Pongezi na hongera sana Wanakagera, nyie ni watu wastaarabu mno

Hivi Kigamboni alipata kura ngapi? Tafakari.....pooooooooh! Haki Elimu.
 
Hahahaha.... Hili haliwezi kuwatoa kisiasa wapinzani. Limeshapita.

Mbunge wao kasema anamuunga mkono Magu
Watu ni wanamsifia kinafiki tu.yaliyoko ndani ya mioyo yao wanayajuwa wenyewe. Yeye si Mungu umzomee si atakumaliza hapo hapo.
 
Tatizo lasiku izi kila mtu anajua ila anasahau unaweza sema mengi ya muhimu ila yatakayo sambazo niyale hasi tu ivi nani anatembelea akili zetu wakizazi ichiii? Nakuwa na simanzi kila mara ninaposoma maandiko mbalimbali. Siku si zetu bali kumbuka upandalo ndo uvunalooo
Unafiki utatumaliza watanzania. Hata kama unampenda sana Magufuli lakini jaribu kuwaza kwa kina kidogo kuhusu kauli za dharau anazotoa Mfalme kwa watu wake waliopatwa na majanga. Hapa ni ubinadamu tu wala haihitaji uwe professor kulitambua hili.
 
Nimempenda yule mzee aliesema."hata ukinipa bati moja poa tu" na bwana mkubwa akamwambia "nitakupa mabati salasini" I hope alimaanisha thalathini....
Inasikitisha sana pale mwanachi anapopiga magoti kumuomba rais bati moja as if ni anaomba uhai kwa Mungu.
 
Magufuli angependeka sana kama angekuwa na huruma ya kweli. Ile hotuba siyo ya kuhamasisha wafiwa. Anawezaje kupenda kujenga vitu kuliko kusaidia watu binafsi kwanza? Watu na familia zikijengeka ndiyo unapata Taifa la kujenga shule na hospitali na vingine.
Mjane anayetafuta hela ya kujenga nyumba atalima saa ngapi?
Poleni wana Kagera.
Huyu jamaa ni mnafiki na ana roho mbaya kuliko wote waliopita.
 
Inaonyesha watu wengine hawapendi kusikia ukweli. Kunasehemu nyingu Tanzania maafa yalitokea lakini wananchi hawakujengewa nyumba kwanini wananchi wa bukoba pekee ndio wajengewe kwani wao nitofauti na watanzania wengine? Au ndugu mwandishi umetumwa?
Hatukatai kusema ukweli lakini ukweli huu uendane na mazingira ya unaowaambia ukweli.
Amini nakwambia 2020 jamaa atapata tabu sana kagera.
 
Ndugu zangu wanakagera nyie ni watu wastaarabu mno, pamoja kwamba mmepatwa na majanga ya tetemeko la ardhi na serikali ikashindwa kuwasaidia bado mmeonesha kiwango cha juu kabisa cha kustaraabika nyie sio wa nchi hii kwa ustaarabu mlionesha kwa Mheshimiwa rais.

Pamoja na Mheshimiwa rais kuwasimanga baadala ya kuwapa pole lakini mliendelea kuwa wapole na kumsikiliza hadi mwisho, maneno aliyokuwa anayatamka Mhe rais hayana staha na sio maneno ambayo wafiwa wanapaswa kuwaambiwa, ikumbukwe kwamba hakuna mhanga aliyetaka kujengewa nyumba kama alivyosema Mhe watu walitaka pesa za rambirambi zitumike kuwasaidia wahanga na serikali ijenge miundombinu kwa pesa zake.

Mhe rais anasema nyie ni watu majanga tu, tetemeko, ukimwi, ugonjwa wa mnyauko bila kujua kwamba majanga haya ni asili hayakwepeki hii ni dhihaka kubwa sana kwenu pamoja na dhihaka hizo zote mlienda kumvumilia hata kumshangilia kinafiki.

Nina uhakika Mhe rais angeatamka haya kwa jamii ya watu wengine angepopolewa na mawe na uwanja ungegeuka wa damu, peleka dhihaka kama hizo Tarime uone utakachoambulia, endeleeni na ustaarabu huo Mwenyezi Mungu atawalipia.
mto Ngono na kijiji cha Katerero vina uhusiano gani na tetemeko la Kagera?
 
Tunataka chanel zile za bure zirudishwe la sivyo waturudishie analogia yetu maana antena bado tunazo. Hii ni laana na unyonyaji mkubwa kwa kutaka kuwakamua maskini wa nchi hii kila walichonacho.
 
Hahaaa kaka kweli unawajua waTz, atakayepingana na kauli yako huyo si mtanzania. Akili zetu tunazijua wenyewe..
 
Wakati pale anaongea kuhusu haya majanga yaliyotokea yote Kagera. Ilitakiwa watu waangue kilio nadhani watu ndio wangejua kwamba watu tumepatwa na majanga na sio utani
 
2020 atapata kura nyingi kutoka huko,sina shaka juu ya hili.na atakayebisha ni yule asiyewajua watanzania
Wengi ni wepesi kusahau, lakini ukweli ni huo,
2020 kura zitakuwa nyingi kuliko 2015.
 
Ahsante sana Mkuu kwa hekima na busara zako nyingi kwenye hili bandiko lako. Baadhi ya Watanzania wasiojitambua wanataka kupigia makofi kauli za kustaajabisha katika hafla ya kuwafariji wahanga. Inashangaza sana kusema kweli. Kama Watanzania tusipojithamini wenyewe basi hata majirani zetu wakitudharau tusipige kelele maana kiongozi wa nchi yeye hakuona shida kutumia lugha ya kustaajabisha katika hafla ya kuwafariji wana Kagera na eti anawashangaa! Ukimwi wao tetemeko wao! Maafa hayana mmoja leo yametokea Kagera kesho yatakuwa sehemu nyingine nchini.
Aisee.......tetemeko wao, ukimwi wao, .... alisahau VITA vya Amin wao... Hii haikuwa poa.
 
Inaonyesha watu wengine hawapendi kusikia ukweli. Kunasehemu nyingu Tanzania maafa yalitokea lakini wananchi hawakujengewa nyumba kwanini wananchi wa bukoba pekee ndio wajengewe kwani wao nitofauti na watanzania wengine? Au ndugu mwandishi umetumwa?
Sawa yawezekana ametumwa, je, zilepesa tulizo changishwa kwa dhumuni la kuwasaidia wahanga watetemeko hapo napo vipi?
 
IMG-20170104-WA0001.jpg
 

Attachments

  • AUD-20170104-WA0002.mp3
    1.2 MB · Views: 18
Sawa yawezekana ametumwa, je, zilepesa tulizo changishwa kwa dhumuni la kuwasaidia wahanga watetemeko hapo napo vipi?
Zile pesa azikufika kwa walengwa,
Mfano likitokea janga lingine sehemu nyingine sidhani kama watu watachangia kwa mtindo huu
 
2020 atapata kura nyingi kutoka huko,sina shaka juu ya hili.na atakayebisha ni yule asiyewajua watanzania

Huu ndio ukweli, ataebisha ni kweli hawajui watanzania.
Ni moja ya Taifa lenye watu wa ajabu sana, kwa mataifa ya watu wanaojitambua kwenye huo mkutano ama angekuwa peke yake na Viongozi wenzie au wangekuja wananchi wachache sana.
Lakini sisi duh!!...
 
Back
Top Bottom