadi mwisho, maneno aliyokuwa anayatamka Mhe rais hayana staha na sio maneno ambayo wafiwa wanapaswa kuwaambiwa, ikumbukwe kwamba hakuna mhanga aliyetaka kujengewa nyumba kama alivyosema Mhe watu walitaka pesa za rambirambi zitumike kuwasaidia wahanga na serikali ijenge miundombinu kwa pesa zake.
Mhe rais anasema nyie ni watu majanga tu, tetemeko, ukimwi, ugonjwa wa mnyauko bila kujua kwamba majanga haya ni asili hayakwepeki hii ni dhihaka kubwa sana kwenu pamoja na dhihaka hizo zote mlienda kumvumilia hata kumshangilia kinafiki.
Nina uhakika Mhe rais angeatamka haya kwa jamii ya watu wengine angepopolewa na mawe na uwanja ungegeuka wa damu, peleka dhihaka kama hizo Tarime uone utakachoambulia, endeleeni na ustaarabu huo Mwenyezi Mungu atawalipia.