IGP Sirro, angalia Polisi wako wa Arusha Wanavyo lazimisha Rushwa kwa Kushirikiana na Mgambo

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,495
3,458
TUKIO LA WAANDISHI WA HABARI KUKAMATWA NA KUPEWA KESI YA MCHONGO ARUSHA.

Waandishi wa Habari wawili wa vyombo vya Habari tofauti mmoja Korumba Victor Moshi na Wa Global Tv na Alphonce Kusaga Wa Tripal A Redio wote wa Mkaoni Arusha walikamatwa na jeshi la polisi mkoani Arusha wakiwa wanafatilia tukio la Askari wanaoshirikiana na Migambo kuwakamata Raia na kiwabambikizia kesi katika kituo kidogo cha Polisi Sakina Kilichopo jijini Arusha.

Waandiashi hao wa habari walipigiwa Simu na wananchi wakilalamikia vitendo vya Askari wa jeshi la polisi kuwakamata hasa dereva bodaboda wakiwa wamepakia abiria huwa wanawasimamisha na kuwasachi wateja wao kwanguvu na kuwapeleka kituoni sakina bila kiwaeleza makosa yao.

Waandishi hao wa habari baada ya kifika eno la tukio laska zone jijini Arusha ilipopigwa Simu na wananchi walikutana na wananchi hao waliopiga Simu na kuaanza kuwafanyia mahojiano.

Wananchi wakaanza kifunguka wapo walioelezea jinsi walivyo kamatwa Kama dereva bodaboda bila makosa na kupelekwa kwenye kituo hicho cha sakina na Kunyolewa Nywele Kichwani na Ndevu na mikasi na kuonyesha Makovu ya vidonda vilivyotokana na vipigo hivyo huku wakieleza kuwa walikuwa wakilazimishwa wakiwa ndani kuvua Nguo na kupigwa makofi ya migongoni na kukanyagwa kwenye unyanyo na Mabuti ya Askari hao.

Tukio la mwisho walilolielezea walilolishuhudia madereva bodaboda wote likitokea tarehe 23.2.2022 kijana Mmoja alishushwa kwenye Bodaboda akiwa Kama Abiria na Askari hao kijana Huyo alifahamika kwa jina la Idi Abdalah baada ya kushushwa akiwa amepakiwa kwenye pikiki na Askari hao Wa kituo cha polisi cha Sakina wakiwa na Migambo kwa Ku block Pikipiki aliyokuwa ameipanda akaambiwa ashuke
Kijana yule akawauliza nyinyi nikinanani yakiwa ni majira ya saa 2 kasoro usiku.Wale watu walio walio wablock kwa Pikipiki tatu aina ya boxer kwa mbele na pembani wakajibu sisi ni Askari Inamaana hutujui?
Yule kijana Iddi akawaambia nawaomba mnionyeshe vitambulisho vyenu

Baada ya kusema hivyo ikawa kosa wakamnyanyua juujuu huku wakimpiga na kumwambia ametukana Askari wakamfaulishia kwenye Pikipiki yao moja na kuondoka nae hadi kituoni kufika kituoni ikawa nikipigo ndugu zake walipomfata kituoni wakaambiwa walipe laki moja ndo aachiwe wakatoa elfu 90 ndo akachiwa huku kichwani akiwa ameshanholewa nywele zake kichwani na mkasi maana wakati wanamkamata alikuwa namenyoa Aflo.

Baada ya waandishi kuwasikiliza wananchi wakampigia Simu kamanda Wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo simu yake ilipokelewa na Msaidi wake aliyesema kuwa RPC yupo kisongo anazindua kituo cha Polisi akimaliza atamwambia ataturejea.

Waandishi wakiwa eneo la Tukio Askari waliokuwa wakituhumiwa kuwanyanyasa Raia wakapita eneo lile wakiwa Doria Kama kawaida yao na Pikipiki mbili wamepakiana wawiliwawili baada ya kupita waandishi wakawasimamisha wakiwa kwenye Pikipiki zao na wakajitambulisha kwao kuwa wao ni waandishi wa habari wapo pale wananchi wana malalamiko dhidi yao ya kuwapiga na kuwatengenezea kesi je wao ni Askari momoja akajibu kuwa wao ni Askari mwingine akajibu hapana sisi ni Mg yani Migambo.

