Maalim Seif ni mahaba

Rubawa

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2015
Messages
1,397
Points
2,000

Rubawa

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2015
1,397 2,000
Maalim Seif ni mahaba

Na Ahmed Rajab

KUNA aina ya mapenzi, aina ya mahaba, ambayo ni taabu kuyaelezea. Ni mahaba yenye kutia wazimu kama yale ya Layla na Majnun, wapenzi waliotungiwa mashairi katika fasihi za Kifarsi na Kiarabu mnamo karne ya 12.

Yote hayo yamenijia nilipokuwa nikifikiria jinsi apendwavyo Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa katibu mkuu wa zamani na mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Wananchi (CUF). Mapenzi hayo ni mwiba wenye kukichoma Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali zake mbili.

Ni jambo lenye kuwashangaza wengi kwamba juu ya kuonewa na watawala baada ya kupokonywa ushindi katika uchaguzi wa urais wa Zanzibar 2015 na juu ya ahadi chungu nzima alizozitoa tangu hapo bado wafuasi wake wana imani naye. Wanamuamini na wanazidi kumpenda.

Inaweza kuwa Watanzania wenye kumpenda mwanasiasa huyo wanampenda yeye mwenyewe binafsi kama Seif Sharif Hamad. Lakini zaidi nadhani wanampenda kwa msimamo wake wa kuwa imara kupigania haki na kuwa tayari kujitolea muhanga.

Miaka yote hii tangu afukuzwe CCM ameendelea kuwa alama ya mapambano ya kupigania haki, usawa na demokrasia ya kweli. Wenye kumpenda wameonyesha mahaba makubwa kwake.

Na tukiwaangalia Wazanzibari ambao ni kama uti wa mgongo wa ufuasi alionao tunaona kwamba kwao yeye ni alama ya kitu kilicho adhimu zaidi ya hayo. Ni alama ya kupigania nchi yao isimezwe lakini iwe na usawa na Tanganyika katika muungano wa mfumo utaoirejeshea Zanzibar mamlaka yake na uungwana wake. Hayo ni mahaba ya daraja ya juu.

Nguvu kubwa ya Maalim ni umma alionao. Mara tu baada ya kuamua kuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo umma huo kwa kauli moja ulimwambia: “Ulipo tupo”. Mkururo wa wanachama wa zamani wa CUF waliomuunga mkono umekishtua chama cha CCM na serikali zake.
Hivi karibuni tumeona jinsi Edward Lowassa alivyokiacha mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilichompokea alipoondoka CCM baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Kuna tofauti kubwa baina ya Lowassa “kurudi kwao CCM” na Maalim kuhamia ACT-Wazalendo.

Lowassa alirudi CCM yeye na familia yake peke yao. Maalim amekwenda ACT-Wazalendo na umma mzima wa wafuasi wake wote. Haijawahi kutokea katika historia ya kisiasa ya Tanzania kuona umati mkubwa wa wanachama wa chama kimoja wakihamia chama kingine kwa mpigo kama huo tena katika muda usiozidi hata dakika 10 tangu kiongozi wao kukihama chama chao cha zamani.
Bila ya shaka tukio hilo limetuma ujumbe mzito kwa watawala wa Zanzibar na wa Muungano ambao ikiwa wao ni watu wenye kutafakari lazima wakiri kuwa wanapaswa kuuacha mwenendo wao wa kuikandamiza demokrasia.

Ni jambo lisilo na shaka kwamba Maalim Seif ana ule unaoelezewa na wanasosiolojia kuwa ni uongozi wa haiba. Aina hiyo ya uongozi unaochangia kumvutia kwa umma.

Kwa sasa ameitumia uzuri haiba hiyo katika kukata uamuzi ambao wengi wanaouona kuwa ni wa busara wa kukata uamuzi wa kuacha kuking’ang’ania chama cha CUF na, badala yake, kujiunga na ACT-Wazalendo. Amejiunga na chama kichanga lakini kikakamavu chini ya mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe.

Viongozi imara daima huwa tayari kukata uamuzi mgumu na kujitolea muhanga ili wayakidhi matakwa ya umma wanaouongoza. Sifa hizo Maalim na Zitto wanazo.

Lakini mchakato uliohitimika kwa Maalim na wafuasi wake kuwasili ACT-Wazalendo ni mchakato wa muda mrefu. Ulianza hata kabla ya Maalum kupigwa pute na kupokonywa ushindi wa uchaguzi wa urais wa 2015.
Mchakato huo uliendelea na kumalizikia baada ya mkutano wa vyama vya upinzani uliofanywa kwenye hoteli ya Verde, Zanzibar.
Ulianza, kwa hakika, tangu Profesa Ibrahim Lipumba, aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, alipowasaliti wenzake na kujiuzulu ghafla katika wakati nyeti wa uchaguzi uliopita na Dk. Wilbrod Slaa, aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, kukiacha mkono chama chake.
Duru za uchunguzi za ndani ya CUF zilikuwa zishachoshwa na vitimbi vya Lipumba na baadhi ya washirika wake katika serikali ya Muungano na hata ndani ya upande wa CUF wa Zanzibar.
Intelijensia ya CUF ilikwishamuonyesha Maalim jinsi watawala walivyopanga kula njama za kukiua chama cha CUF upande wenye kumuunga mkono yeye.

Kazi ikawa kuandaa lisilofikiriwa: namna ya kuchupa kutoka CUF inayozamishwa na Lipumba kwa msaada wa watawala na kujiunga kwingine kuendelea na mapambano.
Pamoja na kuendelea kumfuatilia Lipumba na washirika wake wa ndani na nje ya chama hicho, pakaundwa kwa siri kubwa tume mbili za uchunguzi ndani ya CUF.

Tume moja ilifanya utafiti wa kina kuhusu vyama vya upinzani kuzitathmini sifa zao njema na taksiri zao. Ulikuwa zaidi ni utafiti wa kisiasa.
Tume ya pili ilitathmini intelijensia ya vyama vya upinzani. Vyama ambavyo Maalim alivipa kipaumbele vilikuwa vyama vyilivyounda mwavuli wa Ukawa kuanzia Chadema na nje ya Ukawa hata chama cha ACT-Wazalendo kilipigwa darubini.
Pakaamuliwa orodha fupi aliyokabidhiwa Maalim ya vyama vya kuzingatiwa. Vyama hivyo vilikuwa Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD chini ya Emmanuel Makaidi na ACT-Wazalendo.
Mchujo uliofuatia hapo ulivibakisha NLD na ACT-Wazalendo. Na mchujo wa mwisho kabisa uliibakisha ACT-Wazalendo kuwa ndio chama cha kuungana nacho.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa nilizonazo ni kuwa intelijensia ya wote waliokuwa wakimshauri Maalim, ndani na nje ya CUF, ikionyesha wazi kwamba chama cha kuungana nacho ni ACT-Wazalendo.
Na hayo licha ya kwamba wakati wa ule utafiti wa kina wa tume za uchunguzi ni ACT-Wazalendo iliyoendewa mwisho kupigwa darubini.
Taarifa za kiuchunguzi zinasema kwamba wakati wote huo Maalim na viongozi wa juu wa CUF/Zanzibar wakimkingia kifua Lipumba. Kila walichokuwa wakielezwa kuhusu vitimbi vya Lipumba wao walikuwa hawaamini. Baadhi yao walikubali kwamba kweli Lipumba alikuwa mkorofi lakini hawakuamini mambo waliyoambiwa kwamba alikuwa akiyafanya.

Wakati huo wapinzani kama akina Zitto na hata viongozi wachache wa CCM wenye kutaka demokrasia ya kweli isimame Tanzania walifanya juhudi za siri za kuleta suluhu baina ya Lipumba na Maalim kabla ya mambo kuzidi kuchacha. Nimeambiwa kwamba wakati wote Lipumba akiwapiga chenga.

Kazi ya Maalim na wafuasi wake waliohamia ACT-Wazalendo ndiyo kwanza inaanza upya huku wakikabiliwa na changamoto nyingi.
Moja ya changamoto hizo kwa sàsa ni kuungwa mkono na kukubaliwa na wanachama wa maeneo tofauti ya Bara.
Changamoto nyingine ni namna ya kujikinga na shari za CCM na serikali zao. Kwa hilo watabidi waandae mkakati wa kujiepusha wasiwe kila mara wanaangushwa ovyo na njama za watawala.

Nadhani changamoto kubwa zaidi ni vipi chama hicho kitaweza kufikia malengo ambayo awali yalishindwa kufikiwa na CUF likiwemo suala la kushinda na kuongoza serikali Zanzibar.
Tunaona tayari kina Musa Haji Kombo, mmoja wa wafuasi wakubwa wa Lipumba, wanaitaka serikali ikipige marufuku chama cha ACT-Wazalendo.

Waziri wa mambo ya Ndani Kangi Lugola alitua Zanzibar Jumapili na kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya ACT-Wazalendo. Hatua hiyo bila ya shaka itazidi kuifanya CCM na serikali ya Muungano zichukize machoni mwa Wazanzibari.

Jambo moja lililotumiwa na dola kupitia Lipumba ni mianya iliyokuwamo katika katiba ya CUF. Kwa hivyo, kuna haja kubwa ya kuifuma upya, tena vizuri, katiba ya ACT-Wazalendo ili isitoe mianya kwa maadui wa chama hicho. Kwa mfano, kiongozi akitangaza kuwa anajiuzulu huo ndio uwe mwisho wake. Isikilazimu chama kuitisha mkutano mkuu kwa gharama ya zaidi ya TSh milioni 800 ili kukubali kujiuzulu kwake.
Jingine ni “kutahadhari kabla ya athari,” kukata maamuzi mapema kabla ya kuangukiwa na janga. CUF ingefanya maamuzi mapema ya kumalizana na Lipumba ingeinyima dola nafasi ya kuendeleza migogoro ya ndani ya chama hicho.
CCM ina uhodari wa kuwatega viongozi wa upinzani. Ndiyo maana haishangazi kuwaona waliokuwa viongozi wa vyama tofauti vya upinzani Mkumbo (ACT-Wazalendo) na Julius Mtatiro (aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, upande wa Maalim Seif) waliokuwa wakiparurana na kukashifiana hadharani hivi sasa wote wametua CCM bukheri wa salmin.

Hali iliyozuka sasa ina maana kubwa kwa siasa za mabadiliko Tanzania. Tunaweza kusema kwamba tangu wiki iliyopita kumeibuka ACT-Wazalendo ambayo itakuwa ngome muhimu katika siasa za Tanzania kuliko hata ilivyokuwa CUF.

Faraghani baadhi ya wana CCM kindakindaki huko Zanzibar wanakiri kwamba wanakabiliwa na mtihani mgumu. Wanazungumzia juu ya kuzorota kwa chama chao visiwani humo na kuzidi kufukuta kwa mivutano ya ndani kwa ndani.
Kingine kilicho wazi ni kuwa CUF sasa imejimaliza yenyewe kisiasa ikisaidiwa na watawala na vyombo vya dola. Lipumba na katibu wake mkuu, Khalifa Suleiman Khalifa, hawafui dafu visiwani na hasa Pemba.

Kutanda kwa ukimya miongoni mwa viongozi wa CCM/Zanzibar kunaonyesha kama viongozi hao wamepigwa na bumbuwazi.
Tukio hili la kuzidi kutiwa pumzi gurudumu la mageuzi la ACT-Wazalendo liwe onyo kwa watawala wa Tanzania. Wasigande katika ile kauli yao ya kila siku: “Hapa hayo hayatokei.” Huko ni kujidanganya

Kuna siku mambo yatabadilika Tanzania nzima. Yatabadilika kwa sababu lazima yabadilike.

Baruapepe: mailto:aamahmedrajab@icloud.com" \t "_blank"aamahmedrajab@icloud.com;

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mfianchi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
9,332
Points
2,000

mfianchi

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
9,332 2,000

Mpemba mwenzake Maalim,nani asiyejua mwenyewe una mahaba na Maalim,rudi nyumbani kumenoga ,unachonga ukiwa ugenini halafu unajifnya unayajua ya huku ,kama una ujasiri rudi badala ya kusikiliza simulizi ukiwa kwenye flats huko UK
 
kichwa mbovu

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
710
Points
1,000

kichwa mbovu

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
710 1,000
Mpemba mwenzake Maalim,nani asiyejua mwenyewe una mahaba na Maalim,rudi nyumbani kumenoga ,unachonga ukiwa ugenini halafu unajifnya unayajua ya huku ,kama una ujasiri rudi badala ya kusikiliza simulizi ukiwa kwenye flats huko UK
Umeelew lakini? Au unataka nawe kwenda Uk ukaishi kwenye hizo flats

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,379,304
Members 525,377
Posts 33,742,048
Top