Pombe zinachafua sherehe hasa za Harusi!

Pombe zinachafua sherehe hasa za Harusi!

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,427
Reaction score
10,749
Kuna harusi nilihudhulia ya kurwa na doto waliamua kufunga ndoa na wapenzi wao waislamu swaafi. Sasa pale ukumbini ilisomwa sala kabisaa na shehe kupiga marufuku na kulaani unywaji wowote wa kilevi ktk harusi, cha ajabu baada ya dua, watu wakaingia na mabia yao toka nje! Acha watu wagambike sasa! Full mavurugu.
Utakuta mtu ni muislam au mkristu halafu harusi au sherehe inajaa pombe. Mbaya zaid watu wanafunga ndoa Jumamos au Ijumaa, au Alhamis then kesho yake ni siku ya ibada/misa! Je, wadau watahudhuria ibada kweli? Kwa kweli nawapongeza makanisa wanaozuia mipombe ktk harusi, maana inachafua sherehe. Pia ndg zangu waswaha hongereni kwa sheria ya kupinga ulevi hasa ktk sherehe!
Ndoa ni tendo takatifu, sio vizuri kuichanganya na ulevi ambapo shetani atajihudhurisha.
Zipo dhambi nyingi, ila leo nimeiongea hii maana sherehe zinaharibiwa zaidi na ulevi.
Wasalaam!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
aisee...
946969_525160644188301_441365542_n.jpg
 
Huyu sio siri kitu kishapanda kichwani! Istoshe ndo Bwana harusi sasa!
Hizi pombe hizi, hazileti furaha ktk harusi ila kupoteza mwelekeo wa sherehe.


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Tyta wewe ni balaa Excel (biashara yako ya kuuza mahindi mabichi na mvua hii sidhani kama inaenda) umeona hii na Tized (kwanza habari yako mafuriko yamekuachia suruali ya kazini) na utafiti (sijui kibanda chake cha simu kimepona na mafuriko haya na Mndengereko (ule mchanga uliokusanya kuuza nina uhakika mafuriko yameurudisha mtoni
 
Last edited by a moderator:
kuzuia pombe ni jambo ambalo halizuiliki watu wamechanga pesa zao kusudi wakagambeke
 
Maandiko matakatifu yanasema mpe masikini kilevi asahau shida zake.
 
Kwa sisi wengine harusi ni kanisani ukumbini kushereheka. Hatufungi ndoa ukumbini.
 
Tyta wewe ni balaa Excel (biashara yako ya kuuza mahindi mabichi na mvua hii sidhani kama inaenda) umeona hii na Tized (kwanza habari yako mafuriko yamekuachia suruali ya kazini) na utafiti (sijui kibanda chake cha simu kimepona na mafuriko haya na Mndengereko (ule mchanga uliokusanya kuuza nina uhakika mafuriko yameurudisha mtoni
Mr Rocky mimi mvua naionaga tu kwenye tv, huku kwetu ikipita tu unaenda na safari zako. Muulize Excel kama kule juu ya mti kashashuka au bado?
 
Last edited by a moderator:
Suala la sherehe kutumika pombe baada ya kufunga ndoa huwa haliepukiki maana pale waalikwa ni watu wa namna tofauti kitu ambacho ni kigumu kuzuia matumizi ya pombe,kama unafanya sherehe na hujamchangisha mtu na ukatoa kadi tu kwa masharti ya kutotumika pombe inawezekana lakini si vinginevyo.
 
Ukweli ni kwamba tumezidi kuendekeza ulevi kiasi kwamba baadhi ya sherehe hugeuka karaha!
 
ila harusi bila kilahuri aisee inaboa kidogo watu wasiwe na akili zao ndo mambo yananoga loh
 
Back
Top Bottom