Polisi wahaha kufuta ushahidi wa bomu na risasi

Polisi wahaha kufuta ushahidi wa bomu na risasi

na zilizo kuwa uploaded kwenye online servers wanakuomba password wadelete?? jeshi linafanya kazi kizamani sana:becky:
 
Masikini polisi, wanafanya kazi kizamani sana! Hawajui kuwa watu wana akaunti zao kwenye mitandao yote ya hapa duniani, kama vile You tube, Yahoo na mingine mingi, ambako ndiko vitu kama hivyo huhifadhiwa. Zaidi ya picha kama hizo za kwenye memory card, siku hizi watu wanahifadhi vyeti vyao (scanned) na CV zao huko mitandaoni ili kuepuka kutembea na bahasha za vyeti kizamani. Ukikutana na nafasi ya kazi kokote uliko duniani una apply na kuambatisha vyeti na cv on the spot, tena online. Hawa polisi wanachekesha eeh. Anyway waacheni hivyo hivyo waendelee kuingia chaka.
 
CHADEMA wanawapeleka mchaka mchaka polisi tu, hawana mkanda unaoonesha mlipuaji wa bomu AR!
 
Mpiga Picha Dennis aliyekamatwa na polisi na kunyang'anywa camera, laptop, Memory Cards amefunguliwa kesi ya mauaji.
Serikali ya ccm inajaribu kutumia nguvu nyingi kutaka kuondoa tention ya watubwa Arusha kuwa serikali na polisi hawahusiki kulipua bomu na kupiga risasi raia wasio na hatia.
Watahangaika sana hata wamesahau kuwa kuna Mungu!!!
 
wanatoa maelezo gan wanapowapekua? na wanakuja na search warranty?...na wanashikiliwa kwa charges gan?

kama wao ni dola unafikiri watakosa sababu ya kukupa?
 
Waje kwangu niwape ili waone aibu...

Lakini wao nao ni wazembe kweli! Mbona siku ile walikuwepo kwenye gari lao pale uwanjani, ina maana hawana hata simu zenye kamera kurekodi matukio!:clap2:
Post yako imenichekesha sana....
 
Cdm wanatumia teknolojia ya kisasa kuna kila sababu jeshi la polisi likaangaliwa ,mfumo wake na uadilifu
 
Yaani imeshakula kwao.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
CHADEMA wanawapeleka mchaka mchaka polisi tu, hawana mkanda unaoonesha mlipuaji wa bomu AR!

Mbona ushahidi umewekwa facebook watu wamem tag Chagonja na Mwema
 
Polisi mkoani Arusha wakishirikiana na kikosi kilichoundwa kufatilia swala la bomu na risasi walizofurumishiwa wana chadema tarehe 15.06.2013 zilizopelekea vifo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 70, leo wameanza msako wa kukamata wapiga picha wote ambao huonekana kwenye mikutano ya chadema na kila wanapo kukamata wana enda kwako kupekua na kuchukua memory card, flash, cd na kama una komputer wanabeba, mpka sasa wapiga picha wawili wamesha kamatwa.....


Hawana lolote. Wasubiri tu kuvuliwa nguo pamoja na Savimbi Nchemba aliyewatuma..
 
Tatizo la Polisi wetu wanafanya kazi kama hawajaisomea. Kama vile wanakurupushwa tu!!
 
Kwa staili hiyo ndo watake kumlinda obama?-Majanga kwa kweli

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kweli ukistaajabu ya musa utaona ya firauni,Police badala ya kumtafuta Aliyelipua bomu wanatafuta wapiga picha
 
Back
Top Bottom