Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kupiga marufu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo wameandamana.

Maandamano ya CCM yamefanyika jijini Mwanza. Yameanzia katika Kata ya Mahina na kwenda kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Barabara ya Nyerere kisha kupokelewa na Idd Mkowa, Katibu wa CCM Wilaya.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi nchini lilipiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa kwa kile ilichodai kutokuwepo kwa hali nzuri ya usalama jambo ambalo limeibua mjadala kitaifa.

Hatua ya polisi kuzuia mikutano hiyo ilitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano ya hadhara ya kuishtaki serikali kwa wananchi kutokana na kuendesha nchi bila kufuata kanuni na sheria pamoja na kuzuia kuoneshwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Hata hivyo, baada ya Chadema kutangaza kufanya oparesheni hiyo iliopewa jina la ‘Okoa Demokrasia Nchini’ Polisi kupitia kwa Kamishna wa Mafunzo wa Polisi, ilizuia kufanyika kwa mikutano hiyo kwa kile ilichodai, hali ya usalama kuwa tete nchini.

Kutokana na zuio hilo, Chadema chini ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kimekwenda mahakamani kuwashitaki Wakuu wa Polisi wa Wilaya za Geita na Kahama, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi Makao Makuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pamoja na kuwepo kwa katazo hilo, leo wafuasi wa chama tawala (CCM) wameandamana kwa madai kuwa James Bwire, Diwani wa Kata ya Mahina ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mwanza ananyanyaswa pia kutishiwa kuuawa na baadhi ya madiwani na watumishi wa jiji hilo ambao hawakutajwa majina.

Wanachama na wafuasi hao waliandamana wakiwa na mabango huku wakiimba nyimbo za chama hicho. Kwenye maandamano hayo polisi hawakuingilia kati.

Maandamano hayo yaliongozwa na Felician Balukali, Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mahina na Teleza Chacha, Katibu wa CCM wa kata hiyo.

“Tunataka diwani wetu (James Bwire) awaachie umeya wao abaki kuwa diwani wa kushughulikia matatizo yetu, kwa nini anyanyaswe kama shida ni uongozi wao wabaki nao waendeleo nao,” amesema Chacha.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa wanahabari leo amedai kuwa, hana taarifa za tukio hilo na kwamba, polisi hawapo kwa ajili ya kukibeba chama chochote cha siasa licha ya kushindwa kuyazuia maandamano hayo.

Msangi ambaye pia ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) amesema, ” kwanza hilo tukio silifahamu ndio nasikia kutoka kwenu, nitalifuatilia kwa ukaribu na polisi hatupo kwa ajili ya kukilinda chama chochote kile cha siasa,” amesema.
IMG-20160614-WA0073.jpg
 
Msangi anajulikana alikotoka hadi hapo alipo....nini accelerator yake kufika hapo inajulikana! Hana lolote awezalo kufanya! Aibu imemjaa hata week bado double standard imemuumbua! Mchumia tumbo number 1 ndani ya jeshi la Polisi!.....Siku si nyingi watagombana na RC wake maana wote wajuaji! Tuone........sham on you RPC
 
Hizi Taarifa za Kiintelijensia za Jeshi la Polisi huwa ni kwa vyama vya Upinzani pekee yake? Mbona maandamano ya Chama Cha Majipu/Magamba (CCM) hizo intelijensia hupoteza dira?!?

Katika Serikali inayojinasibu "Hapa Kazi Tu" RPC kushindwa kujua yamefanyika maandamano au la, ni Uzembe wa hali ya juu!

Na kama kweli alikuwa hajui, basi Chama Cha Majipu (CCM) kishtakiwe kwa kuendesha maandamano bila kibali cha Polisi.

Haya yanawezekana tu, katika nchi isiyofuata Misingi ya Utawala wa Sheria, Haki na Usawa.
 
Msangi anajulikana alikotoka hadi hapo alipo....nini accelerator yake kufika hapo inajulikana! Hana lolote awezalo kufanya! Aibu imemjaa hata week bado double standard imemuumbua! Mchumia tumbo number 1 ndani ya jeshi la Polisi!.....Siku si nyingi watagombana na RC wake maana wote wajuaji! Tuone........sham on you RPC
Huyo RPC sidhani kama kichwa chake kizima. Anajibu lightly tu kuwa hajui?? Kweli? atakuwa kajaza nyama kichwani na wala siyo akili
 
Back
Top Bottom