Polisi wetu ni wana CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wetu ni wana CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Jun 16, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimefedheheshwa na kitendo cha kiongozi wa juu wa jeshi la polisi kutangaza nia zao za ubunge kwa tiketi ya CCM.

  Tibaigana, na jana nikachoka kusikia kamanda wa trafiki Kombe.

  Hivi hawa walijiunga na chama lini au walikuwa na rangi ya kijani mfukoni? Muda waliostaafu awajapata uzoefu wa siasa hizo.


  source: Kamanda Kombe kuwania ubunge Vunjo
   
 2. kabyesiza

  kabyesiza Member

  #2
  Jun 16, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  The constitution does not prohibit any Ex-officer of the government from contesting or exercising the right to peaceful petition the government , who having previously served under any administrative entity of either branched of the government , such prohibition lays up on to the hands of the people when exerting their constitutional right to vote!

  No for this case just how stupid the some folks are, will go ahead and put those individuals back into the system and continue wining about the acts of the government for not fulfilling its duty ... Good luck!!
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hawa wezi na mafisadi wakubwa hutashangaa kuwa wamerudi serikalini kwa mlango wa ubunge. Wasipewe nafasi hizi kabisa maana tunafahamu walivyokuwa si waaminifu wakiwa kazini.
  Hold on, Msharika anachosema ni kweli. Ingawa sheria haiwazuii wafanyakazi kugombea lakini inawakataza kuwa members wa vyama. The questions begins here, inakuwaje wanaacha kazi lakini kwenye maelezo yake anaonyesha alikuwa active member wa chama kwa miaka yote tangu uhuru? Hapa ndipo nadhani maswali mazito yanapoanzia. Issue ni kwamba pamoja na sheria tukigundua kuwa mfanyakazi anayebanwa na sheria za vyama akigundulika alikuwa kada wa chama akiwa kazini what next? otherwise sheria hiyo haina maana ni bora waachwe kwenda mbele kwa mbele kila mtu awe member wa chama cha siasa Tanzania.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huwa si wana-CCm wanapokuwa kazini, bali kwa vile wamekuwa wakitumikia sera za chama kinachotawala kwa miaka nenda rudi, then automatically wanakuwa kama wanachama.
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Huna haja ya kusikitika na kufedheheka mkuu(utajiumiza bure)........Tanzania ni nchi ya kidemokrasia.....Na hawa maafandea ni haki yao ikatiba kujiunga na chama chochote(ikiwa ni pamoja na kugombea uongozi kwa chama chochote wanachokitaka) ikizingatiwa tu hawavunji sheria.......

  Vipi kama wangetangaza kugombea kwa tiketi za UDP,CUF,CHADEMA,TLP ama NCCR-Mageuzi.....Bado ungesikitika tu?
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  1.Hivi wakuu,sheria inasemaje kuhusu watumishi wa serikali na shughuli za kisiasa....Je wanaruhusiwa kuwa wanachama wa vyama vyovyote pasipo kujishughulisha moja kwa moja na siasa(kuwa active katika shughuli za kisiasa?) ama wanakatazwa(hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vyovyote vya siasa)......Pasco popote ulipo naomba uje hapa uniweke sawa hapa(please)

  2.Nini maana ya Kada(cadre)?
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kamanda Kombe kuwania ubunge Vunjo


