Katambi: Ukitaka kuandamana, katoe taarifa Polisi

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,738
Reaction score
42,830
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amezungumzia utaratibu wa maandamano na mikusanyiko ya hadhara kwa mujibu wa Katiba na Sheria, ikiwemo wajibu wa kutoa taarifa kwa Kituo cha Polisi saa 48 kabla ya kuandamana.

Akizungumza leo Julai 2, 2026, Jijini Dar es salaam, Katambi amesema kwa mujibu wa Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura ya 322 kwa kuzingatia matakwa ya vifungu vya 42, 43, 44, 45 na 46 vya Sheria hiyo.

“Utaratibu wa maandamano na mikusanyiko ya hadhara ni lazima uzingatie masharti yaliyowekwa katika kifungu cha 42 kinacholipa Jeshi la Polisi mamlaka ya kusimamia na kuratibu mikusanyiko yoyote Nchini, sambamba na hilo kifungu cha 43 kinaeleza kuwa Mtu au Waandaaji wanaotaka kufanya mikusanyiko au maandamano katika maeneo ya umma wanapaswa kuwasilisha taarifa ya maandishi kwa Mkuu wa Polisi saa 48 kabla ya tukio,” amesema Katambi.

Kauli ya Katambi inakuja baada ya kuibuka kwa utata kuhusu maagizo yake ya kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kuzuia vibali vya mikutano ya Vyama vya Siasa.

Amefuta mikutano ya siasa. Anarudi na kusema ukitaka kuandamana omba kibali. Kweli kachanganyikiwa.
 
Je vipi wale watakao taka kutoa kwako mojakwa moja?
 
Back
Top Bottom