OGTV
JF-Expert Member
- May 22, 2016
- 353
- 167
SOURCE : MWANANCHI:
Polisi wazuia mahafali ya shirikisho la wanafunzi Chadema
Polisi mkoani hapa, wamezuia kufanyika kwa mahafali ya wanafunzi wanaounda Shirikisho la wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa Chadema yaliyopangwa kufanyika kwenye Hoteli ya African Dream.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema , Salum Mwalimu amesema wanafunzi saba wamekamatwa katika tukio hilo akiwamo Makamu wa Rais wa Udom, Rose Maluchu.

SOURCE: ITV
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limesambaratisha mahafali ya wanachama wa umoja wa wanafunzi wa Chadema vyuo vikuu (CHASO) kwa madai kuwa ni utekelezaji wa agizo la kuzuia mikusanyiko ya vyama vya siasa kufuatia kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.
SOURCE : MWANANCHI
SUMAYE: POLISI WANATULAZIMISHA TUFANYE SIASA
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema polisi wanawalazimisha kufanya siasa kutokana na kitendo chao kuzuia kufanyika kwa mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya mkoani Dodoma ambao ni wanachama wa chama hicho katika Hoteli ya African Dream.
Sumaye ambaye ndiye angekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema lengo kuu la mahafali hayo ilikuwa kuwahusia vijana wanaomaliza chuo jinsi ya kwenda kuishi kama viongozi na jamii n...a kuwatunuku vyeti lakini walichokifanya polisi ni kuwalazimisha waanze kufanya siasa kwa kulaani vitendo hivyo kila kona.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Dodoma Sumaye amesema kilichomshangaza zaidi hafla kama hizo zimefanyika Mkoani Dar es Salaam kwa viongozi wa Chadema kukutana na wanafunzi wa mkoa huo na pia mkoani Iringa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kukutana na wanafunzi wa mkoa huo.
Picha na Edwin Mjwahuzi