Polisi yatoa sababu "nzito" kuzuia Mahafali ya CHASO Dodoma

Baada ya ukimya mwingi hatimae polisi mkoani Dodoma wametoa sababu "nzito" za kuzuia mahafali ya CHASO-CHADEMA mjini Dodoma.

Polisi wanasema hivi karibuni Dodoma walifariki watu nane kwa kilichodaiwa kula ugali wenye sumu,hivyo walihofia tukio kama hilo kutokea kwenye mahafali ya CHADEMA.

Hongereni Polisi kuokoa maisha ya wana CHADEMA....Haah haah.Tunawasubiri Polisi Moshi wajibu mashambulizi ya wenzao wa Dodoma
hizi sababu kama ingekuwa zinatolewa kwenye usaili wa kazi kamwe huwezi kuajiriwa
 
Baada ya ukimya mwingi hatimae polisi mkoani Dodoma wametoa sababu "nzito" za kuzuia mahafali ya CHASO-CHADEMA mjini Dodoma.

Polisi wanasema hivi karibuni Dodoma walifariki watu nane kwa kilichodaiwa kula ugali wenye sumu,hivyo walihofia tukio kama hilo kutokea kwenye mahafali ya CHADEMA.

Hongereni Polisi kuokoa maisha ya wana CHADEMA....Haah haah.Tunawasubiri Polisi Moshi wajibu mashambulizi ya wenzao wa Dodoma

hahahaha! harafu Siku hiyohiyo kulikuwa na kongamano kubwa la Restless development ndani ya chuo kikuu cha Dodoma lilihusisha wanafunzi wa vyuo, secondary na shule za misingi ambao walitokea maeneo mbalimbali ya mkoa na nje ya mkoa. lilifanyika na kumalizika bila polisi kulisambaratisha
 
Naona polisi wameanzisha campaign clouds TV ya kulazimisha watu wawapende hapa wamechemsha kabisa
 
Utakamatwa wewe, hawawezi kutoa sababu ya kijinga namna hiyo
 
Wangeifunga Udom kwa kuwa kuna vi hoteli pale,pia mama ntilie,migahawa,mishikaki wafungiwe.

Halafu walijuaje kwamba ukawa wangekula ugali?

Yaani graduation kabisa Mkuu wa polisi anawaza watu wangekula ugali?
 
Munaohoji uwepo wa bunge dodoma wakati huu wa ugonjwa usiojulikana nani kawaambia hao wabunge wanakula kwenye bufee?

Wabunge hawali kwenye bufee.....wale wananchi 8 waliokufa ndo wanakulaga kwenye bufee.
 
Ugonjwa uliozuia wajulikana mahafali ya Chadema
Serikali imesema uchunguzi wa awali wa vifo vya watu wanane mkoani Dodoma
umeonyesha kuwa vilitokana na familia kula ugali wa unga wa mahindi wenye sumu kuvu
B (aflatoxins B).

DALILI ZA UGONJWA

Dalili za ugonjwa huo ni kutapika, kuharisha, kupata rangi ya manjano, machoni na sehemu nyingine za mwili, maumivu ya tumbo, kuvimba tumbo kwa kujaa maji ndani kwa muda mfupi.

Sharon Sauwa, Mwananchi ; ssauwa@mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema uchunguzi wa awali wa vifo vya watu wanane mkoani Dodoma
umeonyesha kuwa vilitokana na familia kula ugali wa unga wa mahindi wenye sumu kuvu B (aflatoxins B).

Jeshi la Polisi lilizuia mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Dodoma ambao ni
wafuasi wa Chadema yaliyokuwa yafanyike kwenye hoteli ya African Dream, likisema
mikusanyiko yote imezuiwa baada ya kuzuka ugonjwa usiojulikana ambao awali uliua watu sita.

Wakati Jeshi la Polisi likizuia mahafali hayo ya Chadema, taasisi nyingine zilikuwa zikiendelea na mikutano kwenye hoteli hiyo, jambo lililowafanya viongozi wa Chadema kulalamikia hafla yao kusambaratishwa na polisi waliokuwa na silaha za moto na gari la maji ya washawasha.

Mbali na kuongezeka kwa idadi ya waliofariki dunia, watu waliougua ugonjwa huo
wameongezeka kutoka 21 hadi 28.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Khamis Kigwangalla alisema pamoja na matokeo hayo ya awali,
watalaamu wengine wa afya walienda wilaya za Chemba na Kondoa kuchukua sampuli nyingine.

Alisema wataalamu hao wanatoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Alisema sumu kuvu inatokana na fangasi wanaokuwa katika mazao ya nafaka au mahali ambapo mazao hayo yamehifadhiwa.

Hata hivyo, alisema athari za sumu kuvu hizo ni za muda mrefu na inamuweka mtu katika hatari ya kupata saratani ya ini.

Dk Kigwangalah alisema uchunguzi huo umethibitisha kuwa ugonjwa huo si Homa ya Bonde la Ufa wala manjano, ingawa baadhi ya dalili zinafanana.

Jumapili iliyopita Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alisema wamechukua hatua mbalimbali
ikiwamo kuchukua sampuli za maabara kwa ajili ya utambuzi wa ugonjwa na damu, mkojo, kinyesi, matapishi na vinyama vinavyotokana na ini vimechukuliwa. “Sampuli zote zimepelekwa Maabara ya Taifa, Mkemia Mkuu wa Serikali na Maabara ya Kilimanjaro Christian Research Institute (KCRI) iliyopo Kilimanjaro kwa uchunguzi zaidi,” alisema.​


vs


 
Back
Top Bottom