Pombe ni dhambi, acha kuitumia

ngono sio dhambi ila ikitumika nje ya maan ni dhambi sio?
How about pombe?
Vipi mtu akitumia na asitende hayo uliyosema ?
 
Ukiona mtu akinywa Pombe anasababisha matatizo ujue huyo muhusika tayari alikuwa ni tatizo kabla hata hajanywa.

Utasikia oohh!! ukinywa pombe unatukana ama unapigana, mbona hatujawahi kuona bia zinapigana ama zinatukana zikiwa kwenye jokofu?

Kama pombe ingekuwa tatizo ama dhambi Yesu asingegeuza maji kuwa divai kwenye harusi ya Kana (Yohane 2: 1-25). Angewaambia wageni wanywe maji tu na chakula wasepe na sio kuwageuzia maji kuwa divai ili waburudike.

Ama unataka kutuambia wewe unajua sana kuliko Yesu?
 
Mbona Yesu alikunywa pombe kwahiyo alitenda dhambi?
 
Mkuu wewe endelea na juisi yako ya mapapai, kwani Shida iko wapi?
Hujui umuhimu wa Gambe wewe. Hayo madhara yote ya Game uliyo orodhesha ni dhaifu sana ukilinganisha na Faida ya Gambe.
Gambe iheshimiwe mkuu
 
Pombe ina faida zake nyingi sana kisayansi na kitiba, inategemea tu unaitumia wapi na kwa kiwango gani.
 
Imeandikwa
"Kunywa Kistaarabu"

Pombe sio ya Kila mtu.
 
SAwa vipi kuhusu bangi nayo ni dhambi,leta kifungu.
 
Sio sahihi kusema hivyo. Ukweli ni kwamba kitu chochote kile kikitumika vibaya ni dhambi. Tumia pombe kiasi na usilewe. Ulevi ni dhambi, ulafi ni dhambi, ukifanya sana tendo la ndoa na mkeo kiasi cha kupitiliza ni dhambi kama ulevi na ulafi.
 
Unatukosea mkuu
Ww ndouache dhambi
Pombe sio dhambi
"Mpe mvinyo masikini asahau tabu zake"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…