Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Msangi anajulikana alikotoka hadi hapo alipo....nini accelerator yake kufika hapo inajulikana! Hana lolote awezalo kufanya! Aibu imemjaa hata week bado double standard imemuumbua! Mchumia tumbo number 1 ndani ya jeshi la Polisi!.....Siku si nyingi watagombana na RC wake maana wote wajuaji! Tuone........sham on you RPC
Mungu ampe nguvu Dr Ulimboka .
 
hongera wanachama wachache wa ccm kwa kuanza kuamka huo ni mwanzo mzuri na wengine fateni nyayo za wenzenu ili kulinda na kutetea democrasia ya kweli msiwaachie upinzani tu kwani ni jukumu lenu pia kukemea palipo na dosari. ccm msilale lale lale bado mapambano.
 
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kupiga marufu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo wameandamana.

Maandamano ya CCM yamefanyika jijini Mwanza. Yameanzia katika Kata ya Mahina na kwenda kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Barabara ya Nyerere kisha kupokelewa na Idd Mkowa, Katibu wa CCM Wilaya.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi nchini lilipiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa kwa kile ilichodai kutokuwepo kwa hali nzuri ya usalama jambo ambalo limeibua mjadala kitaifa.

Hatua ya polisi kuzuia mikutano hiyo ilitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano ya hadhara ya kuishtaki serikali kwa wananchi kutokana na kuendesha nchi bila kufuata kanuni na sheria pamoja na kuzuia kuoneshwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Hata hivyo, baada ya Chadema kutangaza kufanya oparesheni hiyo iliopewa jina la ‘Okoa Demokrasia Nchini’ Polisi kupitia kwa Kamishna wa Mafunzo wa Polisi, ilizuia kufanyika kwa mikutano hiyo kwa kile ilichodai, hali ya usalama kuwa tete nchini.

Kutokana na zuio hilo, Chadema chini ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kimekwenda mahakamani kuwashitaki Wakuu wa Polisi wa Wilaya za Geita na Kahama, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi Makao Makuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pamoja na kuwepo kwa katazo hilo, leo wafuasi wa chama tawala (CCM) wameandamana kwa madai kuwa James Bwire, Diwani wa Kata ya Mahina ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mwanza ananyanyaswa pia kutishiwa kuuawa na baadhi ya madiwani na watumishi wa jiji hilo ambao hawakutajwa majina.

Wanachama na wafuasi hao waliandamana wakiwa na mabango huku wakiimba nyimbo za chama hicho. Kwenye maandamano hayo polisi hawakuingilia kati.

Maandamano hayo yaliongozwa na Felician Balukali, Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mahina na Teleza Chacha, Katibu wa CCM wa kata hiyo.

“Tunataka diwani wetu (James Bwire) awaachie umeya wao abaki kuwa diwani wa kushughulikia matatizo yetu, kwa nini anyanyaswe kama shida ni uongozi wao wabaki nao waendeleo nao,” amesema Chacha.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa wanahabari leo amedai kuwa, hana taarifa za tukio hilo na kwamba, polisi hawapo kwa ajili ya kukibeba chama chochote cha siasa licha ya kushindwa kuyazuia maandamano hayo.

Msangi ambaye pia ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) amesema, ” kwanza hilo tukio silifahamu ndio nasikia kutoka kwenu, nitalifuatilia kwa ukaribu na polisi hatupo kwa ajili ya kukilinda chama chochote kile cha siasa,” amesema.
Wanahabari hawajui maandamano ni nini. Inasikitisha sana. Uchunguzi lazima ufanywe kujua lengo la huyu mwandishi kuita hili kusanyiko ni maandamano huku kashindwa kutuonesha hata mita ishirini ya watu wakitembea bali ni kutuonesha wakiinua mabango yao wakiwa ofisi za chama cha mapinduzi. Kama lengo lake ni kuuhabarisha umma kuwa polisi wanaupendeleo wakati si kweli hatua kali lazima zichukuliwe dhidi ya mwanahabari huyu.
 
Mbona hilo linaeleweka kwani unadhani RPC nae haogopi amri ikitoka juu..."eti sina taarifa kama kuna tukio kama hilo"
Hivi maandamano si yanahitaji kibali? Kilitolewa na nani kama polisi hawajui? Je Ccm wanaweza kwenda kinyume cha sheria za nchi na kuihujumu serkali yao wenyewe??
 
Wanahabari hawajui maandamano ni nini. Inasikitisha sana. Uchunguzi lazima ufanywe kujua lengo la huyu mwandishi kuita hili kusanyiko ni maandamano huku kashindwa kutuonesha hata mita ishirini ya watu wakitembea bali ni kutuonesha wakiinua mabango yao wakiwa ofisi za chama cha mapinduzi. Kama lengo lake ni kuuhabarisha umma kuwa polisi wanaupendeleo wakati si kweli hatua kali lazima zichukuliwe dhidi ya mwanahabari huyu.
Hujielewi wewe kabisa.. bora kunyamaza kuliko kujidhalilisha
 
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kupiga marufu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo wameandamana.

