Polisi yaeleza mazingira mwalimu aliyetoweka Simiyu na kukutwa amefariki Musoma

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
432
999
Musoma. Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu Monica Patrick (31) mkazi wa Simiyu aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha baadaye mwili wake kupatikana kwenye kichaka kilichopo pembezoni mwa Ziwa Victoria mjini Musoma.

Pia soma - Mwalimu aliyetoweka Simiyu akutwa amefariki Musoma

Mwili huo ulipatikana na kuopelewa Februari 19, 2023 katika kichaka kilichopo Mtaa wa Nyang'wena mjini Musoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishibwamu amesema leo Jumatano, Februari 22, 2023 kuwa kufuatia uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini mtandao wa watu ambao wanadaiwa kufanya tukio hilo Januari 24 mwaka huu.

Ameeleza kuwa mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Lagangabilili wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu alifika mkoani Mara kwa lengo la kukutana na mganga wa kienyeji aliyemtaja kwa jina la Makere John ili kufanyiwa dua kabla ya kuanza biashara ya madini aliyotarajia kuanza muda si mrefu.

"Baada ya mwalimu kufika na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye ndiye huyo mganga, walikwenda kwa mganga huyo ambaye ni miongoni mwa watu wanaoshikiliwa na jeshi hilo na kukuta watu wengine wanne ambao walisema kuwa ili dua hiyo ili iweze kuwa na matunda mazuri lazima ikafanyikie ziwani," amesema.

Amesema kuwa baada ya maelekezo hayo watu hao watu hao watano pamoja na mwalimu waliongozana hadi ufukweni mwa Ziwa Victoria na kwamba kabla ya kufanyiwa dua mwalimu huyo alitakiwa kunywa juisi iliyokuwa imeandaliwa kama sehemu ya awali ya dua.

"Mwalimu alikunywa juisi ile ambayo tumebaini kuwa iliwekewa dawa aina ya valium na baada ya muda alilewa na kupoteza fahamu," ameeleza.

Kamanda Tibishibwamu amesema kuwa baada ya mwalimu kupoteza fahamu watu hao walimnyonga kwa kutumia mikono hadi alipofariki kisha kutupa mwili wake ziwani kwenye matete ili usiweze kuibuka na kuonekana.

Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo watuhumiwa hao waliondoka na simu ya marehemu pamoja na Sh9.5 milioni ambazo alikuja nazo kwaajili ya dua hiyo, kisha wakatuma ujumbe mfupi wa simu kwa mwalimu mwenzake pamoja na dada wa marehemu.

"Walichukua simu ya marehemu na kumtumia mwalimu mwenzake ujumbe kuwa 'Nimeamua kuacha kazi kwa akili zangu mwenyewe bila kushurutishwa' baadaye wakatuma ujumbe kwa dada yake marehemu kuwa 'Nitunzie wanangu naenda nje ya nchi kutafuta maisha' baada ya hapo hiyo simu haikupatikana tena," amesema.

Kamanda Tibishibwamu amesema kuwa kabla ya tukio hilo mapema mwezi Januari mwalimu huyo akiwa anasafiri kutoka nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro kurudi Simiyu kwenye kituo chake cha kazi alikutana na mtuhumiwa Makere.

Amesema kuwa wakiwa njiani mwalimu huyo alimweleza mtuhumiwa huyo juu ya nia yake ya kutaka kuanza biashara ya madini ambapo mtuhumiwa alimwambia kuwa ili biashara iweze kuzaa matunda kwa haraka ni vyema akafanyiwa dua na mtu wa kufanya dua hiyo alikuwa ni mtuhumiwa huyo.

"Walikubaliana na akaambiwa kuwa akija Musoma aje na Sh10 milioni za mtaji ili ziweze kufanyiwa dua na siku hiyo ya Januari 24 ndipo alipofanya safari na kukutana na hali kadhia hiyo," amesema

Credit: MWANANCHI
 
Jaman tuendelee kumwomba Mungu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na kufanya KAZI halali zitazotuingizia pesa hata kama n kidogo;

Leo tamaa mbaya, ushirikiano na kutaka mafanikio ya haraka vimepoteza maisha ya ndugu zetu wengi na wengine wameua wenzao ili wafanikiwe!

Hili tukio limeniumiza Sana na kunipa kuwaza mengi kwamba binadamu tunaoishi nao na hata kuongea nao wengi mawazo mabaya n si watu mwema kwetu!Mungu atusaidie Sana!
 
Biashara ya kutegemea uchawi, ni biashara ya kipuuzi tu. Pole sana mwalimu kwa kuamini kufanikiwa kupitia nguvu za giza.
 
"Walikubaliana na akaambiwa kuwa akija Musoma aje na Sh10 milioni za mtaji ili ziweze kufanyiwa dua na siku hiyo ya Januari 24 ndipo alipofanya safari na kukutana
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
RIP Mwalimu!
 
Kumbe mualimu alikua mtu wa kilimanjaro, alitaka kuanzisha biashara ya madini, alitaka pesa zake ziombewe kwanza loh!
Hapo ndio utakapojua kuwa tajiri kuingia kwenye ufalme wa mbinguni ni shughuli pevu...
 
Hao mbuzi wawakamue vinyeo mpaka waharishe utumbo. Bora wangempa tu madawa wakayeya na pesa.
Kuna mwingine walimuua maeneo ya Madale katoka kutoa pesa pale Kibo Complex Tegeta, wakamdaka wakamvutia kwenye gari. Wakaenda kumpora na kumvunja shingo Madale wakautupa mwili huko.
Senge sana hawa watu.
 
Hao mbuzi wawakamue vinyeo mpaka waharishe utumbo. Bora wangempa tu madawa wakayeya na pesa.
Kuna mwingine walimuua maeneo ya Madale katoka kutoa pesa pale Kibo Complex Tegeta, wakamdaka wakamvutia kwenye gari. Wakaenda kumpora na kumvunja shingo Madale wakautupa mwili huko.
Senge sana hawa watu.
Madale sehemu gani ndugu,mimi ni mwenyeji sana mitaa ile tangu Barabara ikiwa vumbi mpaka leo kumekuwa kwa kishua
 
Back
Top Bottom