  na Beatrice Maina, Moshi


  [​IMG] ALIYEKUWA mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishna (ACP) James Kombe ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31. Kombe ametangaza nia hiyo jana mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema ameamua kutangaza baada ya wananchi wa jimbo hilo kumuomba awanie kiti hicho kinachoshiliwa na Aloyce Kimaro.
  Alisema baada ya kustaafu alirudi kijijini kwake ili kuendelea na shughuli mbalimbali lakini wananchi walimtaka awania ubunge kwa kuamini uwezo wake pamoja na kuwa yeye ni kada wa siku nyingi wa CCM.
  Alisema wananchi walimtaka ajitokeze katika kinyang'anyiro cha kura za maoni na ameamua kukubaliana na ombi lao huku akiamini atashinda kiti hicho.
  "Miezi miwili iliyopita wanachama waliandamana mpaka nyumbani kwangu kuniomba nijitokeze kwenye kura za maoni za kugombea ubunge katika jimbo hili la Vunjo," alisema Kombe.
  Alisema endapo atashindwa katika kinyang'anyiro hicho ataendelea kushirikiana na atakayechaguliwa katika kampeni za uchaguzi ili kuhakikisha jimbo hilo linaendelea kuwa mikononi mwa CCM.
  Kombe ni mgombea wa tatu kutangaza nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mbali na mbunge wa sasa Aloyce Kimaro na mwanasheria Chrispin Meela.
  Mpaka sasa wagombea watano wamekwishatangaza nia ya kugombea akiwemo Mwenyekiti wa TLP Agustino Mrema pamoja na mkurugenzi wa shughuli za Bunge na halmashauri ya CHADEMA, John Mrema.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  .
  Balantanda, Wajeshi, Polisi, Wanausalama na Waserikali, hawaruhusiwi kujishughulisha na siasa wakiwa katika nyadhifa zao, ila haki zingine zote zakiraia wanazo kama raia wengine wowote ikiwemo haki ya kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila wasishabikie siasa, hivyo hizi taarifa za mjeshi fulani, polisi fulani au mserikali fulani kuwa kada wa chama akiwa kwenye utumishi wa umma, morally its wrong ila practically ndio watu wa kupongezwa na kupewa ulaji zaidi na zaidi kwa vile ni makada wa chama tawala.

  The deviding line kwenye conflict of interest btn their political affiliation and duty of care is very thin, ndio maana Mahita, Ex-Darasa la 8 akiwa RPC Moshi, alimvurumishia mabomu Mrema bila huruma, akaonekana amefanya kazi mzuri, akapewa U IGP, hata kwa kumwangalia tuu machoni, utatambua wazi, thinking capacity yake ni sero flani kama kina Makamba type.

  Sasa hawa wakuu baada ya kustaafu utumishi wa umma, wanahaki kushiriki shughuli za kisiasa kama raia wengine, ndio maana uliwaona kina Maj.Gen. Jesse Makundi, ulimsikia Mboma, Afande Tibaigana etc, ni haki yao.
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana mkuu........Hope hii itasaidia kupunguza lawama na tuhuma zisizo na msingi dhidi ya watanzania hawa(waaliokuwa watumishi wa serikali) walioamua kuitumia haki yao ya kikatiba kwa kugombea uwakilishi bungeni
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi naona ni kale kamchezo kao ka kupenda kutufisadi tu kwa kila kona. Pia wamezoe kutetemekwa si unajua raha ya madaraka sasa kustaafu then ukawe mkulima kijijini hivi hivi wakati ulishazoea masaruti na viroba vya mchele na nyama unaweza kufa kabla ya wakati wako mwisho ndio hao wanakimbilia kugombea ubunge!!! Hawana lolote hao!!!...ngoja wapewe kura ili waweze kula!!!:hungry::hungry::hungry:
   
 11. I

  Isae Member

  #11
  Jun 17, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli lazima tushangae kwani wanaosema sheria haiwakatazi sio kweli kwani kisheria Askari yeyote hatakiwi kuwa na chama, sasa Kamanda Kombe kastaafu juzi tu je kachukuakadi tu ya CCM na kugombea Ubunge? Shaka ipotena kubwa sana na hawa askari wetu
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jun 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Binafsi ningewapiga marufuku majaji, maafisa wa jeshi kuanzia vyeo vya Kanali na Mrakibu Mwandamizi kugombea nafasi ya kisiasa ndani ya miaka mitano baada ya kutoka katika nafasi yao jeshini.
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Habari ndiyo hiyo. HUkujua Mkuu? Huwaoni wanavyoenenda katika kazi zao? Elewa kwamba ""Polisi wala wanajeshi hawana chama"" Na ukiona wanacho chama basi usome hivi, ""Polisi wala wanajeshi hawana chama""
   
 14. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka mwaka 2005 kipindi cha kampeni, magari makubwa(maroli) na madaladala yaliyobandikwa picha ya mgombea wa urais wa ccm, JK
  Matrafiki polisi walikuwa hawayasiamamishi.
  Hii inadhihirisha mapenzi yao ya dhati kwa chama tawala CCM.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,515
  Trophy Points: 280
  .
  Mzee Mwanakijiji, huku kutakuwa ni ukwiukwaji wa haki za binaadamu, ila kwa mtu mwenye akili timamu, kuna issue ya moral resiponsibility kwa jamii uliyoitumikia, binafsi naona ni kujiaibisha na kujidhalilisha, leo Mbona achukue fomu, Apson nae achukue, Mahita pia achukue, kwa kujiaminisha na utumishi wao uliotukuka ndani ya serikali, wanajifariji walifanya kazi nzuri, lakini chama kinaweza kuwagomea kuwapitisha kwa vile sio popula, hii si ni aibu ya mwaka!.

  Nadhani hawa makamanda, tuwaache wajistaafie tuu kwa heshima.
   
 16. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Waraka wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2000 unaeleza wazi katika Ibara ya 8 kuwa WATUMISHI WA UMMA WASIORUHUSIWA KUSHIRIKI KATIKA SIASA:

  "Kwa mujibu wa Ibara ya 147(3) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" ni kama ifuatavyo:

  Askari wote wa Jeshi la Wananchi "JWTZ", Jeshi la Kujenga Taifa "JKT", Polisi na Magereza.

  Sasa hapo wanapotangaza nia nadhani inategemea na Taratibu za Chama husika, kama unaweza kuchua kadi leo na kuomba nafasi au mpaka uwe na uanachama usiopungua muda fulani. Kwa kuwa hawa walikuwa watumishi wa Umma na wamesha koma Utumishi wao, wana haki kama raia wengine kugombea nafasi yoyote ya Kisiasa.

  Tuchukulie mfano wa CCJ, chama ndio kwanza kinaanza unataka kuniambia kuwa wagombea wake wanatakiwa kuwa ni Wanachama kwa muda gani? Kama Kombe angegomea kupitia CCJ ungekuwa na la kuhoji?

  Lakini nashukuru kwa hoja kwani itawasaidia na wengine kuelewa Uraia.
   
 17. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Pasco,
  Hiyo haki ya kugombea hatuipingi. Kinachogomba ni hiyo bolded. Kama angestaafu halafu akachukua kadi ya chama akipendacho na kuomba kusimamishwa hakuna shida; ila pale anaposema kuwa yeye ni kada wa siku nyingi, ndipo panapoleta shida. Wakati alipokuwa kamanda alienganishaje kazi yake na ukada wake? Kwasababu, anapotakiwa kusimamia haki itendeke wakati huo huo anamaslahi ya chama chake, itaishia tu kuwapiga mabomu na kuwatia ndani wanachama wa vyama vya upande wa pili. Nadhani tungekuwa na tume huru ya uchaguzi ingeliangalia hili na kulitolea kauli, ila kwa kuwa majeshi yote, tume pamoja na msajili wa chama ndio hao hao, ndipo inapokuwa taabu.
   
 18. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Tunawasubiri kina Tendwa na Makame waje pia kuelezea ukada wao wa siku nyingi na kuomba kusimamishwa kugombea kwa ticket ya CCM kwani haikosi nao ni makada wa siku nyingi
   
 19. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kuwa hawa makamanda wastaafu wana HAKI ya kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi baada ya kustaafu kwao, lakini ni wazi pia kutokana na uanachama wao kwa CCM ( ambao hawakuukana wakiwa madarakani) hawakusimamia haki! na hii ni dhahiri kabisa kumbukeni Mahita alivyokuwa akiwaandama CUF kipindi kile hadi akawazushia kuwa mameakiza kontena la jambia, alipoombwa atoe proof, kimya, na sasa nimesikia ana nia ya kugombea ubunge Morogoro Mjini! Ki maadili tu hawa jamaa wasingegombea sasa wangesubiri labda 2015! lakini kwa kuwa ni wale wale wachumia tumbo hawaoni hii conflict of interest na doubt juu yao!
   
 20. T

  Tom JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zamani kila mmoja alikua mwanachama wa CCM kwa lazima kwa njia moja ama nyingine, sielewi kama kuliundwa utaratibu wa kufuta uanachama wa CCM baada ya kuudwa vyama vingi hasa kwa watu kama Polisi.
   
Loading...