Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kupiga marufu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo wameandamana.

Maandamano ya CCM yamefanyika jijini Mwanza. Yameanzia katika Kata ya Mahina na kwenda kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Barabara ya Nyerere kisha kupokelewa na Idd Mkowa, Katibu wa CCM Wilaya.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi nchini lilipiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa kwa kile ilichodai kutokuwepo kwa hali nzuri ya usalama jambo ambalo limeibua mjadala kitaifa.

Hatua ya polisi kuzuia mikutano hiyo ilitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano ya hadhara ya kuishtaki serikali kwa wananchi kutokana na kuendesha nchi bila kufuata kanuni na sheria pamoja na kuzuia kuoneshwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Hata hivyo, baada ya Chadema kutangaza kufanya oparesheni hiyo iliopewa jina la ‘Okoa Demokrasia Nchini’ Polisi kupitia kwa Kamishna wa Mafunzo wa Polisi, ilizuia kufanyika kwa mikutano hiyo kwa kile ilichodai, hali ya usalama kuwa tete nchini.

Kutokana na zuio hilo, Chadema chini ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kimekwenda mahakamani kuwashitaki Wakuu wa Polisi wa Wilaya za Geita na Kahama, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi Makao Makuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pamoja na kuwepo kwa katazo hilo, leo wafuasi wa chama tawala (CCM) wameandamana kwa madai kuwa James Bwire, Diwani wa Kata ya Mahina ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mwanza ananyanyaswa pia kutishiwa kuuawa na baadhi ya madiwani na watumishi wa jiji hilo ambao hawakutajwa majina.

Wanachama na wafuasi hao waliandamana wakiwa na mabango huku wakiimba nyimbo za chama hicho. Kwenye maandamano hayo polisi hawakuingilia kati.

Maandamano hayo yaliongozwa na Felician Balukali, Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mahina na Teleza Chacha, Katibu wa CCM wa kata hiyo.

“Tunataka diwani wetu (James Bwire) awaachie umeya wao abaki kuwa diwani wa kushughulikia matatizo yetu, kwa nini anyanyaswe kama shida ni uongozi wao wabaki nao waendeleo nao,” amesema Chacha.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa wanahabari leo amedai kuwa, hana taarifa za tukio hilo na kwamba, polisi hawapo kwa ajili ya kukibeba chama chochote cha siasa licha ya kushindwa kuyazuia maandamano hayo.

Msangi ambaye pia ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) amesema, ” kwanza hilo tukio silifahamu ndio nasikia kutoka kwenu, nitalifuatilia kwa ukaribu na polisi hatupo kwa ajili ya kukilinda chama chochote kile cha siasa,” amesema.
Hawaja chemka. Huo ndio muendelezo wa ukandamizaji wa upinzani. Yaani kama Chadema walusimama kusakimiana na wafuasi wao wakawekwa selo itakuwa watu kuandamana na mabango polisi hawajui?? Aibu jamani.
 
Mkuu ni kweli <UKWELI SIKU ZOTE UTATUWEKA HURU> Lakini si hiki ulichokileta hapa ambacho hakina kithibitisho chochote zaidi ya maneno uliyoaandika ukiwa CHUMBANI.....TUPIA PICHA ZA HAYO MAANDAMANO unayoita ni ya CCM hapa MWANZA...

Hivi unaishi sayari gani?
 
Hii ingekuwa ni ukawa hasa Chadema...hapo angekufa mtu?...maana polis wangepiga wauwe
 
Nimeangali taarifa ya habari ya ITV saa 2 usiku pamoja na ile ya Star tv kuhusu kile kinachodaiwa ni wafuasi wa CCM kuandamana huko mkoani Mwanza.

Star tv hawajasema kama wafuasi hao wa CCM wameandamana badala yake wameonyesha picha za wafuasi hao wakiwa wamekusanyika katika ofisi za CCM huko Mwanza.

ITV,kwa upande wao wameripoti kuwa wafuasi hao wa CCM wameandamana kwa aina yake kwa kukodi magari (magari 3 kama sikosei) mpaka katika ofisi hizo za CCM.

Maswali:
1.ITV,kusafiri kwa magari ya kukodi ndio kuandamana?

2.Je,inawezekana ITV mkawa mmeripoti tukio hili pasipo ukamilifu wake?

3.Star tv,nanyi hamjasema kama waliandamana au laa,je ukweli ni upi?

4.ITV,nimewasikia mkiripoti kumuhoji RPC wa Mwanza kuhusu maandamano hayo.Sasa ITV, mnaweza kweli kumuhoji RPC kuhusu maandamano kama kweli walisafiri kwa magari na si kuandamaa barabarani?

Bahati mbaya hata maelezo ya RPC mliyoyatoa nilishindwa kuyaelewa kama ndio yalikuwa mahususi yanajibu swali hilo au ndio alikuwa anatoa tu maelezo ya jumla kuhusu tukio zima maana sikumsikia akitamka neno maandamano.

Kwa taarifa,katika moja ya kituo cha tv kati ya hivi viwili nilivyovitaja hapa (sikumbuji ni kipi) wafuasi hawa wa CCM wameonekana kukusanyika huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Ninachojouliza,mabango bila kuandamana inawezekana?

Je,ndio tuseme mabango yale yalikusudiwa kuonyeshwa katika ofisi za CCM tu na si huko walikopita?

Naona tusubiri magazeti ya kesho labda ndio yataweka wazi ni nini hasa kilitokea huko Mwanza.
 
Mkuu uzi wako umeleta saa kumi na mbili jioni na taarifa ya HABARI chanel ten ni saa moja hivyo moja kwa moja wewe ndio primary source kuu ya information humu JF sasa tunategemea uje na full evidance na si kuniuliza nimeangalia taarifa chanel ten
Azam Tv,ITV na Channel 10 wameonesha...ushaidi tosha na mungu akipenda kesho front page ndio habari kuu
 
ITV wapo kwenya payroll ya mzee wa mamvi so lazima wajitutumue ili kulipa fadhila
 
Kama hiyo kauli kweli imetolewa na RPC, basi nchi hii tuna watu wa ajabu kupindukia. Hata kama ni uswahiba wake na CCM, basi angetafuta jibu la kutumia akili japo kwa kiwango kidogo. RPC, yanafanyika maandamano mpaka yanaisha, unasema hukuwa na taarifa! Hivi unataka uletewe taarifa na nani? Watu wanaandamana barabarani huna taarifa, je, wizi unaofanyika ndani ya nyumba za watu, utaweza kuwapata majambazi?
 
Habari hii imethibitishwa? Watu wanajua kulaumu bila kuwa na facts hivi ikiwa RPC amejibu kwamba hana taarifa unawezaje kumlaumu bila Ushahidi?
a9ee2d8066c60295b54eee8c7b58cb69.jpg

Hiyo hapo
 
Wanahabari hawajui maandamano ni nini. Inasikitisha sana. Uchunguzi lazima ufanywe kujua lengo la huyu mwandishi kuita hili kusanyiko ni maandamano huku kashindwa kutuonesha hata mita ishirini ya watu wakitembea bali ni kutuonesha wakiinua mabango yao wakiwa ofisi za chama cha mapinduzi. Kama lengo lake ni kuuhabarisha umma kuwa polisi wanaupendeleo wakati si kweli hatua kali lazima zichukuliwe dhidi ya mwanahabari huyu.

Hata mimi nimeshangaa mno...Kichwa cha habari kinasema maandamano lakini maelezo ni tofauti...Hata ITV walisema ni maandamano, lakini maelezo yake ni kwamba wale wanachama wa CCM kumbe walikodisha daladala tatu wakatoka huko walikokuwa wakaenda walikopanga kwenda na kuteremka ndipowalipoingia ofisini wakiwa na mabango yao...sasa hayo sijui ni maandamano kweli au nini sijui...Nadhani hizi propaganda zitatuua mwaka huu...Lakini kama kweli hayo ni maandamano basi ni vema polisi wachukue hatua kwa wahusika kwani itatuletea shida zisizo na msingi....
 
Back
Top Bottom