Polisi wazuia mkutano wa UKAWA Zanzibar

Polisi wazuia mkutano wa UKAWA Zanzibar

Naamini wakilazimisha kichapo cha wananchi watakipata. Pesa wanazolipwa na wenyenchi ni kwa ajili ya katiba tu bungeni sio mikutano ya eti kuja kupima je, huko mitaani tuna wajinga wangapi? Ukishindwa kuchangia ama kujenga katiba ilo bora ondoka!
Mikutano mnayoitaka itajadili katiba kwa kanuni gani! Msiwafanye watz wote majuha.
Mambo yote bungeni hadi kieleweka.
Ukawa acheni utapeli hao cdm watawakokota kama mkokoteni hauna breki hadi shimoni puuuuuuuuuuuii
 
UOGA AU SHERIA DHIDI YA.
UKAWA???
Katika hali inayoshangaza watu wengi ndani na nje, ni kupigwa maarufuku kwa UKAWA kufanya mkutano wao hapo kesho tarehe 19/04/2014 mjini Zanzibar
Hili kwangu limeniogopesha sana na kuona kuwa wana- Ukawa wamenyimwa haki ya kikatiba kama viongozi wa Vyama vyao. Katika jumuia yao kuna viongozi wa kitaifa kama Prof. Lipumba, Mbowe na Mbatia. Hawa ni viongozi ambao wanapaswa kuheshimiwa kama walivyo wale wa Serikali.
Lakini kitendo cha kuwanyima ruksa ya kufanya mkutano ni kuwavunjia nidhamu ya mamlaka yao katika taifa hili.
Mi na hofu kuona kuwa Tanzania tuitakayo haiwezi kupatikana bila katiba mpya yenye nchi mbili huru na zenye mamlaka kamili.
Si busara zilizotumika kuwanyima Viongozi hawa wasifanye mkutano huko Zanzibar. Hivi inaweza kuwa ni sababu za kiusalama au ni hofu tu ya kisiasa?
Tanzania ni nchi ya Vyama vingi na ya kidemokrasia Ibara ya 3(1), kama ni hivyo kwanini viongozi wa vyama na wengi ni waserikali kama Seif wanakataliwa kufanya mikutano? Hiyo demokrasi ipo wapi sasa? Au ni demokrasia kwa baadhi ya watu fulani? Mbona haijawahi kutokea kiongozi wa CCM anakataliwa kufanya mkutano kwa sababu za kiusalama?
Ndugu zangu hii nchi ni yakwetu sote, hakuna mwenye haki kuliko mwingine kama kweli ni kidemokrasia, ila kama ni ya Kidikteta. Hatuwezi kupongeza dhuluma ifanyike nasi tushangilie, hata kidogo, kama mtapiga makofi mimi niko radhi kubaki mwenyewe ni kilia na kuomba haki itendeke.
CCM naipenda sana kwa kuwa nafahamu misingi yake ilivyo, na hapo ndipo nikoradhi kuitetea popote pale kwa mazuri yake. Lakini ni budi sana kukosoa pale panapoonekana hapaendi sawa ima kwa kusababishwa na mwanachama, kiongozi au mtawala fulani.
Nilipenda sana kauli ya Katibu mkuu wa CCM ndg. Comrade Kinana aliyoitoa jana akiwa Katavi kuwa '' Milango iko wazi kuikosoa CCM na Viongozi wake kwa kuwa ndiyo demokrasia''
Hii kauli ni nzuri kwa wenye busara tu, na wale makanjanja wataiona haifai kwa kuwa hawataki kukosolewa kwa matendo mabaya wanayofanya katika kudidimiza taifa hili. Mfano mzuri ni ile kauli ya Lukuvi aliyoitoa Kanisani kuwa Zanzibar ikijitenga itaongozwa katika mfumo wa kiislamu. Hii ni kauli ya kichochezi, kiubaguzi na inaonyesha chuki yake dhidi ya Waislamu.
Kwa hili namshauri kwa niaba ya serikali ajiudhuru ili kuiachia Nchi ipumue sivyo itasababisha mambo yaliyofichwa yatolewe.
Kila Nchi inasiri nyingi za kiutawala lakini kwa TZ itakuwa imefikia mwisho katika utunzaji wa siri hizi. Na hii imesababishwa na watu kama Lukuvi kuanza kutugawa kidini, kiukanda na kimakabila.
Naomba tena, utu uzima wake autumie kujiudhuru ili kupisha Rais kuteua mtu mwingine mwenye busara kuongoza Sera na Uratibu wa bunge, maana busara zake zimefika mwisho.
Nchi hii imevimba inapaswa kupumua sasa na ikicheleweshwa itapasuka yenyewe, hapo itakuwa haiwezekani tena kurudishwa katika amani iliyodumu kwa miaka zaidi ya 50. Viongozi wa Chama changu cha Mapinduzi, tuangalie na tuendane na madiliko ya Elimu, Technolojia, utandawazi na Demokrasia la sivyo tutaipeleka Nchi katika machafuko makubwa na yatakayotugharimu sana mali zetu, uhuru wetu, amani yetu na umoja wetu.
Mungu ibariki Tanganyika, Zanzibar na Jamuhuri ya Tanzania . Amin
BY TWALLYIB YASSINI

source:BUSTANI YA HABARI
 
Swali ninalojuliza sana ni kwanini JK alianzisha mchakato wa kuandika Katiba ?
 
