Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Polisi wachemka, CCM waandamana Mwanza

Umeipenda mwenyewe...... Chaguo lako milele..... Nauvimbe upasuke...... Utajijua mwenyewe...... Acha uisomenamba eeeeee.... Sisiemu mbele kwa mbele......,.. Najaribu kufukuza mende kwenye spika yangu msinitolee mimacho.
 
Hata mimi nimeshangaa mno...Kichwa cha habari kinasema maandamano lakini maelezo ni tofauti...Hata ITV walisema ni maandamano, lakini maelezo yake ni kwamba wale wanachama wa CCM kumbe walikodisha daladala tatu wakatoka huko walikokuwa wakaenda walikopanga kwenda na kuteremka ndipowalipoingia ofisini wakiwa na mabango yao...sasa hayo sijui ni maandamano kweli au nini sijui...Nadhani hizi propaganda zitatuua mwaka huu...Lakini kama kweli hayo ni maandamano basi ni vema polisi wachukue hatua kwa wahusika kwani itatuletea shida zisizo na msingi....

Lakini anayepita ofisini kusaini na kufanya mikutano yandani yeye anafanya Fuji na sharti intelijensia ing'amue na iact siyo ????!!! Nchi ya wehu hii
 
Hata mimi nimeshangaa mno...Kichwa cha habari kinasema maandamano lakini maelezo ni tofauti...Hata ITV walisema ni maandamano, lakini maelezo yake ni kwamba wale wanachama wa CCM kumbe walikodisha daladala tatu wakatoka huko walikokuwa wakaenda walikopanga kwenda na kuteremka ndipowalipoingia ofisini wakiwa na mabango yao...sasa hayo sijui ni maandamano kweli au nini sijui...Nadhani hizi propaganda zitatuua mwaka huu...Lakini kama kweli hayo ni maandamano basi ni vema polisi wachukue hatua kwa wahusika kwani itatuletea shida zisizo na msingi....
Ni kuwahoji ili tujue nia yao ilikuwa ni ipi? Au wanaufinyu wa msamiati wa lugha ya kiswahili katika kuzungumzia swala husika.
 
Kuongoza nchi kunaitaji umakini sana hakuna anayependa kuonewa hata kidogo.
Hawa wanaandamana...wale no. Nani atavumilia hii!!
 
kama wamekwenda ofisi za chama chao haina shida. Nyumbu lazima wauze sura mtaani kulazimisha bodaboda,mama ntilie n.k waandamane! wazuiwe ru hamna namna nyingine.
 
Wala hawajachemka chama chao hawawezi wala hawana ubavu huo mbona hawakuwafuata kule ofisini wapinzani wangedhibitiwa hizo daladala zingekamatwa na wangelala polisi kwa kufanya mkusanyiko usiokuwa halali jamani kuweni wakweli tu upinzani hautakiwi awamu hii
 
Intelijensia ipo kwaajili ya wapinzani. Acha tuone cinema zao.
 
Ewe mungu muumba tuokoe na udhalimu wa kccm tunatabika sana wanatunyanyasa japo namba tunaisoma wote ila wao walipenda.
 
Binafsi siwezi kutofautisha kati ya CCM na Policcm
 
Hivi wale waliopigwa mabomu uwanjani Kahama walikuwa wamekusanyika au walikuwa kwenye maandamano?! Huko Shinyanga viongozi wa upinzani walipozuiwa kwenda kwenye ofisi za chama chao kusaini walikuwa kwenye magari au walikuwa wanaandamana?! Walipokamatwa kwa kusalimiana na watu kwenye vijiwe vyao walikuwa wameandamana kwa miguu?! ACT juzi wamezuiwa kufanya kongamano lao, walikuwa wanaandamana wapi?!
Mkisema kwa kupanda hiace hawajaandamana, Lipumba amewahi kushushwa kutoka kwenye gari, akapigwa na polisi haohao kwa kutuhumiwa kuwa ameandamana!
 

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kupiga marufu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchini, wafuasi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo wameandamana.

