Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

RPC aneonyesha upendeleo wa wazi anatakiwa arejeshwe wizarani aende kule zimamoto.
 
Hatuwezi kukubaliana na hii Double standard.Wacha na sisi tuitishe maandamano tuone
 
Wakati mwingine jamani muwe watu wa ukweli tu. Kamanda Msangi ni mtu msikivu sana na mweledi kabisa. Kosa la Mh Mbowe ni kutangaza kibabe kuwa anaenda mitaani kuishitaki serekali. Hilo ni kosa tiyari. Huwezi kuishitaki serekali inayo kuongoza. CCM hawakutangaza, waliingia tu kitaa na mabango yao bila kusema mwisho wao ni wapi hivyo Kabla Kamanda hajaamka wao wakawa tiyari weshamaliza kusudi lao.
Chadema, msitangaze nia yenu, temeni cheche ondokeni. Jigaweni kikanda, temeni cheche siku moja wote. Mkija zuiwa mmekwishafikisha ujumbe wenu.
 
Kwanza jiulize ccm walikuwa wanaandamana kwenda wapi?..
 
Huyo RPC arejeshwe wizarani aende akasome magazeti maana huu unafiki wake umepitliza
Uzuri waliombeba wote hawapo ulingoni! Mwema Kova na JK...wote out! Wanamchukia sana sababu amebebwa sana na ameruka levels kibao
 
Halafu eti wanadanganya watu wameandamana kwa kukodi daladala tatu! ha ha ha ha hivi intelejensia ya jeshimletu la polisi ni kunusa wapinzani tu?
 
Acheni kukurupuka wapi wameandamana.. walichofanya wao ni kukodi daladala kama tatu hivi mpaka ofisi ya chama na sio kufanya maandamano
 
Mkono wa chuma kandamiza demokrasia sitaki kusikia wapinzani! Tupa huko! Hii nchi si ya watu wachache au kanda maalum....ya ziwa! Nchi ya watu wote unatengeneza kitu kibaya sana yeye anajua hakuna w kumuuliza ila anaharibu kabisa mfumo mzuri uliokuwepo! Nchi yaenda kwa hisia na visasi vya wazi na mwendo kasi wa kukurupuka!! Labd kama hakujiandaa kuwa Rais
 
Wala usitegemee ajiuzulu, wala usitegemee ccm kupigwa mabomu hata wakiandamana kwenda ikulu, tatizo hapa ni mfumo na tafsiri ya demokrasia ya vyama vingi,, kwanza ni vigumu sana kuona mipaka ipo wapi kati ya serikali na CCM ndio maana hata bungeni wabunge wa ccm badala ya kuisimamia na kuikosoa serikali kwa mujibu wa sheria wanaitetea na kujihisi ni sehemu ya serikali mifano ipo mingi hapo sasa ndio vyombo vya dola hasa polisi vinaichukulia ccm kama sehemu ya dola. Pili vyombo vya dola hasa polisi na wanaccm wengi hata viongozi wanachukulia kuwa upinzani ni uadui tena mkubwa ndio maana wapinzani wakiandamana au kufanya chochote wanapigwa wanauaawa na kutendewa unyama wa kila aina kwa kuwa wanachukuliwa ni maadui wa dola na ccm! Sijui ni elimu gani itatolewa ili watu wajue kuwa vyama vingi vilianzishwa kwa mujibu wa sheria 1992 na upinzani ni mawazo mbadala wa serikali iliyopo madarakani
 
maandamano ya kata! we call this peripheral politics. That was ward level butter and bread politics a reasonable policeman could politely ignore.
Utaongea hadi kichina leo ,
Kwani maamndamano ya level ya kata sio maandamano ya kisiasa yaliyopigwa marufuku nchi nzima?
 
Uzuri waliombeba wote hawapo ulingoni! Mwema Kova na JK...wote out! Wanamchukia sana sababu amebebwa sana na ameruka levels kibao
Mwema ana jipu la Lugumi na kova ana jipu la makontena na ile nyumba aliyompora yule Nzowa, hana mtetezi ajiandae kurejeshwa wizarani kusoma magazeti au atahamishiwa lindi au Rukwa akapambane na wajanja wa vijijini.
 
Huyo kamanda anasema hujui ina maana intelijensia haifanyi kazi?
Intelijensia yao inafanya kazi kwenye mikutano ya Chadema tu?
That's not right
 
Intelejensia ilikuwa wapi jamani toka kata ya mahina unapita kata takribani nne au tatu hadi kufika ilipo ofisi ya ccm Nyamagana.

Unapita kata ya Igoma.....kata ya nyakato.....kata ya mabati then kata ya pamba (hapa ndipo zilipo ofisi za ccm nyamagana)..

Intelejensia haahaaa[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Li nchi lilishakua la kijinga kijinga hili! Yaani polisi wanajua hata saa mwenyekiti wa CHADEMA atafika Shinyanga wanaweka ulinzi kumzuia asiingie ofisini, lakini haya ya kijani yanaandamana katikati ya mji eti mjinga mmoja anakuja kudai hana taarifa?
 
kudadadek..
inanikumbusha TALLYING STATION ya UKAWA oct.2015 ilivyosombwa na jeshi la CCM sijui na kuwekwa ndani na computer zao huku TALLYING STATION za CCM zikiendelea kupeta na takwimu za uchaguzi..
 
Back
Top Bottom