Polisi wazingira Mahafali ya CHASO Dodoma, Watawanywa kwa nguvu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Magari ya polisi yamezingira African dream kuzuia mahafali ya Chaso Dodoma Kwa madai yakukosa kibali

===========

UPDATES;

===========

POLISI WATAWANYA MAHAFALI YA WANAFUNZI WA
CHADEMA WA VYUO VIKUU VYA DODOMA

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma leo limewatawanya wanafunzi ambao ni wafuasi wa Chama cha Chadema wanaosoma vyuo vikuu mkoani humo walikuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika Hotel ya African Dream.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitalajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi walikamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao.



IMG-20160618-WA0048.jpg

IMG-20160618-WA0054.jpg

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limewasambaratisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ) waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika Ukumbi wa African Dreams ulipo Area D mjini Dodoma.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi wamekamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao.

Polisi wamesema mikusanyiko yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili
 
duu kazi kweli kweli aisee du, lakini si kikao kishaanza, sasa waingie na mbwa ndani kwenda kuvuruga
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Magari ya polisi yamezingira African dream kuzuia maafali ya Chaso Dodoma
Sina komenti kwa sasa ni vizuri ukaleta ushahidi wa pics na kadhalika maana kwetu sisi bado ni yamkini.Na kaama itakuwa ni kweli si la ajabu kwani wapinzani hawatakiwi mkusanyiko wowote ule kwa sasa wala maandamano zaidi ya chama/viongozi dola na tawala kama ilivyotokea Mwanza na Viongozi wa usalama hawajui hilo ila kwa viongozi tu wa Upinzani wanajua kutakuwa na viashiria vya uvunjivu wa amani...lete taarifa kamili tafadhali.
 
Polisi mkoa wa Dodoma wamezuia mahafali ya Jumuiya ya wanafunzi was CHADEMA CHASO Mkoa wa Dodoma yaliyokuwa yafanyike leo na yahudhuriwe na Waziri Mkuu mstaafu Mh Sumaye katika ukumbi wa African Dreams Hotel kwa kile walichoita hayana kibali
 
Back
Top Bottom