- Watu wa Dini wameomba kwamba wakati huu wa Pasaka wasingependa kuona kunakuwa na Mammbo ya Mikutano ya UKAWA ni ombi lenye mantiki ndio maana wakakubaliwa, hao UKAWA wasubiri Pasaka iishe waanze fujo zao!!

Le Mutuz System
 
Ukijifanya unajua hili wenzako wanajua lile! Tutaona mwisho wa ukawa.
Rich Pol
===>Hakuna serikali ambayo imemaliza kazi zake kwa usalama kwa kutumia vyombo vya dola badala ya kusikiliza wananchi,
===>Hakuna haja ya kuonyeshana nani ni nani,uhai ni haki ya kila mtanzania,kila mtu atumie busara,aliekosea hili awajibishwe,anajulikana,ni Mzee wetu Lukuvi.
 
Last edited by a moderator:
Tayari hii nchi iko chini ya jeshi make haya matamko ya kijeshi kukandamiza katiba ndo utawala wa jeshi lenyewe alivyotwambia Lukuvi

Swali,vip Znz kuwepo na hari ya hatari na dar pawe shwari kwa maana leo kuna mechi ya simba VS yanga? ama alshaabab wameelekeza mitutu yao Zenji tu,tafadhari makamanda jibuni hili.
 
Mbona katibu mkuu wa ccm anazunguka, jana alikuwa Katavi kwa ajili ya kupigia debe serikali 2?
 
- Watu wa Dini wameomba kwamba wakati huu wa Pasaka wasingependa kuona kunakuwa na Mammbo ya Mikutano ya UKAWA ni ombi lenye mantiki ndio maana wakakubaliwa, hao UKAWA wasubiri Pasaka iishe waanze fujo zao!!

Le Mutuz System

Watu wa dini? Lini na wapi? Na mikutano ya hadhara ina uhusiano gani na dini.ukizingatia kuwa mkutano unafanyika zanzibar.hata kama unahitajika ulinzi katika nyumba za ibada wakati wa pasaka askari wanatosha kulingana na uchache wa waumini wa dini ya kikristo.kwahio kisheria na kimantiki watawala wameishiwa hoja.na namshangaa ndugu Malecela kutoa hoja dhaifu kama hii.hoja dhaifu haitoki isipokuwa kwa watu dhaifu.
 
Mbona katibu mkuu wa ccm anazunguka, jana alikuwa Katavi kwa ajili ya kupigia debe serikali 2?

- Basi warudishe kwanza posho baada ya Pasaka ndio waanze fujo zao tunajua hawana jipya wanafikiri wanaweza kupata kura Zanzibar, vituko vitupu!!

Le Mutuz System
 
Tusitake kurekebisha jambo kwa hasira. Ktk hili na hasa penye wengi kuna mengi.
Umuhimu ni kujitambua nn tunataka ktk mapindinzi yetu ya kiuchumi, kisiasa nk. Sio tuangalie nani kakosea adhibiwe. Anaye hitaji adhabu ni yule tu asiyetaka maendeleo ya watz kujikomboa kiuchumi
 
Watu wa dini? Lini na wapi? Na mikutano ya hadhara ina uhusiano gani na dini.ukizingatia kuwa mkutano unafanyika zanzibar.hata kama unahitajika ulinzi katika nyumba za ibada wakati wa pasaka askari wanatosha kulingana na uchache wa waumini wa dini ya kikristo.kwahio kisheria na kimantiki watawala wameishiwa hoja.na namshangaa ndugu Malecela kutoa hoja dhaifu kama hii.hoja dhaifu haitoki isipokuwa kwa watu dhaifu.

- Viongozi wa Dini wameomba kwamba hawataki vurugu za Lipumba na Mbowe wakati huu wa Pasaka ndio maana wakakubaliwa ikiiisha nendeni mkaandamane tani yenu!!

- Na wala sina tatizo kupokea matusi yako kwamba mimi ni dhaifu, mmetukana Baba baba wa Taifa hili itakuwa mimi hulka yenu ni matusi, sijui mtamtawala nani zaidi ya wenyewe kwa wenyewe mabingwa wa matusi!!

Le Mutuz System
 
Kwani ukawa waliomba kibali cha kufanya fujo mkutano,wacheni kukurupuka na hoja dhaifu.
 
ccm bara wamenyweshwa limbwata la serikali 2, kumbe wa visiwani ni wajanja duu!
 
- Basi warudishe kwanza posho baada ya Pasaka ndio waanze fujo zao tunajua hawana jipya wanafikiri wanaweza kupata kura Zanzibar, vituko vitupu!!

Le Mutuz System

mkuu,wewe unavuta bhange la wapi!?mbona povu tu
 
Serikali ya mkataba zaid zaid ni darajani na malindi na pemba kwa kiasi chao.
Walobaki ni walinda mapinduzi huwadanganyi kwa maandamano wala mikutano. Kina nape wanakagua utekelezwaji wa sera ya chama chao.
Wanapokuta uzembe mtu anawajibishwa kama mawaziri wale wakati wa kusaka majangili. Wengine nafasi ni hii ya kujenga katiba, kiongozi wako akiweza ni sifa kubwa kwake na taasisi yake. Bungeni ndipo pakuonyesha umahiri juu ya hii katiba. Pia ni tunu kwa mtu atambuaye maana!
 
Back
Top Bottom