Waandishi wakawaambia basi Kama ni migambo tusaidieni Ku balance story maana mnalalmikiwa na hawa wananchi hapa.Mwandishi wa Global Tv Korumba akatoa Kamera iliyokuwa kwenye gari alipotoa waliokuwa kwenye Pikipiki wote wakakimbia akabaki mmoja aliyekuwa ameshuka pale akizungumza na waandishi wa habari na aliyejitambulisha awali kuwa yeye ni Askari Polisi
Yule askari akawaambia waandishi Kama mnataka niongee tuvuke ale ng'ambo ya lami hapa wananchi wameshakuwa jamu maaana wananchi walishaanza kuzunguka na kuzomea wakisema sio Askari.

Waandishi wa Habari hao wawili wakavuka lami mkononi wakiwa na Camera yao walipovuka tu
Yuke kijana aliyejitambulisha ni Askari akasema twendeni pale kituoni nikaongelee pale kituoni waandishi wakamakatalia na kumwambi mwenye mamlaka ya kuongelea kituoni ni RPC peke yake hatuwezi kwenda kituoni hapo maana hata mkuu Wa kituo hicho Hana uwezo wakuongelea hili bila kuruhusiwa na RPC na Tayari RPC walishamtafuta.
akatokea Askari mwingine akiwa na nguo za kiraia wakati wakizungumza na yule aliyewaambia wavuke barabara ndo atazungumza baada ya kufika akaukiza kunanini
Yule askari Wa kwanza akamwambia hawa jamaa wanasema wao ni waandishi wa habari wamenipiga picha baada ya kuambiwa hivyo yule askari akamrukia Mwandishi Wa Habari Alphonce Kusaga na Kuaanza kumvuta kumpeleka kituo kidogo cha Pilisi Sakina kilichokuwa pale karibu na yule Askari mwingine akamavaa Korumba na kukamata kamba ya Kamera na kuanza kuivuta kamaera ilikutoiharibu kamera yake Mwandishi huyo alivutwa hadi ndani ya kituo cha polisi Sakina baada ya kuingia ndani Askari waliokuwemo mle ndani akiiwemo askari wa kike walikafungua sero zao na kutaka Korumba Aiingie .

Korumba akawa bado ameng'ang'ani kamera yake akajitambukisha kwa Askari polisi aliowakuta pale ndani jamani Mimi nimwandishi Wa habari huyu bwana anninyang'anya kamera yangu.Baada ya kusema hivyo yule askari wakike akamvaa Korumba na kusema Kama ni mwandishi Wa habari leta simu utaturekodi akamsachi mifukoni kwake huku akifanyamu kuwa ni udhalilishaji na nikosa Asikari Wa kike kumpekua Mwanaume maungoni Akachukua Simu yake.

Korumba Kituoni akaendelea kuwaeleza wale polisi kuwa hii kamera inachukuliwa mbele yanu na nyinyi mpo nipora muichukue nyie lakini sio huyu ambae sina uhakika Kama ni polisi yule askari wa kike na mmoja wakiume wakamwambia muachie hiyo kamara huyo nae ni polisi mbona Korumba akataka kamera hiyo aandikiwe maelezo ya kuchukuliwa kwa kamera hiyo kama ambavyo sheria ina taka lakini hakuna aliyaejali hilo. Wakamakata na kuukunja mkono wake na kumpora kamera hiyo huku mwenzake Kusaga akiwa amebananishwa kwenye kona ya Mlango wa kituo hicho cha polisi na Asikari mmoja.

Yule Askari mwanamke akapiga Simu ndani ya Dakika chache Gari za polisi mbili zikafika pale kituoni zikiwa na Askari zaidi ya 11 baada ya kuingia pale ndani wakanza kumpiga makofi Mwandishi Wa habari Kusaga Korumba Akawaambia mnampiga kwa kosa Gani huyo siyo Muhalifu baada ya Kusema hivyo wakamuacha na kumfata yeye wakachika shati yake na kumchania vifungo vyote huku wakimtishi kumfanyia kitu kibaya akae chini na asiongee kitu .

Korumba akakataa akasema hawezi kukaa chini ahadi ambiwe kosa lake nilipi baada yakusema hivyo wakawatoa mkukumkuku na kuwaambia watoke nje wakapande kwenye magari wapelekwe central polisi.
Waandishi hao wakawaeleza viongozi Waliokuja na polisi hao kuwa simu zao zipo hapo kituoni na kamera ikiwa na riciver ya Mic.wakajibiwa watavichukuwa kwa Afande OCD.
Wakwanza kutolewa alikwa ni Korumba akalazimishwa kuingia nyuma ya buti ya gari akagoma maana ilikuwa nisemu ndogo sana inatosha kukaa spea tairi ya gari tena ikiwa imesimama ndani alimuona mtu mmoja akiwa anatoka damu amejikunja kwenye sehemu hiyo baada ya kukataa akaaza kupigwa sehemu za mbavu na usoni na askari waliokuwa wakijiita chita huku wakimtukana mbele ya viongozi wa Askari hao ambao kwenye mavazi yao walikuwa wananyota tatu mmoja Jina lake kwenye sare zao hizo aliseomeka Jumbe Mwingine alisomeka Mbiwe.

Katika purukushani hizo korumba alijeruhiwa wenye kidole cha chake mkono wa kulia kucha ilichimbika nusura inyofolewe na damu zilikuwa zikimtoka kwenye kidole hicho.
Kwa mangumi na mateke na makofi wakafanikiwa kumsukuma na kuingia kwenye buti huyo ya Gari.

Mwandishi mwingine Kusaga walipomleta apande na yeye kwenye buti hiyo pakawa hakuna nafasi ikabidi wawashushe Korumba na yule mtu mwingine aliyekuwa kwenye buti aleyekuwa akiuja damu usoni na kuwahamishia mbele ya gari hiyo ya polisi na kuwekwe nyuma ya siti za gari hilo.

Mwisho wa Safari ukawa kituo cha polisi Central Arusha OCD Muchunguzi akaagiza wafunguliwe jarada la Uchunguzi Wa kufanya fujo kituo cha Polisi na kutaka kuchoma moto kituo hicho cha sakina.

Waandishi hao wakachukuliwa maelezo chini ya wakili wao na kuchukuliwa dhamana kwa kufata taratibu za kisheria baada ya kupata watu walio wadhamini huku wakisubiria jarada la uchunguzi polisi dhidi ya tuhuma zao likamilike.
Katika tukio hilo waandishi hao simu zao zimevunjwa na vifaa vingine kupotea Kama vile riciver na Betry ya Camera.

Pia, soma:

1). Taarifa za kukamatwa kwa waandishi wa habari jijini Arusha

2). Polisi Arusha: Ufafanuzi kuhusiana na tukio la waandishi wawili wa habari wa Global TV na Tripple A kukamatwa
 
Toka nivifahu vyombo vya usalama:
Sijawahi kuona chombo hata kimoja kinachopenda kufuatiliwa-fuatiliwa na raia katika kutekeleza majukumu yake!
Hawapendi mnooo!!!
 
Inaonekana hiyo ndio M.O. ya polisi na watawala Bongo toka awamu ya 5. Kimsingi pambaneni tu, maana mko wenyewe.
 
kwamba mwenye mamlaka ya kuongelea kituoni Ni RPC peke yake!
Je hao waandishi hawakujua Kama askari wa kawaida Hana mamlaka yoyote ya kujibu chochote anapohojiwa na waandishi wa habari sababu Ni jukumu la msemaji wa jeshi la polisi wa sehemu husika!? Walitaka wamuhoji mtaani barabarani? Hawana akili
 
Poleni kwani hapo Arusha hamna IPID kwenye vituo vya polisi?malalamiko haya hawa IPID ndio majukumu yao maana police hapo ni suspects.....KATIBA MPYA NDIO NJIA PEKEE.
 
Nchi ya ajabu sana. Kwamba kuna Rais wa nchi, waziri wa mambo ya ndani, RPC, OCD nk na polisi hawa wanafanya yote haya kama maelekezo yao halali?

Kwamba hawataki wajibika milele?

La msingi ni kusubiria kuona.
 
Polisi Arusha zile gari zao ni maduka makubwa ya jumla hawana tofauti na Sabaya ipo landcruiser moja kiongozi wao mmasai wana michongo ya kujifanya kukagua mashine na risiti za TRA ili mradi wapate rushwa kubwa tuu wanawaonea sana wafanyabiara wa Chuga...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom