Tundu Lissu atalihutubia taifa kupitia mahafali ya CHASO mkoa wa Dodoma kesho

king Davidson

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
252
1,000
Na: CHADEMA STUDENT'S ORGANIZATION- DODOMA (CHASO)

CHASO mkoa wa dodoma inatarajia kufanya mahafali yake ya wanafunzi wa vyuo vikuu vyote vya mkoa wa Dodoma Tarehe 16/06/ 2017 (Ijumaa) ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh. Tundu lissu (mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na Maendeleo- CHADEMA) Na Rais wa TLS.

katika mahafali hayo Mh. Tundu Lissu anatarajiwa kuongozana na mwenyekiti wa Kanda ya kati Mh. Alphonce Mbassa kuongea na wasomi wote wanachama na wapenzi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Kupitia mahafali hayo Mh. Tundu lissu anatarajiwa kulihutubia taifa na kujibu hoja zote za maswala ya raslmali za nchi na mikataba ya raslmali za nchi na mikataba ya kisheria inavyo liangusha na kulifanya taifa kuwa maskini.

Mada aliopewa na wasomi wa vyuo vikuu kuifafanua kisomi ni

"Mchango wa wasomi katika kusimamia, kukosoa na kupendekeza usimamizi na matumizi mazuri ya rasilimali za taifa"

kupitia mada Tajwa Mh. Tundu lissu atajibu hoja zote za kisiasa zilizotolewa na zinazo endelea kutengenezwa na makundi mbali mbali za kijamii za upotoshaji wa uhalisia wa mikataba ya raslimali za Taifa.

Afisa habari CHASO mkoa wa Dodoma Amethibitisha kuwa mahafali yatakuwa Live (Mubashara) kupitia mitandao yote ya kijamii ya CHADEMA.

Nae mjumbe wa kamati maandalizi ya mahafali ya CHASO mkoa wa Dodoma amethibitisha kuwa maandalizi yote ya mahafali ya kisomi na kihistoria yamekamilika na kilichobaki kwa sasa ni mahafali kufanyika.

Mratibu wa CHASO mkoa wa Dodoma amethibitisha kupata kibali cha Jeshi la polisi wilaya ya Dodoma kupitia kwa OCD-DODOMA MJINI. Hivyo kuwataka wasomi wasomi wote kushiriki kwa nguvu na ummoja wao kushiriki na kupata maalifa ya uchambuzi wa kisomi usio egemea upande wowote.


UKUMBI: AFRICAN DREAMS
TAREHE: 16/06/2017
SIKU: IJUMAA
MUDA: Saa 5 asubuhi mpaka saa 11:30 jioni

Imetolewa na Idara ya Habari
CHASO MKOA WA DODOMA
 

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
8,436
2,000
Hayo mahafali au mkutano wa kisiasa? Hauwezi kuruhusiwa. Au anataka kuwasomea taarifa za makinikia ambazo tayari JPM keshazifanyia kazi?
 

SDG

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
7,652
2,000
Sidhani kama event itafanyika,kama itafanyika lazima baadar ataitwa polisi watamhoji kwa uchochezi
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
170,182
2,000
Kuhutubia Taifa means channel zote za ndani(Tz) zitaonyesha live hotuba yake sio kwa kutegemea zile updates za wafanyakazi wake huku Jf
 

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,559
2,000
Kama vile nawaona maafande wanavyohangaika kujaza mafuta magari wakimbie dodoma kuzuia mkutano huo

Mheshimiwa Rais wa Wanasheria na Sheria zote zinazotungwa nchini kesho anamwaga cheche!

[HASHTAG]#chumahunoachuma[/HASHTAG]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom