Polisi wazuia mkutano wa UKAWA Zanzibar

Polisi wazuia mkutano wa UKAWA Zanzibar

Matendo ya ghiliba kama haya ndiyo yatakayoingiza nchi kwenye machafuko.Tusonge mbele
 
Ccm wapo ukingoni...wanaelekea kuanguka. chama dola nguvu yake inaegemea kwa dola tu kama mbuyu...siku mbuyu ukioza na kushuka....anguko hilo ni wachache wnaojua mshindo wa mbuyu.

Hata enzi za Gadhafi alishajihakikishia kujilinda na kudhani 'anapendwa' sana hadi kuwakejeli waandamanaji kuwa ni PANYA wanaohangaika, alichoshtukia ni pale 'panya' walipoungana na 'PANYA waliokabidhiwa silaha ili kumlinda' (wanajeshi wake mwenyewe) hadi kakimbilia ktk makaro ya Panya kweli, alikookotwa na kujitambua kuwa ni Panya wake mwenyewe wamemweka mikononi...majeshi hayana reliable sustainability kwa wanasiasa...! Siku jeshi linaona kilio cha umma kinasimama imara nalo linasimama kulinda haki na uimara, wanaamua ukweli. Ccm wanaelekea mwishoni.
 
Ccm bado wanatumia propaganda hatari kulinda maslai yao. Udini, Ukabila na Ugaidi.
Hii ni hatari sana.
 
Wataweza mzuia makamo wa raisi kuhudhurua mkutano? Patachimbika
 
Tunatafutiana sababu tu tuonekane hatueshimu sheria za nchi....
 
Watawala wanazidi kudhihirisha kuwa mikutano ya hadhara ni sumu kali kwao na hawana uwezo linapokuja suala la ushawishi wa kisiasa na hoja kwa wananchi.

Wanawasukuma wananchi kwenye 'either make or break it' point!
 
Kwasababu wameshaeema kuna ugaidi lazima ccm wafanye kila njia ili ionekane kuwa kuna ugadi kwenye mikutano ya wapinzani kwa kutupa mabomu kwenye mikutano ya UKAWA wakati kinana na nape wanatamalaki lakini hakuna tishio ka ugaidi
Ngoma bado mbichi kila rangi wataona mwaka huu ccm
 
Ukiona kiongozi anayezuiya maandamano anaanza kuvunja katiba na kuvunja katiba ni kosa la jinai, sasa kama polis wamezuiya maandamano wametumia sheria ipi? Au ndio yale yale ya viongozo wengi barani afrika wanaongoza kwa kuvunja katiba zao wenyewe? Napenda kuwakumbusha viongozi wa tanzania yaliyo mkuta gadafi yatawakuta
 
Ningeshaa sana kama mkutano huu ungefanyika,
1UKAWA si chama cha siasa.ni kundi fulani ndani ya bunge tu
2)Hao UKAWA wametoroka kazi bungeni baada ya kutumia fedha nyingi za umma
3)Hao UKAWA wametoroka bungeni baada ya kukashifu waasisi na wakiwa na munkari
4)Kwa maana hii walikuwa wanaenda kuendeleza munkari na kashfa zao mitaani
5)KINANA hajatoroka bungeni,hajakashfu mtu hat mdogo na hana munkari wowote

so what is your point
 
Yaaani ccmni kama hili jamaaa
 

Attachments

  • 1397839613127.jpg
    1397839613127.jpg
    20.1 KB · Views: 175
Ni vigumu sana kuzuia mafuriko ya mvua za Elnino(UKAWA).
UKAWA ni level nyingine.
 
Naomba nakala ya usajili wa chama kiitwacho UKAWA.
 
Ni wazi huu Muungano ni wa viongozi wachache wa CCM.
 
Mkutano upo pale pale hadi tupate maelekezo kutoka UKAWA.
 
Kupiga marufuku mikutano ya hawa watu ni kuwaongezea umaarufu, ni vizuri wangeruhisiwa kikubwa Jeshi la Polisi lingeimarisha ulinzi tu, maana sasa watanzania wataelewa kuwa wanaogopwa. Wangeachwa wakaeleza kile wanacholalamikia, kisha kila mtu angeongeza akili za mwake mwenyewe kwa kuchambua pumba na mchele.
 
Barua kutoka Jeshi la Polisi kwenda kwa Katibu Mkuu CUF 18.04.2014

YAH: TAARIFA YA KUSITISHA MKUTANO WA HADHARI
Naomba urejee barua yangu ya kumbukumbuku namba ............ya tarehe 17 April 2014 inahusika.

Ninakujuulisha rasmi kua, Mkutanoh huo uliokuwa ufanyike kesho tarehe 19 April 2014 hapo Viwanha vya Demokrasia Kibanda Maiti umesitishwa kwa sababu za KIUSALAMA WA NCHI.
Kwa barua hii, unatakiwa kuwajuulisha Wanachama na wapenzi wote wa Chama kuwa watulivu kwa muda huu, hadi hapo hali itakaporuhusu kufanyika tena kwa mkutano huo.

Tafadhali nawasilisha

Ramadha ....SSP
Mkuu wa Polisi
Wilaya ya Magharibi Unguja


[h=2]Askofu Kakobe kuzungumzia muundo wa Muungano katika Neno la Pasaka 20.4.14[/h]
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa waumini wanaosali katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), linaloongozwa na Askofu Mkuu Zachary Kakobe, zinaeleza kwamba, Jumapili iliyopita katika Ibada Kuu ya Kanisa hilo, lililoko Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar-Es-Salaam, karibu na Mlimani City; Mzee wa Kanisa anayehusika na matangazo, alitangaza kwamba, katika Ibada Kuu ya Sikukuu ya Pasaka, Jumapili hii tarehe 20.4.2014, Askofu Kakobe atahubiri Neno la Mungu, ambalo pamoja na mambo mengine ya rohoni, litazungumzia pia juu ya mustakabali wa nchi yetu, hususan kuhusu Bunge Maalum la Katiba, linaloendelea na vikao vyake, mjini Dodoma. Hata hivyo, taarifa za uhakika zilizopatikana jana, kutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Kanisa hilo, zinafafanua kwamba, Askofu Kakobe, atachukua muda mrefu zaidi katika mahubiri yake, kuzungumzia juu ya muundo wa Muungano unaoifaa nchi yetu.

Ibada Kuu ya Pasaka katika Kanisa hilo, itaanza saa 3 kamili asubuhi, na kumalizika saa 6.30 mchana. Hata hivyo, kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Mavazi, za Kanisa hilo; Viongozi hao wa Kanisa, wamewakumbusha watu wote watakaohudhuria, kumheshimu Mungu kwa mavazi watakayoyavaa. Watakaovaa vimini, jeans, milegezo, na nywele bandia; hawataruhusiwa kuingia katika Nyumba hiyo ya Mungu. Vilevile, wanawake hawapaswi kuvaa suruali, na wanatakiwa kufunika vichwa vyao. Vivyo hivyo, wanaume hawakubaliki kuingia Kanisani humo, wakiwa wamevaa kofia.​
 
Bora, hakuna cha CUF wala CCM, wanataka kutoa nafasi ya uamusho kumwagia watu tindikali tu hao
 
Back
Top Bottom