Kwani bila pombe sherehe haikamiliki?

hannibali

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
468
427
Habari za muda huu!

Juzi nimehudhuria harusi kuna watu waliamua kufunga ndoa na ilikuwa ndoa ya Kiislam.

Sasa pale ukumbini ilipigwa sala kabisa na mashekhe walipiga visomo kadhaa, mashekhe muda wote walikuwa wanapiga marufuku na kulaani unywaji wowote wa kilevi, cha ajabu baada ya dua, watu wakaingia na mapombe yao toka nje! Acha watu wagambike sasa! Mavurugu kama yote.

Sasa nilijiuliza hotuba yote ile ya mashekhe wale lakini watu walishindwa kuacha lipite wakagambika kisawasawa, matokeo yake wale mashekhe waliondoka bila kuaga na kupelekea lawama mzito kwa wahusika.

Jamani eeeh ndoa ni tendo takatifu, sio vizuri kuichanganya na ulevi ambapo shetani ndio leader hasahasa mkiwa mmekatazwa matokeo yake munaharibu ndoa za watu.
 
Ni kweli uliyoandika!

Ni kweli ili sherehe ifane hasa harusi ni lazima watu washiriki, wale, Wanywe na kucheza.

Lakini kwenye kunywa siyo lazima iwe pombe, kunywa wanaweza kunywa juisi, togwa, maji n.k
 
Umeona? Yaani ni kama tu traffic light chato!! Haina maana bila pombe!! Nimekumbuka songi flani la longi "wameiba pombeeee! Tutafanyaje hii sherehe"
 
Wakatoliki mna shida sana.

Sisi walokole sherehe zetu zinanoga sana bila hata hayo mapombe pombe yenu.
 
Ni kweli uliyoandika!

Ni kweli ili sherehe ifane hasa harusi ni lazima watu washiriki, wale, Wanywe na kucheza.

Lakini kwenye kunywa siyo lazima iwe pombe, kunywa wanaweza kunywa juisi, togwa, maji n.k
Watu wanywe juice tu inatosha.
 
Hannibali, Hannibal, Hannibal! Mara ngapi hizo nimekuita?

Sikiliza....

Mambo yasiyokupunguzia siku zako za kuishi yanini kuyaangaikia?

Mambo ya wanywa pombe tuachie wenyewe wanywapombe, pilipili usiyoila yakuwashia nini?

Hizi mada za kupinga na kupiga vita unywaji wa pombe zimekuwa nyingi Sana humu siku hizi.

Ebu tuacheni sisi tulewe,, ebooo!

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Sherehe ili ifane lazima watu wale , wanywe na kucheza na kusaza!

Lakini kunywa siyo pombe!

Kwa hiyo mtu akisifia sherehe mimi huwa napima katika maeneo 3

Kula
Kunywa lakini siyo pombe
Kucheza

Kusaza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom