Sunday Talk: Kwanini Misa na sherehe za harusi zisifanyike mapema?

Sunday Talk: Kwanini Misa na sherehe za harusi zisifanyike mapema?

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,161
Reaction score
35,716
Wanabodi,

Nimetafakari hapa kwanini tumeendelea na utaratibu wa misa za harusi kuwa jioni na sherehe kufanyika usiku?

Kwanini ibada ya ndoa isifanyike asubuhi ili baada ya misa watu waende ukumbini kupata chakula cha mchana na shughuli zingine za kusherekea ziendelee na kukamilika mapema?

Nchi za wenzetu wanafanyaje? Hizi shughuli zikifanyika mapema na kumalizika mapema inatoa fursa nzuri ya ushiriki kikamilifu kwa watoto na pia kuepusha mambo mengi ya usiku.

Hivi hili la misa za ndoa kuwa jioni na sherehe usiku hatuwezi kubadilisha? Kwanini? Nafikiri mabaraza yetu ya maaskofu wanaweza kuangalia hili.
 
Back
Top Bottom