Polisi yatoa sababu "nzito" kuzuia Mahafali ya CHASO Dodoma

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,007
114,354
Taarifa hii ipo front page ya Gazeti la Mwanachi na imeripotiwa zaidi kurusa ya 3 kushoto

Jeshi la polisi lilizuia mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Dodoma ambao ni wafuasi wa Chadema yasifanyike kwenye hoteli ya African Dream, likisema mikusanyiko yote imezuiwa baada ya kuzuka kwa ugonjwa usiojulikana ambao umeua watu sita.

Wakati jeshi la Polisi likizuia mahafali hayo ya Chadema, taasisi nyingine zilikuwa zikiendelea na mikutano kwenye hoteli hiyo.

Mbali na kuongezeka kwa idadi ya waliofariki dunia, watu waliougua ugonjwa huo wameongezeka kutoka 21 hadi 28.
 
Baada ya ukimya mwingi hatimae polisi mkoani Dodoma wametoa sababu "nzito" za kuzuia Mahafali ya CHASO-CHADEMA mjini Dodoma.Polisi wanasema hivi karibuni Dodoma walifariki watu nane kwa kilichodaiwa kula ugali wenye sumu,hivyo walihofia tukio kama hilo kutokea kwenye mahafali ya Chadema......Hongereni Polisi kuokoa maisha ya wana CHADEMA....Haah haah.Tunawasubiri Polisi Moshi wajibu mashambulizi ya wenzao wa Dodoma

Siyo intelijensia ya Polisi tena.Ok na wale wa Mwanza nao ilikuwa sababu ni nini??Naona baada ya IGP kuwatwanga ma RPC majibu yanayokuja hata mtoto mdogo anajua tu na ukada wa chama kwa kupitiliza
 
Munaohoji uwepo wa bunge dodoma wakati huu wa ugonjwa usiojulikana nani kawaambia hao wabunge wanakula kwenye bufee?
 
Baada ya ukimya mwingi hatimae polisi mkoani Dodoma wametoa sababu "nzito" za kuzuia Mahafali ya CHASO-CHADEMA mjini Dodoma.Polisi wanasema hivi karibuni Dodoma walifariki watu nane kwa kilichodaiwa kula ugali wenye sumu,hivyo walihofia tukio kama hilo kutokea kwenye mahafali ya Chadema......Hongereni Polisi kuokoa maisha ya wana CHADEMA....Haah haah.Tunawasubiri Polisi Moshi wajibu mashambulizi ya wenzao wa Dodoma

I love and enjoy politics.....
 
Sababu za kuzuia mahafari ya moshi ni nini? Au ni ugali wenye sumu pia? Waache kutudanganya
 
Back
Top Bottom