Zifuatazo ni athari za kumchafua mtu wa ndani kwa matendo ya mtu wa nje

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
21,625
33,691
Salaam,Shalom!!

Twende Kwa kifupi zaidi,

Mtu wa ndani ni nani?

Mtu ni ROHO, anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Mtu wa nje ni nani?

Mtu wa nje ni mwili uliotokana na udongo,

Mtu wa ndani ana viungo vya mwili vyote kamili, hata kilema wa Kuzaliwa au kipofu wa mwili, katika yule mtu wa ndani, ana viungo vyote kamili, ndiyo maana Yesu alisema Mungu haangalii kama watazamavyo WANADAMU.

Mtu wa ndani ana viungo vyote, anapoingia ndani ya MWILI na kuwa NAFSI hai, anazaliwa akiwa sawia 100%

MADHARA YA KUMCHAFUA MTU WA NDANI KWA MATENDO YA MTU WA NJE.

1. Mama mjamzito unapotumia kilevi Ukiwa mjamzito, unaingiza ULEVI ndani ya mtoto ndani ya tumbo, madhara yake, unamlazimisha mtu wa ndani aliyevaa mwili naye awe mlevi, azoee pombe, matokeo yake ni kumchafua na kumtoa katika kusudi mtoto huyo na mission aliyoletwa nayo duniani.

2. Mtu wa ndani Huwa hajatobolewa pua au sikio kitendo Cha kumtoga mwanao pia au sikio, unamlazimisha mtu wa ndani pia awe na matundu puani na sikioni Kwa kukaribisha Roho za kuzimu zenye kuhusika na kutoga pia na masikio, matokeo ni ukahaba Kwa mtoto mbeleni na uchawi na kutofanikiwa, unamtoa mwanao Toka baraka za Mungu. Usipotubu, utakataliwa geti la Mbinguni Kwa kulichafua hekalu la Mungu ( mwili) jitakase 🙏

3. Baba unapenda kutafuta msaada Kwa mganga wa kichawi mpiga ramli, jua unaenda huko Ukiwa na wanao viunoni ambao hawajazaliwa Bado, na uliokwisha wazaa, usilolijua, Kwa kwenda huko, unawakabidhi wanao Kwa Roho za kuzimu zifuatwe kizazi chako, ukizaa mtoto wako wa kwanza usishangae akikataa NDOA na kukimbilia kuanza uzinzi kabla ya wakati tena na watu wasioamini, chanzo ni wewe Kwakuwa umemchafua mtu wa ndani ( mtoto) aliyekuwa viunoni mwako ulipomkabidhi Kwa Kutoa sadaka Kwa mganga wa kichawi Ili akusaidie ktk jambo lolote.

3. Kijana unaposuka Rasta au kuvaa wigi, unamchafua mtu wa ndani kumletea hasira na magomvi, Rasta na wigs ni nyoka hizo katika Ulimwengu wa Roho, imagine unavaa kofia kichwani iliyojaa nyoka, saangapi uwe na utulivu wa Roho NAFSI na MWILI? Usichafue mwili wako, utafunga baraka zako. Hakuna Malaika Mbinguni mavazi wigi, msuka Rasta Wala mnyoa denge!

4. Binti unapofuga kucha ndefu, uwe na uhakika kuwa unamchafua mtu wa ndani, kucha ndefu ni za mapepo yaliyolaaniwa na misukule, sasa kufuga kucha ndefu au kuweka bandia, ni kusema kuwa katika Roho kuwa unapenda kuwa msukule, utamchafua mtu wa ndani Kwa kuwa utakatibisha Roho za kuzimu ziingie kushindana na mtu wa ndani aliye Roho akaaye ndani ya MWILI wako aliye wewe halisi. Usishangae Roho za uzinzi kukuingia au za mauti Ili uwe msukule halisi.

5. Usiposoma BIBLIA, uwe na HAKIKA kuwa unamkondesha mtu wa ndani wakati ukimnenepesha mtu wa nje Kwa kula Kila siku na saa, mtu wa ndani, aliye Roho chakula chake ni neno la Mungu a Ibada na maombi na kufunga.

7. Mtu wa nje ukivaa nguo za kubana au nusu uchi, unakaribisha majini yenye kuhusika na ukahaba yake ndani Yako kumchafua mtu wa NDANI na kumdhoofisha afuate uamuzi uliouchukua wa kuchafua mtu wa nje.

8. Mwanamke unapovaa suruali na mavazi ya kiume unakaribisha usiheshimiwe na JAMII, unakaribisha mapepo ya kuzimu Ili kukaa ndani Yako Ili kumchafua mtu wa ndani na kumbadilishia asili yake, matokea TABIA za kudharau wewe kuwa mwanamke na kutamani kuwa Mwanaume kutainuka, ghafula utaanza kuona mumeo ni sawa nawe, na utaanza kuwaona wanawake wavaa sketi na gauni wako chini Yako, usagaji na USHOGA utaingia pole pole. Mwisho wa siku utakataliwa kuingia Mbinguni sababu wasio WATAKATIFU wanajisio miili Yao, hawaingii Mbinguni.

ONYO: Takasa mwili wako Kwa kuwa Hilo ni hekalu la Mungu, anatakiwa akae humo Ili kumwabudu Mungu katika Kila ufanyacho maishani.

Wengi wanakataliwa katika geti la Mbinguni Kwa kuchafua miili Yao Kwa mapambo na uchafu katika miili( mtu wa nje) unaochafua hekalu la Mungu ( mwili) na kumtia najisi mtu wa ndani ( Roho).

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako na ungependa kusafisha mwili wako uendane na mtu wa ndani ( Roho), fuatisha Sala hii;

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMEN

Karibuni 🙏
 
Back
Top Bottom