Polisi wamsaka ...

Polisi wamsaka ...

Kabisa Mkuu juzi nimeona tena Mo Ibrahim karudisha bulungutu lake Bungeni kwa kukosa Kiongozi mstaafu wa Afrika akiwemo Kikwete kushindwa kutimiza vigezo vya utawala bora walipokuwa madarakani.

Inashangaza sana kuona mtu anachukua uongozi wa nchi na kuahidi mazuri mengi ikiwemo kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania lakini akishaingia tu Ikulu basi anageuka na kulinda maslahi ya wezi, mafisadi, watoa rushwa na wapokea rushwa na huyu wa sasa kaingia na jipya la kukandamiza haki zetu za kikatiba katika kujadili mambo mbali mbali nchini ikiwemo mustakabali wa nchi yetu. Anataka tuwe mazombie na maovu yote nchini tuyanyamazie. Inasikitisha sana kusema kweli. Na hivyo vyama vya upinzani watangaze rasmi kwamba vimefutwa.

Tuzo za Mo zitaendelea kukosa wakupewa kwa miaka mingi sana ijayo mkuu, utawala bora, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, uwajibikaji vinazidi kuwa bidhaa adimu sana kwenye hizi nchi zetu.
 
Ameshanunuliwa huyu Mkuu, si yule Mwanakijiji aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini wa kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania na kuwa mwiba mkali sana kwa Serikali ya awamu ya nne na mafisadi nchini. Sijui wamemlipa kiasi gani.

Mzee Mwanakijiji......anaamini dikteta wa Magufuli ndo kinachotakiwa Tanzania
 
Mkuu Samaritan hakuna aliye salama, labda kama maovu yote unayoyaona nchini mwetu uyafumbie macho na kuamua kukaa kimya. Kitu ambacho si sawa. Kwanini Watanzania tukae kimya kama tunaona nchi yetu inaharibika? Kwanini tukae kimya kama haturidhiki na uongozi wa nchi na maamuzi yao mbali mbali ambayo yanatuathiri Watanzania? Je, hao wanaotaka kutunyamazisha tusiwakosoe na kukemea maovu mbali mbali nchini wao wana hati miliki ya Tanzania? Jibu ni HAPANA Tanzania ni yetu sote.
Mkuu BAK nimejiuliza sana nikiwa usingizini. Majeshi yetu hayatakiwi kuwa na upande katika siasa. Lakini Polisi wameamua kuwa sided na ccm. Jee kesho tukiamka JWTZ nao wameamua kuwa na upande kwa Chadema, KMKM na CUF jee tutafika au tutakuwa kama Misri ile ya Mubarak ambayo raia walikuwa wanaandamana wakisindikizwa na vifaru?
 
Hivi huyu ngwajima aliwaponyokaje askariiii?,
inapofikia mchungaji anakuwa na mbinu za kijeshi kuwapita makachero wetu,hatari sana
 
Polisi wamsaka Gwajima....Polisi wamuhoji Zitto, Polisi wazuia maandamano Pemba, Polisi watangaza kuzuia mikutano ya kisiasa nchi nzima, Polisi wazingira hoteli ambayo ACT wangelifanyia mkutano wa bajeti, Polisi wamkamata kijana aliyemuita rais "Bwege", Polisi wawatawanya wanafunzi wa UDOM waliohudhuria mahafali ya CHASO katika hoteli moja huko Dodoma, Polisi wazuia msafara wa Maalim Seif, Polisi.....Polisi....Polisi!!!!!!!????????

Ukiona kila taarifa ya habari inaanza na Polisi, jua tayari tumeingia kwenye...........

Kwa hisani ya Mtatiro
Hali ni mbaya sana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mzee Mwanakijiji aliamini CCJ kinge make noise 2010....

So there you have it!


Mimi nilifikiri njia rahisi ya kuongoza ni kuwapa watu enough space ya kuondoa stress zao zote
maandamano,mikutano....we unawaachia tu

JK alikuwa anaita 'upepo tu utapiita'....

Sasa nashangaa Magufuli halijui hili
 
Hivi toka lini mtu akawa dikteta wakati anajua baada ya miaka kumi atarudi uraiani? Magufuli sheria mnalinda, nyie kama mna hoja mpingeni kwa hoja siyo kulalama kama watoto wadogo
 
Back
Top Bottom