Maandamano ya CCM yamefanyika jijini Mwanza. Yameanzia katika Kata ya Mahina na kwenda kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Barabara ya Nyerere kisha kupokelewa na Idd Mkowa, Katibu wa CCM Wilaya.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi nchini lilipiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa kwa kile ilichodai kutokuwepo kwa hali nzuri ya usalama jambo ambalo limeibua mjadala kitaifa.

Hatua ya polisi kuzuia mikutano hiyo ilitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano ya hadhara ya kuishtaki serikali kwa wananchi kutokana na kuendesha nchi bila kufuata kanuni na sheria pamoja na kuzuia kuoneshwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Hata hivyo, baada ya Chadema kutangaza kufanya oparesheni hiyo iliopewa jina la ‘Okoa Demokrasia Nchini’ Polisi kupitia kwa Kamishna wa Mafunzo wa Polisi, ilizuia kufanyika kwa mikutano hiyo kwa kile ilichodai, hali ya usalama kuwa tete nchini.

Kutokana na zuio hilo, Chadema chini ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kimekwenda mahakamani kuwashitaki Wakuu wa Polisi wa Wilaya za Geita na Kahama, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi Makao Makuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pamoja na kuwepo kwa katazo hilo, leo wafuasi wa chama tawala (CCM) wameandamana kwa madai kuwa James Bwire, Diwani wa Kata ya Mahina ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mwanza ananyanyaswa pia kutishiwa kuuawa na baadhi ya madiwani na watumishi wa jiji hilo ambao hawakutajwa majina.

Wanachama na wafuasi hao waliandamana wakiwa na mabango huku wakiimba nyimbo za chama hicho. Kwenye maandamano hayo polisi hawakuingilia kati.

Maandamano hayo yaliongozwa na Felician Balukali, Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mahina na Teleza Chacha, Katibu wa CCM wa kata hiyo.

“Tunataka diwani wetu (James Bwire) awaachie umeya wao abaki kuwa diwani wa kushughulikia matatizo yetu, kwa nini anyanyaswe kama shida ni uongozi wao wabaki nao waendeleo nao,” amesema Chacha.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa wanahabari leo amedai kuwa, hana taarifa za tukio hilo na kwamba, polisi hawapo kwa ajili ya kukibeba chama chochote cha siasa licha ya kushindwa kuyazuia maandamano hayo.

Msangi ambaye pia ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) amesema, ” kwanza hilo tukio silifahamu ndio nasikia kutoka kwenu, nitalifuatilia kwa ukaribu na polisi hatupo kwa ajili ya kukilinda chama chochote kile cha siasa,” amesema.
Kaka unaaa utakusaidia nini humu jukwaani na makala ndefu ukikwepa ukweli? Je hii ndio freedom of expression kujenga chuki baina ya jamii?
Ukweli ITV imerusha Habari hiyo. Jamaa waliwapiga chenga jeshi La polisi kwa kupanda hiace mpaka eneo la tukio.
Acha ujuha kijana.
Hata chadema waki apply hii method police watachemka.
Ukweli utakuweka huru, Acha mbinu taka kuhalalisha upuuzi wako.
 
Kumbe walikodi haisi tatu toka Mahina mpaka hapo ofisini na walipomalizana na viongozi wao wakakwea haisi zao bila hata kutembea mita ishirini.

Hayo maandamano yamefanyikia barabara gani?

Naona ITV imemuumbua huyu mleta udaku.

Yaani watembee kutoka Mahina hadi Nyerere road na kusiwepo picha ya tukio mitandaoni?
 
Kaka unaaa utakusaidia nini humu jukwaani na makala ndefu ukikwepa ukweli? Je hii ndio freedom of expression kujenga chuki baina ya jamii?
Ukweli ITV imerusha Habari hiyo. Jamaa waliwapiga chenga jeshi La polisi kwa kupanda hiace mpaka eneo la tukio.
Acha ujuha kijana.
Hata chadema waki apply hii method police watachemka.
Ukweli utakuweka huru, Acha mbinu taka kuhalalisha upuuzi wako.
Walifanyanini mpaka kufika pale walipofika wacha ujuha
 
Suala no maandamano kuzuiliwa haijalishi ya amani au ya nini jamani CCM mwogopeni mungu
 
Kueleza nini zaidi ya hiki hapa?
Kumbe ulinielewa kiasi cha kutokuwa na hoja za kupinga nilichoandika!! Haya ukipata ushahidi wa maandamano utatuonesha. Kilichoonekana ni mkusanyiko wa wanaccm wakiwa na mabango kwenye ofisi yao.
Wanachadema huwa hamjui kuteua maneno ya kuwasilisha taarifa zenu kwa makusudi au kwa kutokujua. Mlichokiandika maandamano si maandamano.
 
Kumbe ni mkusanyiko maana huo uliruhusiwa
 
Back
Top Bottom