Maandamano ya CCM yamefanyika jijini Mwanza. Yameanzia katika Kata ya Mahina na kwenda kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Barabara ya Nyerere kisha kupokelewa na Idd Mkowa, Katibu wa CCM Wilaya.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi nchini lilipiga marufuku maandamano na mikutano ya vyama vya siasa kwa kile ilichodai kutokuwepo kwa hali nzuri ya usalama jambo ambalo limeibua mjadala kitaifa.

Hatua ya polisi kuzuia mikutano hiyo ilitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano ya hadhara ya kuishtaki serikali kwa wananchi kutokana na kuendesha nchi bila kufuata kanuni na sheria pamoja na kuzuia kuoneshwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Hata hivyo, baada ya Chadema kutangaza kufanya oparesheni hiyo iliopewa jina la ‘Okoa Demokrasia Nchini’ Polisi kupitia kwa Kamishna wa Mafunzo wa Polisi, ilizuia kufanyika kwa mikutano hiyo kwa kile ilichodai, hali ya usalama kuwa tete nchini.

Kutokana na zuio hilo, Chadema chini ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kimekwenda mahakamani kuwashitaki Wakuu wa Polisi wa Wilaya za Geita na Kahama, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi Makao Makuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pamoja na kuwepo kwa katazo hilo, leo wafuasi wa chama tawala (CCM) wameandamana kwa madai kuwa James Bwire, Diwani wa Kata ya Mahina ambaye pia ni Meya wa Jiji la Mwanza ananyanyaswa pia kutishiwa kuuawa na baadhi ya madiwani na watumishi wa jiji hilo ambao hawakutajwa majina.

Wanachama na wafuasi hao waliandamana wakiwa na mabango huku wakiimba nyimbo za chama hicho. Kwenye maandamano hayo polisi hawakuingilia kati.

Maandamano hayo yaliongozwa na Felician Balukali, Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Mahina na Teleza Chacha, Katibu wa CCM wa kata hiyo.

“Tunataka diwani wetu (James Bwire) awaachie umeya wao abaki kuwa diwani wa kushughulikia matatizo yetu, kwa nini anyanyaswe kama shida ni uongozi wao wabaki nao waendeleo nao,” amesema Chacha.

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza akizungumza na waandishi wa wanahabari leo amedai kuwa, hana taarifa za tukio hilo na kwamba, polisi hawapo kwa ajili ya kukibeba chama chochote cha siasa licha ya kushindwa kuyazuia maandamano hayo.

Msangi ambaye pia ni Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) amesema, ” kwanza hilo tukio silifahamu ndio nasikia kutoka kwenu, nitalifuatilia kwa ukaribu na polisi hatupo kwa ajili ya kukilinda chama chochote kile cha siasa,” amesema.
View attachment 356584

VIP ndugu hao walioandama hakuna aliyekamatwa kwa kuvunja amri ya jeshi la polisi? Hakuna aliyepigwa mabomu? Kama hakuna basi jeshi la polisi itabidi lijitathimi upya kama kweli ni jeshi la polisi au chama
 
Kama hiyo kauli kweli imetolewa na RPC, basi nchi hii tuna watu wa ajabu kupindukia. Hata kama ni uswahiba wake na CCM, basi angetafuta jibu la kutumia akili japo kwa kiwango kidogo. RPC, yanafanyika maandamano mpaka yanaisha, unasema hukuwa na taarifa! Hivi unataka uletewe taarifa na nani? Watu wanaandamana barabarani huna taarifa, je, wizi unaofanyika ndani ya nyumba za watu, utaweza kuwapata majambazi?
Umechelewa Sana mkuu kujua kuwa nchi hii Ina watu wa ajabu kupindukia!!
 
Sometimez nachekaga sana maana hizi njaa zinatulesi vibaya hivi na wale waliomsapoti yure kajanja kure buguruni sijui walipewa ngapi jamaan tupeni hiyo michongo mie hata nguo nitavua barabarani kumsapoti mtu
 
Ccm wanajua kuandamana kwa amani,

Hapo ingekuwa machadema watu wangefanyiwa fujo na kulazimishwa kuandamana
ungekaa kimya ungeonekana una busara kuliko kuandika kitu ka hichi inaonyesha jinsi ufahamu wako ulivo
 
Back
Top Bottom