Ni hatari, nchi inaelekea kubaya
Alirudishe tu,tutatengeneza mabulungutu ya kwetu wenyewe.Kabisa Mkuu juzi nimeona tena Mo Ibrahim karudisha bulungutu lake Bungeni kwa kukosa Kiongozi mstaafu wa Afrika akiwemo Kikwete kushindwa kutimiza vigezo vya utawala bora walipokuwa madarakani.
Inashangaza sana kuona mtu anachukua uongozi wa nchi na kuahidi mazuri mengi ikiwemo kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania lakini akishaingia tu Ikulu basi anageuka na kulinda maslahi ya wezi, mafisadi, watoa rushwa na wapokea rushwa na huyu wa sasa kaingia na jipya la kukandamiza haki zetu za kikatiba katika kujadili mambo mbali mbali nchini ikiwemo mustakabali wa nchi yetu. Anataka tuwe mazombie na maovu yote nchini tuyanyamazie. Inasikitisha sana kusema kweli. Na hivyo vyama vya upinzani watangaze rasmi kwamba vimefutwa.
Watu ambao wamejikita zaidi kwenye democracy wakati wanatakiwa wajikite zaidi kwenye shida za wananchi za kila siku watakua hawawazi vizuri.
Ndugu watanzania, naomba mniombee. Nimejitoa mhanga kuwakomboa watu wa hali ya chini ambao naamini ndiyo walionipa kura nyingi. Mimi sikuchaguliwa na matajiri. Mnataka nimtumbue hapa hapa au? Namlipia huyu kijana akapate huduma huko regency. Hivi mlitarajia serikali iendelee kuwalipia na kuwakumbatia hawa va la za ? Haiwezekani kabisa hao wanaowatetea nao ni va li za. Hakuna siasa vyuoni. Nakumbuka hata JK hakuwa hata na kadi ya TANU alipokuwa chuo. MTAJIJU.
Ndio sababu nimemshauri mtoa kauli hiyo aifute. Hatutaki mashetani wala hatutaki malaika. Tunataka watu waishi kama binadamu na sheria iwe ni msumeno.Kuishi kama shetani haitawezekana.
Bado kumzingira Mungu sasa na yeye akifanya Fyokofyoko anazingirwa. malaika jiandaeni!Polisi wamsaka Gwajima....Polisi wamuhoji Zitto, Polisi wazuia maandamano Pemba, Polisi watangaza kuzuia mikutano ya kisiasa nchi nzima, Polisi wazingira hoteli ambayo ACT wangelifanyia mkutano wa bajeti, Polisi wamkamata kijana aliyemuita rais "Bwege", Polisi wawatawanya wanafunzi wa UDOM waliohudhuria mahafali ya CHASO katika hoteli moja huko Dodoma, Polisi wazuia msafara wa Maalim Seif, Polisi.....Polisi....Polisi!!!!!!!????????
Ukiona kila taarifa ya habari inaanza na Polisi, jua tayari tumeingia kwenye...........
Kwa hisani ya Mtatiro
Tatizo mnalaumu idara ya polisi bila kufahamu kuwa polisi wanafanya kazi yao ya kila siku nayo ni kutekeleza maagizo kutoka kwa watawala, nashauri tusiwalaumu polisi wetu bali lawama zote zipelekwe kwa wanaotoa hizi ORDERS. Idara yetu ya Polisi ni nzuri sana sema aina ya wanasiasa tulionao ndio wanawaingiza matatizoni.Uzi huu unaweza kabisa kuwa muafaka kuhusu unyanyaswaji mkubwa unaofanywa na Polisi nchini katika kubaka demokrasi ili kutimiza lengo la Dikteta la Watanzania kuishi kwenye nchi iliyojaa vitisho vya hali ya juu. Kufungua uzi mwingine pia wa manyanyaso ya Polisi nchini RUKHSA.